Siku ya Wanawake Duniani; Nini kifanyike katika kulinda mahusiano?

Beesmom

JF-Expert Member
May 30, 2016
17,221
28,666
Maana kiukweli dunia hii imeshatawaliwa na pesa, yaan utu wa binadamu umezongwa na kitu pesa. Mwanaume hataki kuhudumia ila anataka kisafi chenye mwonekano bora na mwanamke anataka kuhudumiwa(pesa) ili awe safi na mwonekano bora ambao mwanaume anautaka.

Sasa kilichonileta ni kutaka kujua toka kwenu vijana na watu wazima tuwafanyie nn ili mjisikie aman kuwa mpo penzini na mnapendwa mtulie pia na muweze kutafuta pesa ndani izidi kuongezeka kutokana na amani ya nafsi mliyonayo.

(hapa kwa wanawake kama hatujui,mwanaume ukimpa stress hata nguvu ya kusaka mavumba hupungua...ni jasiri kimwonekano ila moyoni ni dhaifu ivo kama unampenda usimpe stress mumeo).

Je tuwasikilize kwa kila kitu mpaka tuonekane punguani? Je tuwaachie majukumu ya kulea then sisi tuwatafutie mkwanja...maana nyie mmetusahau tunalea wenyewe? Yaan kuna muda huwa nashangaa mwanaume anaposema nani kama mama wakati hapohapo mama wa watoto wake hamjali.

Mpaka nimeandika hivyo vyote ni kwa sababu nimeona kuna wanaume wanateswa sana kihisia na wanawake tena sana( kuna wanaume wananyanyaswa ila hawasemi tu kuogopa dharau za wanalimwengu na ndo maana huishia kuua,kujiua,kuchanganyikiwa na kuzorota kiuchumi.Inaogopesha sana wanadamu kuishiwa kiupendo kias hiki.

Leo ni siku ya wanawake duniani,tuambieni tuwafanyie nn ili tulinde mahusiano yetu? Maana tukubali tukatae kupendana na kuheshimiana penzini ni raha sana.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom