Siku ya Sheria Tanzania: Ili Tanzania ifanikiwe kwenye uwekezaji ni muhimu kuwe na utengamano wa kisheria na mfumo wa haki unaheshimiwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Dar es Salaam. Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Rugemeleza Nshala amesema ili Tanzania ifanikiwe kwenye uwekezaji ni muhimu kuhakikisha kuna utengamano wa kisheria na mfumo wa haki unaheshimiwa.

Nshala ameyasema hayo leo Alhamisi Februari 6, 2020 katika maadhimisho ya siku ya sheria yanayofanyika jijini Dar es Salaam yenye kauli mbiu ya ‘Uwekezaji na biashara wajibu wa mahakama, wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.’

Amesema tafiti zinayonyesha kinachowavutia wawekezaji sio kodi, misamaha ya kodi bali utengamano uliojikita katika misingi ya sheria na kuheshimika kwa mfumo mzima wa haki.

“Ni wazi kuwa utengamano wa nchi na utawala wa kisheria ndiyo unavutia wawekezaji kuwekeza katika nchi yetu na kukuza uchumi wetu. Na imani hiyo inakuwa na kuongezeka pale juu ya maamuzi ya mahakama kuhusu migogoro yote ya kisheria, kikodi, kijinai na madai yanapoheshimiwa,” amesema.

Amesema katiba inaelekeza wazi kuwa kunapokuwa matatizo yoyote yanayohusiana na uwekezaji na biashara ni vyema yapelekwe mahakamani tofauti na inavyofanyika sasa.

“Mikataba mingi inayosainiwa kati ya nchi yetu na mataifa mengine inapoka mamlaka ya mahakama zetu na kuipa mamlaka hayo mashirika ya usuluhishi au taasisi za usuluhishi za migogoro ya kimataifa.”
 
Back
Top Bottom