Siku yangu ya kwanza kujiunga JF nilidhani haya

Nilidhani kuwa google ndio JF maana kabla sijaijua JF, nilikuwa kila nikiuliza swali Google, majibu yake yalikuja kwa kumalizia na link ya JF(maana nilikuwa najibiwa na members waliowahi kuchangia kwa majibu yao nayona nikiwa huko huko google hata kama mimi siyo member). nilijua ili nipate jibu la uhakika nilikuwa kama nauliza mbinu za kuwa tajiri namalizia na JF mwishoni mwa swali langu... hali hii ilinifanya niipende JF kuanzia hapo!
 
Mimi wakati naingia JF mwaka 2009 niliambiwa kwamba kila kinachosemwa humu vingi ni ukweli, tena ukweli usiopatikana magazetini.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa ingawa hapa katikati kuliingia vihabari vya uongo kuvunja sifa hii lakini bado kuna ukweli mwingi wa mambo mengi yanayosemwa humu.

Nakumbuka ilikuwa mwaka 2010 nikiwa natumia ID flani maarufu baadae nikaiacha,

Nilipojiunha JF
1. Nilidhani kila anayetumia jina la mwanamke ni demu kweli, na wengine niliwaibukia nkidhani naweza pata mchumba hapa hapa, haha , na mbaya zaid nikaamini kila mmoja ni mrembo

2. Nilidhani kila anayeleta story MMU ni ya kweli kumbe wengine uchangamsha baraza tu

3.Nilidhani kila mtu anayesema mnyetishaji wangu kasema, nikadhani wana access ikulu ama usalama wa taifa kumbe uongo mtupu

4. Nilidhani kila anayesema niko ulaya yupo kweli kumbe wengine ni story but wanasimuliwa wanatuletea,

5. Mbaya zaid nilidhani ........

Je we ulipojiunga JF siku ya kwanza ulikuwa na mawazo gani?
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom