Siku za Humphrey Polepole na wenzake ndani ya CCM zinahesabika

Mwanachama machachali sana ndani ya CCM ndugu Humphrey Polepole a.k.a Comred Polepole pamoja na genge lake lipo hatiani kuondoka ndani ya Chama cha mapinduzi kutokana na kwenda sawa na mfumo wa awamu ya sita...
Bila fitna humo mmh!
 
Sijaona mgogoro wa kumfukuza mtu uanachama hapo!

Labda kama wewe ni mgeni wa siasa za ccm...
Polepole hata akifukuzwa Uanachama, hawezi kupoteza ubunge. Ubunge wake hautokani na nafasi za chama. Bali ni zile nafasi kumi za Rais, ambazo anaweza kuteua mtu yeyote hata asiye na chama au kutoka chama Cha upinzani (rejea Mbatia). Hivo ubunge ni wa miaka Mitano full, mpaka bunge litakapovunjwa au mazingira mengine kabisa.

Mzee wa Asasi za Kiraia, hana cha kupoteza katika ubunge wake. Labda Gwajima, huyo sababu hiyo inaweza kumuondoa Bungeni but siyo Polepole. He is there to stay!
 
Mwanachama machachali sana ndani ya CCM ndugu Humphrey Polepole a.k.a Comred Polepole pamoja na genge lake lipo hatiani kuondoka ndani ya Chama cha mapinduzi kutokana na kwenda sawa na mfumo wa awamu ya sita.

Walifanikiwa kuwakonyeza Watanzania kuwa tupo fiti na tukitaka kupindua tunaweza; hayo walionesha kupitia gazeti la Uhuru la tarehe 11/8/2021.

Humphrey na genge lake ni watu waliopata umaarufu na kuaminiwa sana nyakati za hayati mwendazake JPM, lakini kutoka na mabadiliko ya ghafla yaliyotokea hawa jamaa bado hawaamini kama CCM sio mlengwa wao tena na kwa sababu hiyo basi wanafanya mikakati mingi sana kuna inayoonekana na ile isiyoonekana.

Kutokana na upepo uliopo ndani ya chama cha mapinduzi hata sasa ni dhahiri kuwa wana siku chache sana za kuvumiliwa.
Polepole bado yupo sana CCM!
 
Hebu msomeni hapa kama alivyonukuliwa na Dar Mpya

Polepole_anamtaka_Nini_Mama_yake%F0%9F%98%85%F0%9F%98%85_Tuendelee_kudai_Katiba_Mpya_%23MboweS...jpg
 
Back
Top Bottom