Noor
Senior Member
- Feb 5, 2012
- 146
- 49
Ndugu zangu,
Nimeona si vibaya kuwakumbusha tunapoenda kwenye siku ya Ukimwi duniani hapo kesho tujaribu kuangalia kwa mapana baadhi ya mambo na kujitafakari kwa mapana kama tuko kwenye njia salama ama la.
Nafarijika kusikia na kutambua kwetu kuwa janga la UKIMWI linahitaji elimu kwa jamii yote ili kufanikisha mapambano dhidi yake. Na nafarijika pia kusikia aghalabu siku hizi vitendo vya unyanyapaa vinapungua kwa kiasi kikubwa. Ndugu zetu walioathirika wasitengwe au kunyanyaswa.
Ningependa sote tujiulize tena maswali magumu bila aibu na tuchukue hatua bila ajizi. Je, tangu mwaka huu uanze tumeshiriki kiasi gani kuzuia kuenea kwa UKIMWI? Je, wewe umekwisharekebisha mwenendo wako na kuacha tabia zinazochangia kuenea kwa UKIMWI? Je, kwenye mazingira unayoishi (sehemu ya kazi au vyuoni) pamekuwa na mwamko mpya wa kupambana na UKIMWI? Wewe unashiriki vipi?
Kila mmoja atafakari kwa dhati moyoni mwake na achukue hatua. Tusaidiane kwa kila hali kuweza kujikinga, na kwa walioathirika tayari kuwatendea haki bila ubaguzi. Kila sehemu iwe na utaratibu wa kukumbushana mara kwa mara juu ya UKIMWI, na mkakati mahususi wa kuzuia kuenea kwa virusi vya UKIMWI.
Nawatakia afya njema na mchango mwema kwenye jamii yetu inayotuzunguka ili tuutokomeze UKIMWI na kuifanya Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla kua ni sehemu yenye mafanikio yanayotokana na afya njema.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika.
abdulnoor3@gmail.com