Siku yangu ya kwanza kujiunga JF nilidhani haya

Mi nilidhani wanaume wote Jf wana Choonyonyo (Ndinga) kumbe wengine wanatembelea Rickshaw (Guta).
 
Nilidhani kujiunga Jf ni mpaka uwe na iPhone au Samsung,kujaribu na Tecno Y4 ngoma ikajipa,mpaka sasa naleta thread,na_like na ku_coment kwa raha mustarehe...
 
Nilizani Mzizi mkavu ni mganga kumbe mgangaanjaa tu nilizani Miss chaga ni bonge la mama kumbe kawaida nikazani nyani ngabu ana undugu na lemutuzi kumbe sio.

nilizani Britanica ni mfanya biashara kumbe ni walewale wa tuma kwenye number hii. nilizani lara one ni single kumbe ni mama na mtoto nikazani jamii forum members karibia wote wanaishi njee ya Tz kumbe wengi ni wanafunzi tena st. kayumba na Udom.
 
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2010 nikiwa natumia ID flani maarufu baadae nikaiacha,

Nilipojiunha JF
1. Nilidhani kila anayetumia jina la mwanamke ni demu kweli, na wengine niliwaibukia nkidhani naweza pata mchumba hapa hapa, haha , na mbaya zaid nikaamini kila mmoja ni mrembo

2. Nilidhani kila anayeleta story MMU ni ya kweli kumbe wengine uchangamsha baraza tu

3.Nilidhani kila mtu anayesema mnyetishaji wangu kasema, nikadhani wana access ikulu ama usalama wa taifa kumbe uongo mtupu

4. Nilidhani kila anayesema niko ulaya yupo kweli kumbe wengine ni story but wanasimuliwa wanatuletea,

5. Mbaya zaid nilidhani ........

Je we ulipojiunga JF siku ya kwanza ulikuwa na mawazo gani?
Mimi nilidhani wote ni GT kama wanavyojinasibisha.....
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom