SIKU ZA MEYA WA JIJI LA ARUSHA KALIST LAZARO ZAHESABIKA. GODBLESS LEMA

kunena

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
506
711
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amerejea katika kikao cha kamati ya fedha kwa mara ya kwanza tangu aende gerezani karibu miezi 8 iliyopita na kuvuruga hali ya hewa. Katika kikao hicho maalum cha kupitia taarifa ya mkaguzi wa hesabu, mbunge huyo alimwambia meya Kalisti Bukhay Lazaro kuwa" wewe hii ni mara ya mwisho siku zako zinahesabika huna uwezo kabisa wa kuiongoza halmashauri hii na kama huna misimamo tuachie halmashauri yetu"Lema alisema meya huyo ameshindwa kumdhibiti mkurugenzi wa jiji hilo Athumani Kihamia pamoja na washirika wake. Ambapo naibu meya amesema kamati yao imechoshwa na mkurugenzi huyo ambaye anataka kamati ifuate mawazo yake tu badala ya maamuzi ya kamati, analolitaka lazima litekelezwa hii haikubaliki. Lema amesema mkurugenzi amefikia hapo kwa sababu ya udhaifu wa meya ambaye ameshindwa kabisa kumsimamia mkurugenzi huyo ambaye kimsingi ni dikteta. Hali hiyo ilikuwa aibu sana kwa Meya ambaye alidhalilishwa na mbunge huyo mbele ya watumishi wa halmashauri pamoja na wataalam wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha. Kabla ya kikao cha hicho hapo jana kulikuwa na kikao cha madiwani ambapo nusura diwani wa Levolosi ndg Nanyaro Efatha akunjane ngumi na diwani mwenye utata Doita Isaya baada ya kumkejeli diwani mwenzake huyo.
 
Wee kinena a.k.a Mrisho Gambo uchonganishi wako umechelewa
 
Back
Top Bottom