Siku ya Vijana Duniani: BAVICHA Bukoba na Mbunge wao washiriki kufanya Usafi sehemu mbalimbali ndani ya Bukoba

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
690
841
Jinsi ilivyoadhimishwa Wiki ya Vijana Duniani na Mbunge wa Bukoba mjini ashiriki

Siku chache baada ya kesi ya Ugaidi iliyokuwa inamkabili mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Wilfred Lwakatare kuisha kufuatia mahakama ya rufaa Tanzania kuyafuta maombi ya kibali cha Mkurugenzi wa mashtaka DPP kutaka kupinga maamuzi ya mahakama kuu kufuta shitaka hilo la ugaidi,tayari amewasili jimboni kwake na ameeleza jinsi alivyokwama kutekeleza shughuli za maendeleo kufuatia kesi hiyo.


Akiwa katika zoezi la usafi lililofanyika leo katika makaburi ya kishenge manispaa ya Bukoba,ambapo ameungana na vijana waliojitoa katika wiki hii ya vijana duniani kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo wakiwa sambamba na madiwani wa Chadema pamoja na viongozi wa chama hicho manispaa ya Bukoba,ametumia fulsa hiyo kusema kuwa kesi ilidumu kwa zaidi miaka minne kitendo kilichomfanya aishi kwa wasiwasi na kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa muda muafaka kutokana na usumbufu aliokuwa akiupata

Aidha Lwakatare amewapongeza wanabukoba na wanachi wote kwa ujumla kwa sala walizomuombea mpaka kuhakikisha kesi hiyo inaisha huku akiahidi kuendelea kushirikiana na wanajimbo lake katika shughuli za kuleta maendeleo.

Ameongeza kuwa kilele cha Wiki hii ya vijana Dunian kitafikiwa siku ya jumamosi na manispaa ya Bukoba wamepanga siku hiyo kufanya usafi katika stend kuu ya mabasi ndani ya Manispaa hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kutunza mazingira na amewaomba wanabukoba kujitokeza kwa wingi ili kuweza kufanikisha Zoezi hilo.

Sanjali na hayo mh Lwakatare amesema kuwa bado anakabiliwa na kesi nyingine ambayo ni ndogo ya hiyo iliyoisha na anatakiwa kuhudhuria Tarehe 22 mwezi huu katika mahakama ya Kisutu na ametumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania kumuombee ili na yenyewe iweze kuisha salama ili arudi jimboni kwake rasmi kwa ajili ya kuendelea kupambana na maendeleo ya wananchi.

Tazama picha mbalimbali za shughuli ya ilivyokuwa.
3cd24350-98d8-4079-9510-5d7cf64b2c6a.jpg
23442a15-0d1c-49d5-b69d-790283747e5b.jpg
e005e60f-5b91-444c-8509-c70f43a84335.jpg
70985ca6-e4bf-46a1-b945-11528d1a9f30.jpg
b8d1f73e-26b3-4d2d-8259-10bac05e16f6.jpg
 
Wakati vijana wengine MAREKANI wako SILICON VALLEY wanajenga mawazo yao ya KIUBUNIFU na kuwa MAKAMPUNI MAKUBWA, Huku kwetu vijana wamekuwa MISUKULE na WABEBA MIKOBA wa WANASIASA. SHAME !
 
Wakati vijana wengine MAREKANI wako SILICON VALLEY wanajenga mawazo yao ya KIUBUNIFU na kuwa MAKAMPUNI MAKUBWA, Huku kwetu vijana wamekuwa MISUKULE na WABEBA MIKOBA wa WANASIASA. SHAME !
Dunia unaijua wewe??? ebu funga ilo li bakuli lako
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom