Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017: Rais Magufuli mgeni rasmi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,713
13,464
Rais John Pombe Magufuli atahudhuria maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo kitaifa zitafanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 2-3/Mei /2017.

Aidha, Rais Magufuli anategemewa kuhutubia tasnia ya habari kuhusu mwenendo wa uhuru wa habari nchini, maadhimisho hayo pia yatahudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari, Waziri wa habari na michezo Dr. Harrison Mwakyembe na wageni wengine wa ndani na nje.

JamiiForums ni mmoja wa wadhamini wa siku hii muhimu.

MSISITIZO: Maoni ya wadau kupitia Mtandao huu yatasomwa ukumbini jijini Mwanza!

----------
Via Instagram:


Via Facebook:


 
Ha ha ha haaaa... "not to that extent"

Iddy Amin- I can guarentee you freedom before but not after speech.

Hii inaitwa usiyempenda kaja.
 
mh rais asisahau kuwaonya wanahabari wanaotumika ili tujenge tasnia yenye ubora wa hali ya juu
Ikiwezekana wanaokiuka wafutiwe lesen zao
 
Rais John Pombe Magufuli atahudhuria maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo kitaifa zitafanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 2-3/Mei /2017.

Rais Magufuli anategemewa kuhutubia tasnia ya habari kuhusu mwenendo wa uhuru wa habari nchini, maadhimisho hayo pia yatahudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari, Waziri wa habari na michezo Dr. Harrison Mwakyembe na wageni wengine wa ndani na nje.

Ikiwezekana hao Waandishi wa Habari waibadilishe hiyo siku na iwe ni Siku yao ya Mahojiano MAALUM na Mheshimiwa Rais na yaende mubashara / live katika Vyombo vyote vya Electronics.
 
Magufuli ni ngumi jiwe. hatua hiyo ni muhimu sana kwa ujenzi wa uhuru wa habari nchini
 
Hao waandishi wazinguaji walipewaga nafasi ya kumuuliza maswali wakawa hawaeleweki na uhuru wao ulikuwa ushaanza kuingiliwa ni kama alikuwa anawapima sasa tungoje natuone hii ni stage nyingine
 
Hawana lolote hao walishapoteza mwelekeo toka day one walipoitwa ikulu,nadhani wataishia kupiga makofi na kuomba wine kisha wajumuike kwenye pilau.
 
Huyu jamaa hana hata mshipa wa aibu?!!! Adui number moja wa vyombo vya habari ndio anakuwa mgeni rasmi siku ya uhuru wa vyombo vya habari!!!!! Nchi hii haiishi vituko
 
MWENYE BUCHA ANAPOMUALIKA FISI AWE MGENI RASMI. " Nyie wamiliki wa vyombo vya habari, kama mnafikiri mnao uhuru, mimi nawaambia, not to that extent" (Magufuli, 2017)
 
"Kuna kituo fulani cha TV chenyewe huonyesha mapigano ya wakulima na wafugaji. Kwao hiyo ndiyo habari, na inachukua muda mrefuuuuu" (Magu, 2017).

"Kuna magazeti mawili hivi, dawa yao iko jikoni" (Magu, 2016)

"Habari za mitandaoni, mara huyu kavamia sijui nini.... Mimi habari za mitandaoni hazina tija kwangu, ni udaku tu. Wewe Makonda chapa kazi.... Nasema chapa kazi" (Magu, 2017)

" Nyie wamiliki wa vyombo vya habari, kama mnafikiri mnao uhuru, mimi nawaambia, not to that extent" (Magufuli, 2017)

" Magazeti yanamwonyesha mtu anatoa sijui nini huku anarudisha huku..... ukurasa wa kwanza, wa pili..... ni uchochezi tu, kana kwamba huyo mtu katumwa na serikali. Nyie vyombo vya habari 'watch it, watch out" (Magu, 2017)

NB: Sielewi vyombo vya habari vinamwelewaje mtu huyu. Laiti vingemwelewa sawasawa.....
 
Back
Top Bottom