Siku ya ushairi duniani, Jua kidogo kuhusu ushairi na mashairi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
KATIKA KUAZIMISHA SIKU YA USHAIRI DUNIANI, WATAMBUE WASHAIRI NGULI WA TANZANIA

Uwepo wa siku ya ushairi duniani, Machi 21, UNESCO imeonyesha kutambua upekee wa kisanaa ulioko katika mashairi. Maamuzi ya kufanya Machi 21 kuwa siku ya ushairi yalifanyika Paris, mwaka 1999

Ushairi ulianza, zaidi ya miaka 3500 iliyopita. Mashairi hutumiwa kama uwanja wa kuonyesha umaridadi wa lugha na kutoa falsafa. Wayunani, Wayahudi, waarabu, wabantu nk walitumia mashairi kueleza umaridadi wa vitu tofauti tofauti

WAYUNANI NA USHAIRI
Hawa walitumia ushairi kutoa falsafa. Mtu kama Thales of Miletus (626-548 BCE) alitumia mashairi kuelezea falsafa zake. Na wanaflsafa kama Plato walihusudu ushairi,

WAISRAEL NA USHAIRI
Biblical studies zinaonyesha kuwa na ushairi mwingi kwenye biblia, ambao umetumika na waisrael katika kuelezea masuala tofauti tofauti. Vipo vitabu ambavyo hadi sasa vinachukuliwa kama ushairi i.e wimbo ulio bora, lakini Biblical studies zimeona vitabu vingi ndani ya biblia kuwa na poetry style katika uandishi wake, pia yako mashairi kwenye baadhi ya vitabu vya historia

WAARABU NA USHAIRI
Hawa mimi nawaona kama wanahusudu sana ushairi wenye vina, hata quran imeandikwa verses zenye vina, kwa wapenzi wa ushairi wanaweza penda kusikiliza wakiwa wanaswali hata kama hauelewi nini kinasemwa, ushairi una raha yake bwana!

Japo hata kwao mashairi yalianza kale zaidi kabla ya quran, ni waarabu kwa kiasi kikubwa ndio wamewapa washahili, namna ya ushairi wa mavina, na hata washari bora wa tanganyika walikuwa ni wale wa Pwani au visiwani, kama kina Siti Bint Saad nk

WABANTU NA USHAIRI
Kwanza naomba unapowasoma wabantu hapa toa picha yako ya waswahili ambao nimewaeleza hapo juu. Wabantu kabla ya kuchangamana na waarabu na waswahili walikuwa wanatumia ushairi kwenye matukio tofauti tofauti, kama jando, unyago, sherehe za ndoa, vita nk

Mahairi yalitumika kutoa maadili na mafunzo kwa watoto ili kwenda vizazi vingine. Ushairi ndio ulifanya mbantu awe na masuala ya uimbaji kwa kiasi kikubwa sana. Nyimbo ni kitu cha thamani kwa mbantu, si unajua ngoma za makabila mbali mbali zikigongwa, hata kama sio kabila lako unajikuta unafuatilia maneno tu

Kwenye harusi wabantu wanakawaida kusemana kwa mashairi, kama ndugu zangu wangoni huwa wanatunga wimbo hapo hapo kukuchana

MASHAIRI KWA STAREHE
Labda kwa uhaba wa maneno, nitumie maneno ya kiingereza. Kwa wale wanamashairi wenzangu mshawahi kutumia mashairi kumuimbia beibe alale, wazungu wanaita LULLABY, mtoto analala kifuani wazidi kumpiga mashairi ya kuliwaza na kumbembeleza.

Au pia ukutane na mwanamke mpenda mashairi ambaye mara moja moja naye anakuwasha mashairi. Raha iliyoje

Hebu tufikirie kuwahadithia watoto kwa mashair, yaani hata hadithi ikiwa na shairi ndani yake inakuwa na raha zaidi, kama hizi hadith za watoto zinakuwa na ile kitu wanaita BALLAD kwa kiingereza

Nisiseme sana kuhusu Hyms, centicles nk maana mashairi yana uwanja mpana sana

BAADHI YA WASHAIRI NGULI

Tanzania tunao washairi wakubwa wenye mchango mkubwa kwenye lugha na falsafa.

Yupo Shaaban Robert, mzee mwenye heshima katika lugha ya kiswahili kwa tanzu, tenzi na mashairi mengi aliyowahi kuandika wakati wa maisha yake

Euphrase Kezilahabi. Huyu ni mmoja kati ya waasisi wa mashairi ya kisasa. Mashairi yake huwa na wingi wa fikra na falsafa.

Said Sudi Andanenga, huyu ni mzee ambaye amekuwa na ugomvi mkubwa wa kifasihi na Kezilahabi kwa tofauti za uandishi. Andanenga anaandika mashairi ya kimapokeo. Ugomvi wake na Kezilahabi ulikuwa kwa sababu Kezilahabi alikuwa anaandika mashiri ya kisasa, ambayo kimsingi Andanenga hayapendi kabisa

Kezilahabi kuna Shairi lake amemuadress Andanenga kuwa aache uzamani, umapokeo.

Ugomvi wa mashairi ya kisaa na kimapokeo bado upo kati ya waandishi wa kisasa na kimapokeo, nishawahi muona mzee mmoja akimnanga Mpoto unandishi wake haufuati utaratibu.

Ugomvi wa kifasihi una raha yake kwenye mijadala, sio maugomvi yenu vijana ya kutafutana na mapanga na bastola, Ugomvi wa kifasihi mnatafutana kwa hoja na beti za ushairi

Tuwajue vijana wengine wanaofanya ushairi kwa kizazi hiki

Wapo vijana ambao nao wameingi kwenye uandishi wa mashairi na wengine wakighani ili kuwafikia hata wasiopenda kusoma, hapa tuwataje kina Mrisho Mpoto, Justine Kakoko, Male Hanzi, Hellen Burugu, Amos Mwijage na wengineo wengi
 
Utapoteza muda tu ila kama utautumia ki digitali zaidi. Kutengeneza movie kali ambayo inamaneno yenye miguso ya hisia. Nk nk. Sio uanze mambo ya karudi baaabaa mmojaaa toka safariii ya mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwe mkali wa mashairi ya mapenzi...hapo utawin sana....ufungue account Instagram....na YouTube unaweza vipande vya video za mashairi
Unaweka kama maigizo mafupi.
 
Hawa mimi nawaona kama wanahusudu sana ushairi wenye vina, hata quran imeandikwa verses zenye vina, kwa wapenzi wa ushairi wanaweza penda kusikiliza wakiwa wanaswali hata kama hauelewi nini kinasemwa, ushairi una raha yake bwana!

Hivi kaka kuna Mashairi bila "Vina" ? Hivi hujiuliza katika ulimwenguwa usasa wa mashairi wanaongelea sana kutokufata vina wala urari ? Hii inaonyesja ya kuwa asili ya Mashairi ni vina.

Pili, sio kila chenye vina ni SHAIRI. Ndio maana Qur'aan sio MASHAIRI. hii nimeongezea tu.
 
Euphrase Kezilahabi. Huyu ni mmoja kati ya waasisi wa mashairi ya kisasa. Mashairi yake huwa na wingi wa fikra na falsafa.

Kwangu mimi huyu alikuwa muharibifu tu wa fani hii adhimu na ya tangu na tangu ya Ushairi.

Kielimu na ukweli ulivyo hakuna Ushairi wa kisasa katika umbile bali kama katika maudhui hapa tunaweza kujadili ila kwa umbile, huku ni kubabatiza mambo na kuidhulumu fani hii ya kale na kongwe katika lugha.

Ahsante.
 
Hivi kaka kuna Mashairi bila "Vina" ? Hivi hujiuliza katika ulimwenguwa usasa wa mashairi wanaongelea sana kutokufata vina wala urari ? Hii inaonyesja ya kuwa asili ya Mashairi ni vina.

Pili, sio kila chenye vina ni SHAIRI. Ndio maana Qur'aan sio MASHAIRI. hii nimeongezea tu.
Wanamapokeo akiwemo Shaaban Robert waliamini Shairi ni lazima lifuate urari wa vina na Mizani.Wengine walienda mbali na kudai Kama mshololo utakuwa na mizani 16 Basi nusu yake iwe 8 kwa hiyo 8+8=16.Lakini walipokuja wana usasa walitetea Sana kuwa si lazima shairi kufuata urari wa Vina na mizani kikubwa ni ujumbe wa mshairi uifikie hadhira husika yaan Shairi libebe ujumbe.Mmojawapo akiwa Kazilahabi ndo maana Mohammed Seif Khatib katika Diwani yake ya Wasakatonge kachanganya mitindo yote miwili.
 
Wanamapokeo akiwemo Shaaban Robert waliamini Shairi ni lazima lifuate urari wa vina na Mizani.Wengine walienda mbali na kudai Kama mshololo utakuwa na mizani 16 Basi nusu yake iwe 8 kwa hiyo 8+8=16.Lakini walipokuja wana usasa walitetea Sana kuwa si lazima shairi kufuata urari wa Vina na mizani kikubwa ni ujumbe wa mshairi uifikie hadhira husika yaan Shairi libebe ujumbe.Mmojawapo akiwa Kazilahabi ndo maana Mohammed Seif Khatib katika Diwani yake ya Wasakatonge kachanganya mitindo yote miwili.

Safi kabisa.
Kitu gani kinatofautisha kati ya "Nathari" na "Shairi" ?
 
Lakini walipokuja wana usasa walitetea Sana kuwa si lazima shairi kufuata urari wa Vina na mizani kikubwa ni ujumbe wa mshairi uifikie hadhira husika yaan Shairi libebe ujumbe.

Kaka mimi naweza kutoka kifua mbele nakusema ya kuwa wajiitao wana Usasa hawaujui Ushairi ni nini na nini Shairi hata kama wana uwezo wa kutunga mashairi ya asili yaani ya kimapokeo au kama wanaujua basi wameamua kuwa waharibifu kwa maslahi yao binafsi. Na huku tunasema ni kuihujumu Elimu.
 
Back
Top Bottom