Sawa nitaandika nikipata muda kidogoMjukuu hawa sikuwataja kwa kuwa siwajui...
Nakuomba uandike michango yao hata kwa mukhtasari.
Hii ndiyo historia yetu.
Mungu akuweke Shekhe wangu,Mwalim wangu wa historia ya kweli ilotukuka.... Allah atakulipa inshaallah Maandsh yko hayatapotea bureeKipala nimeeleza wapi nimepata picha hii na nyingine labda hukusoma uzi toka mwanzo. Ally Sykes alinikutanisha na Jim Bailey aliyekuwa na mswada wa kitabu cha picha kuhusu Baba wa Taifa. Bailey akaniomba nifanye uhariri wa kitabu chake. Huyu Bailey alikuwa na gazeti lake Drum likichapwa Johannesburg katika miaka ya 1950s. Katika kazi hii ndipo nilipopata picha hii ya 1955. Kulia ni Bi. Chiku Kisusa (Mama Sakina), Bi. Titi Mohamed, huyo wa tatu jina sina wa nne Mwalimu Julius Nyerere wa tano jina sina na wa sita ni Bi. Tatu bint Mzee. Bailey akiniomba pia baada ya kukihariri kitabu nimtafutie publisher. Mimi nikamjulisha Bailey kwa Walter Bgoya wa Mkuki na Nyota ambae ni rafiki yangu wa miaka mingi. Yeye ni publisher wa sifa na kitabu kikachapwa - The Story of Julius Nyerere of Tanzania. Picha hii ni moja picha kutoka Bailey African Collection. Ninazo picha nyingine mkipenda naweza kukuwekeeni hapa pamoja na historia zake.
Alwayz...Mungu akuweke Shekhe wangu,Mwalim wangu wa historia ya kweli ilotukuka.... Allah atakulipa inshaallah Maandsh yko hayatapotea buree