Siku ya wanawake duniani 2019 wanawake wazalendo katika historia ya TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,232
30,620
Kwa kuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika haifahamiki na wengi hii imepelekea pia kwa wanawake wanachama wa mwanzo kujiunga na TANU kupigania uhuru wa Tanganyika wengi wao hawafahamiki ukimtoa Bi. Titi Mohamed.

Lakini tuanze na Bi. Titi Mohamed na kupitia kwake tuwajue wanawake wenzake aliokuwanao siku za mwanzo za kupigania uhuru.

1552020486987.png


Sijui kwa nini picha hii hapo chini haikuwa maarufu hapa nchini na haijawa maarufu hata baada ya kupatikana kwake na kuwekwa hadharani.

Picha hii nimeipata zaidi ya miaka 20 iliyopita kutoka kwa Jim Bailey kutoka kwenye Bailey's African History Archive (BAHA) nimeikuta katika mswada alionipa kuhariri kuhusu kitabu cha Mwalimu Julius Nyerere.

Niliipenda sana picha hii na nikaiweka mtandanoni.

Picha hii inamuonyesha kulia Bi. Tatu bint Mzee, Bi, Titi Mohamed, na kushoto wa kwanza ni Bi, Chiku bint Said Kisusa wakimsindikiza Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Uwanja wa Ndege safari ya kwanza UNO mwezi Februari, 1955.

Kitu cha kusikitisha sana ni kuwa picha hii hadi leo haijapata umaarufu unaostahili na baadhi ya wanaweka katika picha hii majina yao hayafahamiki.

Soma hapo chini historia ya Mwami Theresa Ntare chief wa pekee mwanamke Tanganyika wakati wa kupigania uhuru akieleza historia ya mapambano dhidi ya ukoloni a Waingereza:

1552020580445.png


''Serikali ya kikoloni haikutaka sisi machifu tuwe katika siasa hasa kuisaidia TANU.

Hata hivyo tukiwa wananchi na viongozi wa wanchi wanaotaabika chini ya utawala wa kikoloni, tuliiamua kushiriki siasa kwa siri na kuipa nguvu TANU ili tujitawale.

Kuna wakati taarifa zilinifikia kwamba ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulikuwa unakuja kusikiliza maoni ya kudai uhuru.

Utaratibu wa kikoloni ni kuwa chama japo ni cha kitaifa, kilitakiwa kipate pia usajili katika kila jimbo.

Hivyo TANU ikidai kuwa inawakilisha wananchi wote, watawala wa mikoa walikuwa wakijiandaa kukisuta kuwa si kweli na kuonesha sehemu ambako hakikuwa na wanachama.

Moja ya sehemu hizo wakoloni waligundua ni katika himaya ya utawala wangu wa Buha. Waligundua TANU haipo kwa Waha.

Taarifa za siri zikanifika kwa wakoloni wataiambia tume hiyo ya UNO juu ya hilo. Nikaamua kuchukua hatua kwa siri na kwa haraka.

Nilitoa pesa zangu binafsi na kuagiza haraka kadi za TANU elfu tatu.

Zikaletwa kwenye vikapu.

Nikaweka mkakati wa siri na watu wangu jinsi ya kuzigawa kadi hizo kwa haraka kwa wananchi wa maeneo ya Buha.

Majira ya saa tatu za usiku lilipigwa baragumu la wito wa dharura watu waje kwa Mwami.

Wito ulifikishwa kwa haraka kila eneo wakamiminika.
Eneo la makazi yangu lilikuwa na uwanja mkubwa sana.

Niliwapanga watu wangu katika lango la kuingilia wakiwa na vikapo vilivyokuwa na kadi za TANU na karatasi zake za risiti.

Kila mtu alipoingia alipewa kadi na risiti isiyoandikwa kisha akaambiwa aifikiche kadi na hiyo risiti pasipo kuichana na asiongee chochote hadi afike lango la nyuma ambalo ni la kutokea.

Hapo palikuwepo watu wamejipanga katika meza. Walipofika hapo walimpa huyo aliyekuwepo katika meza hiyo kadi na risiti kisha kumtajia majina yake, anakoishi nk.

Yule karani aliiiandika ile kadi na risiti kwa tarehe za miezi ya nyuma, meza nyingine ilipiga muhuri.

Mwisho mwenye kadi aliambiwa kuwamba ameisha kuwa mwanachama wa TANU wa muda mrefu.

Akiulizwa atoe kadi na aitetee TANU pasipo kumtaja Mwami wala kilichotokea usiku ule; kwake hicho ni kiapo cha utiifu kwa Mwami.

Aliruhusiwa na kusisitizwa kuitunza hiyo kadi na risiti yake.

Ilipofika alfajiri karibu ya saa kumi na mbili za asubuhi, nikaambiwa kuna msafara wa magari ya polisi unaelekea kwenye makazi yangu.

Niliyategemea hayo, maana vibaraka wapelelezi walikuwepo enzi hizo.

Hata hivyo, kwa tukio lile walikuwa wameshachelewa. Mimi siku ile sikuwa nimelala wala kupata usingizi.

Nilikuwa katika nguo zangu za kawaida. Nilipoletewa taarifa ile, nikaingia chumbani na kuwaambia walinzi wangu kuwa wakifika, kwanza kuweni imara kuhusu siri ya kilichotokea usiku.

Pili waambieni kuwa Mwami hajamka.

Ngoja tukamwamshe kisha mje kunigongea na nitakapotoka na kufokeana nao, nyiye onesheni utiifu kwangu na kuwakasirikia wao; wala msioneshe kuwahofu.

Mkakati huo ukaeleweka.

(Alipoamka Mwami akawa kakasirika anafoka kwa Kiingereza)

“How dare you wake me up at this time of the hour?
Can you do this to the Queen of the UK?
Don’t you know I am the the Queen of Buha?
Is it because I’m an African that’s why you are doing this to me?
I will file my complaints and report you to the Governor for this.”

Picha hiyo ya mwisho inaonyesha maandamano ya wanawake wa TANU wa kwanza kushoto ni Bi, Mwamvua Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.

Huyu alikuwa mke wa Abdul Sykes na ndiye mama yake Kleist Sykes aliyekuja kuwa Mayor wa Dar es Salaam.

Mama Daisy ndiye aliyempokea Mwalimu Nyerere na Mama Maria Dar es Salaam mwaka wa 1952 pale Mwalimu Nyerere baada ya kujiuzulu ualimu mwaka wa 1955 alipokuja kwa muda kuishi na Abdul Sykes nyumbani kwake Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Mama Daisy ana mengi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere siku za mwanzo za TANU.

Mama Daisy alikuwa kitabu cha historia ya TANU na harakati za kupigania uhuru.

1552020700665.png
 
Historia nzuri sana, katikati ya bi Chiku Kisusa na mwalimu Nyerere aliitwa nani huyo?
 
Back
Top Bottom