Siku za Mapumziko TZ zimewekwa kisiasa - zinadidimiza uchumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku za Mapumziko TZ zimewekwa kisiasa - zinadidimiza uchumi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Apr 25, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Siku za mapumziko rasmi Tanzania ni mzigo kiuchumi kwa vile siku hizo zimeakisiwa kisiasa zaidi kuliko kiuchumi. Madhara yake kiuchumi ni makubwa kwa nchi inayohangaikia kujikwamua ili kukuza uchumi wa taifa.

  Mzigo huo wa siku za mapumziko unazikumba zaidi sekta binafsi wakati serikali haioni tatizo kwa vile sekta binafsi na wananchi lazima walipe kodi. Serikali ina uhakika wa kukinga pesa lakini si wananchi na makampuni binafsi. Lakini serikali haitilii maanani uchungu wa sekta binafsi wanapowalipa watu siku za mapumziko ambazo mwajiriwa hazalishi.

  Wawekezaji moja ya malalamiko wanayotoa ni pamoja na utitiri wa siku za mapumziko nchini ambazo mfanyakazi lazima alipwe tofauti na mfumo wa kuhesabu masaa kazini ambao hutumiwa na mataifa tajiri duniani. Kwa utaratibu wa kulipwa kwa saa unafaa kwa secta binafsi kwa vile siku ambazo ambayo mtu hayupo kazini halipwi na kunakuwa na makubaliano ya sikukuu ambazo mwajiriwa atakuwa analipwa.

  Utaratibu wa siku za mapumziko unatakiwa uangaliwe upya na kufanya mfumo wa sikukuu za lazima ambazo hata sekta binafsi zinawajibika na sikukuu ambazo sekta binafsi ni huru ila zinatambuliwa na serikali. Hii itasaidia kupunguza makali ya waajiri. Sikukuu nyingi zinabaki kama kumbukumbu kitaifa tu lakini si siku za mapumziko.

  Mfano Marekani kuna sikukuu karibu 15 hivi na kati ya hizo sekta binafsi zinawajibika kuwalipa wafanyakazi ni kuanzia tano na baada ya tano ni hiari kampuni kuongeza, isipokuwa serikalini zipo kama 12 hivi na nyingine ni kumbukumbu tu ambazo hazina uzito wa mapumziko ya kazi. Sherehe ambayo ina hadhi ya mapumziko huhamishiwa mwanzoni au mwishoni mwa wiki kwa vile kupumzika katikati ya wiki huvuruga mtiririko wa uzalishaji viwandani na sehemu nyingine za kazi. Na pia mapumziko yanapopelekwa mwanzoni au mwishoni mwa juma pamoja na siku za weekend mtu anaonja kama mepata likizo kwa vile weekend kurefushwa na holiday.

  Tanzania kila sikukuu ni sherehe ya daraja la kwanza na ni mapumziko nchi nzima, hali hii wawakilishi wetu hawaoni, na serikali haitambui hasara ipatikanayo na utitiri wa siku za mapumzi? Siku za mapumziko nyingi mno na ni hasara kwa sekta binafsi na ukuaji wa uchumi wa taifa ambao msingi ni watu binafsi na makampuni binafsi baada ya kubinafsishwa.
   
 2. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe lalama kadiri utakavyo lakini usiguse Ijumaa Kuu, Jumapili ya Paska na Jumatatu ya Paska.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mfano mimi siona umuhimu wa Mapumziko ya Jumatatu ya Pasaka wakati kulikuwa na mapumziko mengine ya Pasaka Ijumaa Kuu. Hali kadhalika mapumziko ya Iddi pili na X-mas box Desember 26. Mapumziko mengine kama Nyerere day, siku ya wakulima, nk. zingebaki kama kumbukumbu tu na wala si siku ya kupumzika kazi, labda kwa wafanyakazi wa serikali. lakini sekta binafsi ni hasara.

  Wafanyakazi wengi watapinga kauli hii, lakini wafanyakazi hao hao kesho wakiinuka na kuwa na waajiriwa watageuka na kudai mapumziko nimzigo wa kampuni yake. Tuangalie maslahi kitaifa kwa mapana na marefu, si ridhaa binafsi.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hojatoa hoja ya kuridhisha kuhusu mapumziko ya siku hizo tatu. Kwa uelewa wangu siku rasmi ya mapumziko ya Ijumaa Kuu ni sawa, lakini ile ya Jumatatu ya Pasaka sioni uzioto wake ila tu hasara kiuchumi kwa vile haina umuhimu.
   
 5. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa ni vema wangefuta Nyerere day,karume day, 7-7,8-8,jumatatu ya paska, idi pili, boxing day,9 decmbr wangeifuta tu sbb tunasherekea uhuru wa nchi amabyo ilishafutwa(tanganyika)...Taifa linapata hasara kwa huu utitiri wa sikuku zisizo na tija
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Laiti siku za mapumziko tungezitumia kwa manufaa lakini utaona zinatumika kwa ajili ya starehe na wengi turudipo makazini mifuko imejaa pumzi
   
Loading...