Siku za hivi karibuni Rais Magufuli amekuwa akichangisha watu hela kwenye ziara zake

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
87,597
2,000
Ndg sijaona kosa la mheshimiwa sema bado watu huwa hatujifunzi, wote hao kumbuka anachokifanya anauhakika nacho kwani wengi wao n wateule wake, hebu fikiria mkuu wa mkoa anatoa laki tano kweli yuko serious kisa kujitoa n hiari????? Ni heri mara maelfu anachokifanya Magufuli kuliko overspending ya mambo yasiyo na msingi , maendeleo si lele mama ndio maana muda mwingine lazima utumie mbinu ata ambaxo huumiza mfano wake n kama huo,he is correct and correct in collection of money for projects kama hizo, let him atimize ndoto zake kwa taifa ,

Kwanini ma MC harusini huwa bana sana watu kuchangia kama hili suala ni la hiari????? Hivi wangapi siku hizi tunajua ukienda harusini haya mawazo ya kuchangia ni hiari ya mtu hayapo tena? Sembuse jamn na hili kweeeli???

Narudia tena kwangu mm yuko sahihi !!!

Ana uhakika na nini?

Mtu hata kama mshahara wake ni milioni tano kwa mwezi hiyo haina maana hizo hela zake hazina shughuli.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
87,597
2,000
Hii ni akili ya kimjadala kweli? Mbona kama umelenga kuuvuruga mjadala? Hoja ni nzuri, kama wewe unaona huna cha kuchangia katika mjadala; ni vema ukanyamaza. Mijadala kama hii huongeza thamani katika mambo yanayofanyika na mwisho tunaweza kuwa na namna nzuri ya kupata mafanikio kuliko hivi anavyofanya rais. Hata mimi sijaipenda namna yake ingawa nia yake ni njema.

Afadhali mpo mlio waelewa!
 
ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
9,878
2,000

Nijuavyo mimi suala la kuchangia huwa ni la hiari.

Siku za hivi karibuni Rais Magufuli amekuwa akichangisha watu hela kwenye ziara zake sehemu mbalimbali hapa nchini.

Okay, lengo si baya kwa sababu huwa ni za kusaidia ujenzi wa miradi ya maendeleo. Ila mtindo anaoutumia...hmm! Hapana kwa kweli!

Anakuwa anaanza yeye kuchangia halafu anaanza kuita watu tofauti tofauti waje mbele kuchangia.

Kila anayeenda mbele anatoa ahadi ya mchango wake.

Sasa yeye Magufuli, kwa mfano, mtu akitoa ahadi ya milioni moja, yeye ni kama anakataa halafu anamlazimisha huyo mtu atoe zaidi. Badala ya milioni moja, yeye Rais anamwambia huyo mtoa ahadi atoe milioni mbili.

Hivi sasa kama mtu uwezo wake ndo hiyo milioni moja, kwa nini umlazimishe atoe milioni mbili?

Hapana kwa kweli. Sijapenda kabisa huo mtindo, japo naelewa kuwa lengo lake ni zuri.
Hizo ni ndio sura za udikteta. Yeye anatumia bulungutu LA ikulu, wengine mtajiju.
 
Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
3,619
2,000
Inawezekana wanakuwa wamepewa fungu halafu mtoaji anakuona umebana ,kwanini asilazimishe? Mi nimeona watoto wanapewa hela ya sadaka kanisani wanabana kununua big boom au pipi ya kijiti
 
Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
5,846
2,000
Usishanga ni mtindo uliotoholewa toka makanisa ya Kilutheri.
Bila huo mtindo makanisa yetu ya kilutheri yasinge simama. Anachokifanya Raisi kwenye kuchangisha ni Sahihi kabisa. Maana mfano mtu Kama RPC anajua watu alio nao nyuma na madili anayoyapiga kwa Siku iyo million, ni ela ya mboga na ya dili moja ambayo alikuwa anapeleka kwa Bimdogo kwenda kutanua kwa iyo kusema vile ajakosea tena angemwambia atoe milioni 5. Maana anajua madili ya watu wote, kama Trafiki anasimama apo Magomeni Usalama na Kona ya kwa shekhe Yahaya anapiga zaidi ya laki 7 kwa siku, kwanini asibananishwe atoe izo pesa. Kuwa na Jina (status) mjini lazima uwajibike na sio kulia hooo majukumu, maana hata Mama Ndege nae ana majukumu. Maana kuambiwa uchangie vile haimaanishi kwamba lazima uwe na Cash mkononi unaandika jina unatoa Ndani angalau ya mwezi huo, kwa sababu mtu Kama RP'C iyo milioni, anakopeshwa kuwa na cheo au jina ni ishu sana, lazima uwajibike Ndio Utu uzima huo.
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,072
2,000
Halafu wengi wa wachangiaji hawatoi hela zao mfukoni, Waziri,Mkuu wa mkoa, Mkurugenzi, Mkuu wa wilaya, Mbunge wanaenda kukata mafungu tu ofisini kwao.
Wewe unauwezo wa kutoa mln 1, alafu kwenye mchango unatoa 50000/ hpo hata mm lazima nkulazimishe tu utoe hyo 1mln...

Ova
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
87,597
2,000
Bila huo mtindo makanisa yetu ya kilutheri yasinge simama. Anachokifanya Raisi kwenye kuchangisha ni Sahihi kabisa. Maana mfano mtu Kama RPC anajua watu alio nao nyuma na madili anayoyapiga kwa Siku iyo million, ni ela ya mboga na ya dili moja ambayo alikuwa anapeleka kwa Bimdogo kwenda kutanua kwa iyo kusema vile ajakosea tena angemwambia atoe milioni 5. Maana anajua madili ya watu wote, kama Trafiki anasimama apo Magomeni Usalama na Kona ya kwa shekhe Yahaya anapiga zaidi ya laki 7 kwa siku, kwanini asibananishwe atoe izo pesa. Kuwa na Jina (status) mjini lazima uwajibike na sio kulia hooo majukumu, maana hata Mama Ndege nae ana majukumu. Maana kuambiwa uchangie vile haimaanishi kwamba lazima uwe na Cash mkononi unaandika jina unatoa Ndani angalau ya mwezi huo, kwa sababu mtu Kama RP'C iyo milioni, anakopeshwa kuwa na cheo au jina ni ishu sana, lazima uwajibike Ndio Utu uzima huo.

Kwani kodi zetu kazi yake nini hadi tuanze kuchangishana hadharani namna hiyo?
 
pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
3,981
2,000
Akamwambia RPC toa milioni moja hiyo ukikamata tu mtu na bangi tayari utakua umerudisha hiyo pesa....ni kama kahalalisha rushwa kwa polisi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom