Siku yako ya kuzaliwa halafu mpaka Saa Saba mchana hujaona ujumbe wowote wa kukupongeza kutoka kwa mpenzi wako...

Barakoa

JF-Expert Member
Apr 11, 2020
720
1,298
Tukiwa bado tunaendelea na kupiga nyungu tusisahahau kuendelea kuchukua tahadhari nyingine dhidi ya adui yetu Corona.


Kwa kuwa kila mtu kazaliwa, basi kuna siku moja katika mwaka huwa inajirudia kwa maana ya tarehe na mwezi. Kwa wale wenzetu mliopo kwenye mahusiano, najua inapofika siku kama hii basi huwaga mna shauku kubwa ya kuona ni kwa namna wapenzi wenu wanawajali hasa katika siku muhimu kama hii.

Sasa basi inapofika siku yako ya kuzaliwa Ile saa sita hujapigiwa simu, hujapokea ujumbe wowote kutoka kwake, asubuhi unaamka unakutana na simu au meseji ya kukujulia tu hali, ilhali unapokea salamu kedekede kutoka kwa watu tofauti tofauti.

Huwa unajisikiaje unapokutana na hii hali?
 
Mimi mwaka huu nilikumbuka siku yangu ya kuzaliwa saa 10 jioni.. sasa imagine kama mimi mwenyewe nilikua nimesahau huyo mpenzi anaanzaje kukumbuka..
Mbona tunatwishana mizigo isiyo na muhimu. Yaani mimi nikae mwaka mzima nakumbuka tarehe.. no way nina mambo mengi ya kukumbuka na siku ya kuzaliwa sio priority kabisaa..
 
Ivi watu wako serious kabisa kwamba asipopata wish anakasirika? Mimi mwenyewe hua nashtuliwa na tigo kua ni siku yangu ya iuzaliwa wananipa dk 5 za muda wa maogezi, huwa sifatiliagi hilo suala na hata sihitaji mtu anifatilie kuhusu hilo
 
Kwangu mimi siku yangu ya kuzaliwa hata sitaki watu waijue. Yaani ukipokea zile sms za Happy birthday unasikia vipi kwani?

Sijawahi kuwa serious na hiki kitu naona ni upuuzi mtupu.
Kwetu sisi wanawaume huwa ni kawaida tu. Lakini je na mwenzako nae ( mpenzi) wako ukiichukulia kawaida siku yake unadhani itakuwa kawaida ?
 
Kwetu sisi wanawaume huwa ni kawaida tu. Lakini je na mwenzako nae ( mpenzi) wako ukiichukulia kawaida siku yake unadhani itakuwa kawaida ?
Nimeshamwonesha msimamo wa mambo gani nahusudu na nisiyohusudu hivyo huwa sina muda na kitu cha aina hiyo hata kwake siyo kwangu tu.
 
Mwezi huu trh 10 besidei yangu kabla sijamka nikute mushatuma ma wishez kama yote.

Kubwa zaidi mpesa idhibitishe.........
 
Sijawahi kumuelewa mwanaume mwenzangu anayelilia wishes za siku ya kuzaliwa.
Mimi awish asiwish sijawahi kuona tofauti.
Kwanza hata siikumbukagi
 
Birthday ni mambo ya ma slay queen. Sasa sijui wewe mleta mada ni slay queen underground au Expert Member. ..!
Na ukiona mwanaume anapenda sherehe za birthday jua na yeye ni walewale tu, ni slay queen mwenye ndevu.
 
Back
Top Bottom