Siku ya Vijana

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
263
13
SIKU YA VIJANA DUNIANI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kila mwaka tarehe 12/08 ni siku ya vijana kimataifa. Siku ya hii kimataifa iliadhimishwa kwa mara ya kwanza duniani mnamo mwaka 2000 licha ya kupitia michakato mingi kabla ya hapo.Kuanzia hapo siku hii ikawa maalumu kwa vijana ambapo hutakiwa kujadili mada itakayokuwa imependekezwa na umoja wa mataifa. Mada ya mwaka huu ni Vijana na madiliko ya hali ya hewa.
“YOUTH AND CLIMATE CHANGE”.

Kwa hapa Tanzania siku hii iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2003 ambapo asasi ya Tanzania Youth Vision Association [TYVA] kwa kushirikiana na Youth of United Nations Association[YUNA] waliiandaa.

Mwaka huu tena asasi ya TYVA na YUNA kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya vijana imeandaa siku hii inayotarajiwa kuadhimishwa kwa siku mbili yaani tarehe 11 na 12. Kwa kuzingatia uhasilia wa mahitaji na masuala ya nchini mada imemahalishwa na kuwa Vijana ni msimgi wa mazingira endelevu “YOUTH A BASE FOR SUSTAINABLE ENVIRONMENT”.

Lengo kuu ni kuona vijana wanakuwa mstari wa mbele katika kutunza na kuyahifadhi mazingira kwa ujumla wake. Hii ni pamoja na kuibua wanaharakati vijana watakaokuwa wahamasishaji wakuu katika masuala ya mazingira.

Siku ya tarehe 11 kutakuwa na mkutano katika ukumbi wa karimjee utakawahusisha vijana kutoka shule za sekondari hadi vyuo, asasi za kiraia, na wawakilishi wa vijana toka vyama vya siasa.

Siku hii mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri katika ofisi ya Makamu wa Raisi anayeshughulikia Mazingira Mh Dk Batilda Buriani[MB]. Pia watoa mada watarajiwa ni pamoja na Dk Tindu Lissu kutoka LEAT atakaye zungumzia masuala ya mazingira na Hebron Mwakagenda toka Policy Forum atakaye zungumzia mchango wa asasi za vijana Sambamba na hawa , pia kutakuwa na uwakilishi kutoka Ofisi ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa mataifa hapa nchini “UN Residential Coordinator”.

Na hatimaye kilele cha mahadhimisho haya Siku ya tarehe 12 tunatarajia kufanya matembezi yatakayoanzia viwanja vya mnazi mmoja hadi viwanja vya karimjee ambapo yatapokelewa na mgeni rasmi, Mhe. Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.


Mgeni rasmi anatarajiwa kupokea ujumbe wa vijana utakaotokana na mdahalo wa tarehe 11.

Aidha tunapenda kutoa wito kwa vijana wote kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 12 ambayo ni siku ya matembezi.

Siku hii itafanikishwa kwa udhamini wa Tawi la Umoja wa Mataifa “UNIC” pamoja na kampuni ya simu za mikononi ya TIGO.


Imetolewa na;


……………………………
Moses Robson
Mratibu wa Tukio
0754-833 580
0755-459 783
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom