Siku ya wanawake duniani - Tanzania: Nani anawajua wapigania uhuru hawa wanawake?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255

Nani anayajua majina ya wanawake hawa wanne wanachama wa mwanzo wa TANU
na wanawake waliomsindikiza Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Uwanja wa
Ndege wa Dar es Salaam safari ya kwanza UNO 1955?

DSCN1793.JPG

Nani anayajua majina ya wanawake hawa wanachama wa tawi la TANU
Mgomeni Mapipa 1955?

Shariffa bint Mzee

Nani anawajua wapigania uhuru hawa wanawake wafuatao?:
Hawa bint Maftah
Fatuma bint Matola
Dharura bint Abdulrahman
Mama Mwana Mwema
Halima Selengia
Amina Kinabo
Mama bint Maalim
Sharifa bint Mzee
Sakina Arab
(Kuwataja wachache)
 
Umemsahau BIBI TITTI MOHAMMED
Mjukuu...
Hapana Bi. Titi sikumsahau.

Angalia hiyo picha ya Baba wa Taifa ya mwaka wa 1955 amepiga na wanawake
wanne waliomsindikiza Uwanja wa Ndege safari ya UNO...

Bi. Titi yupo hapo ila kwa makusudi sikweka jina kwa kuwa nimeuliza swali, ''Nani
anawajua?''
 
Sawa Babu nimekuelewa
 
Kila Nyerere alipokuja Arusha alifadhiliwa matumizi yake yote kuanza mavazi chakula uandaaji na uhamasishaji wa mikutano mpaka mafuta ya Land Rover yake na marehemu
FATNA BINTI MURSALi
Vivo hivyo alipokwenda Singida hukumu lilimuangukie dada yake marehemu
HAWA BINTI FERUZI
Nakubaliana na mohamed Saidi kwa historia ya kweli kuandikwa
 
Kivava Bi. Fatna na Bi Hawa ni ndugu?
 
Mjukuu...
Hapana Bi. Titi sikumsahau.

Angalia hiyo picha ya Baba wa Taifa ya mwaka wa 1955 amepiga na wanawake
wanne waliomsindikiza Uwanja wa Ndege safari ya UNO...

Bi. Titi yupo hapo ila kwa makusudi sikweka jina kwa kuwa nimeuliza swali, ''Nani
anawajua?''
Mzee wewe ni mpotoshaji namba moja kwanini unaandika ujinga huo

Hao masister wa kikatolic wewe unaandika ujinga kwanini unapotosha mambo Mzee

Wewe hufai kabisa ndani ya jamii ni moja kati ya watu mliopasa kuweko huko Damascus, Allepo au Ghouta mpigwe mabomu ya nguvu huna maana

Masister wakatoliki hao unaleta ujinga na mawazo takataka humu
 
Gussie,
Kwa kawaida na ndiyo ibra ya historia hii mtu akisoma hasa kwa mara ya kwanza
huwa anapandwa na ghadhabu na mara nyingine hunishabulia hadi kwa matusi.

Nasoma lugha yako hapa ya kughadhibika unatumia neno, ''ujinga,'' unaniita ''mzee.''
Hakika mimi ni mzee na kwangu si tusi wiki mbili zilizopiyanimefikisha miaka 66.

Alhamdulilah na nilikuwa nimesahau kuwa ni siku yangu ya kuzaliwa wanangu ghafla
wakaja na ''suprise,'' ikabidi niwaombe radhi nikimbilie chumbani kubadili nguo maana
keki ilikuwa imebebwa na camera zinanilenga.

Unazungunza kwa hamaki kwa kuingiza mambo ambayo si mada iliyopo mezani hapa.
Unazungumza kuhusu mabomu na mambo ya Allepo nk.

Ikiwa mimi napotosha wewe hukustahili kuja na matusi.

Ungekuja na ukweli ili ufute uongo wangu na hapa wasomaji wangenufauika kwa kujua
ukweli.

Unasema ati nakuja na ''takataka.''

Huu kwangu ni muhali ningekuwa naandika takataka watu wasingejazana hapa jamvini
kunisoma kila wanaponiona nipo.

Punguza ghadhabu na andika kwa adabu ikiwa unataka kufanya mjadala na mimi.
Ninayoandika ni kweli tupu na naweza kukupa ushahidi kwa kila neno langu.
 
Pole na matusi naomba utulie. Hata hivyo kuna swali ambalo hata mimi nilijiuliza: je kwenye picha ya kwanza hapo si wengine ni masista?
 
Pole na matusi naomba utulie. Hata hivyo kuna swali ambalo hata mimi nilijiuliza: je kwenye picha ya kwanza hapo si wengine ni masista?
Kipala ikiwa unakusudia picha ya Baba wa Taifa uwanja wa ndege hao ni kama nilivyoeleza.
 
Hii nchi uhuru umeletwa na mkristo julius nyerere
Kirumbuyo mchango wa Mwalimu Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika hauna mfano wake. Lakini ili uweze kujua ilikuwaje akawa kiongozi kwanza TAA HQ New Street 1953 kisha katika TANU 1954 ni lazima ujue historia ya Mwalimu Nyerere. Ukiijua historia hii ndipo utakapoelewa mengi ambayo hayakuwa wazi kwa wengi kwa miaka mingi.
 
Kipala ikiwa unakusudia picha ya Baba wa Taifa uwanja wa ndege hao ni kama nilivyoeleza.
TATU%2BBINT%2BMZEE%2B%25281%2529.JPG

Mzee, katika picha hii uliyoleta naona watu saba. Picha si nzuri. Hakika naona wanawake 5. Siwezi kumtambua lakini nadhani unatuambia mwanaume mwembamba ni Nyerere? Wanawake wawili kushoto na kulia kabisa wanaonekana kama wenye nguo za Kiislamu, na hao wawili wafupi wanavaa nguo zinazoonekana kidogo kama masista? Au wanavaa buibui? Halafu kuna mtu nyuma yao (labda anapita tu, hakukusudiwa awe ktk picha?). Pia mwanamke mmoja mwenye nguo za kisasa.

Kwa hiyo picha hii ilipigiwa na nani? Je ilichapishwa ktk kitabu fulani?
 
Kipala nimeeleza wapi nimepata picha hii na nyingine labda hukusoma uzi toka mwanzo. Ally Sykes alinikutanisha na Jim Bailey aliyekuwa na mswada wa kitabu cha picha kuhusu Baba wa Taifa. Bailey akaniomba nifanye uhariri wa kitabu chake. Huyu Bailey alikuwa na gazeti lake Drum likichapwa Johannesburg katika miaka ya 1950s. Katika kazi hii ndipo nilipopata picha hii ya 1955. Kulia ni Bi. Chiku Kisusa (Mama Sakina), Bi. Titi Mohamed, huyo wa tatu jina sina wa nne Mwalimu Julius Nyerere wa tano jina sina na wa sita ni Bi. Tatu bint Mzee. Bailey akiniomba pia baada ya kukihariri kitabu nimtafutie publisher. Mimi nikamjulisha Bailey kwa Walter Bgoya wa Mkuki na Nyota ambae ni rafiki yangu wa miaka mingi. Yeye ni publisher wa sifa na kitabu kikachapwa - The Story of Julius Nyerere of Tanzania. Picha hii ni moja picha kutoka Bailey African Collection. Ninazo picha nyingine mkipenda naweza kukuwekeeni hapa pamoja na historia zake.
 
Asante kwa ufafanuzi!
 
Back
Top Bottom