Siku za Humphrey Polepole na wenzake ndani ya CCM zinahesabika

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Mwanachama machachali sana ndani ya CCM ndugu Humphrey Polepole a.k.a Comred Polepole pamoja na genge lake lipo hatiani kuondoka ndani ya Chama cha mapinduzi kutokana na kwenda sawa na mfumo wa awamu ya sita.

Walifanikiwa kuwakonyeza Watanzania kuwa tupo fiti na tukitaka kupindua tunaweza; hayo walionesha kupitia gazeti la Uhuru la tarehe 11/8/2021.

Humphrey na genge lake ni watu waliopata umaarufu na kuaminiwa sana nyakati za hayati mwendazake JPM, lakini kutoka na mabadiliko ya ghafla yaliyotokea hawa jamaa bado hawaamini kama CCM sio mlengwa wao tena na kwa sababu hiyo basi wanafanya mikakati mingi sana kuna inayoonekana na ile isiyoonekana.

Kutokana na upepo uliopo ndani ya chama cha mapinduzi hata sasa ni dhahiri kuwa wana siku chache sana za kuvumiliwa.
 
Sijaona mgogoro wa kumfukuza mtu uanachama hapo!

Labda kama wewe ni mgeni wa siasa za ccm!

Kingine, ccm haiwezi kumfukuza uanachama mtu ambae ni mbunge maana wakifanya hivyo na ubunge unakoma na hiyo itabatilisha hata uwepo wa kina Mdee kule bungeni!

Na ccm haitaki kuinekana ina double standard kwa kipindi hiki cha awamu ya mama
 
Kumfukuza Chakubanga ni rahisi sana hawezi kuwasumbua huyo lakini kumfukuza Gwajiboy akili zinawazunguka. Hivyo Polepole ataponea mgongo wa Gwajiboy. Kwa maoni yangu hawawezi kufukuzwa watatishwa tu waache kumshambulia wa KUDEMKA.
 
Back
Top Bottom