Siku ya usafi Musoma, tupeni update!

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,881
2,000
Mkuu wa mkoa wa Mara alitangaza kuwa leo ni siku ya usafi. Wanaodai katiba mpya nao wakakubali kushiriki usafi na baada ya hapo kongamano liendelee.

Tupeni kinachojiri huko!!!

==========
Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi mapema leo asubuhi amewaongoza wananchi wa Mkoa huo na watumishi wa kada tofauti wa halmashauri ya Musoma kwenye zoezi la kufanya usafi katika Stendi ya zamani ya mabasi mjini Musoma, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya Usafi Mkoa wa Mara.

Katika zoezi hilo Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Mhe. William Patrick Gumbo na Makamu wake, huku wananchi wa mji huo wakionekana kuwa na mwitikio mkubwa kwenye zoezi hilo.

Happi Musoma.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi (aliyebeba uchafu) na Katika Tawala wa Mkoa huo Albert Msowela (aliyeshika fagio) wakishiriki zoezi la kufanya usafi wa Mazingira katikati ya Mji wa Musoma nje ya lango la soko Kuu ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa wiki ya usafi wa Mazingira Mkoani humo.
Chanzo: GW Media
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom