Ptro Petro:Wewe ni ng'inyang'inya
Wewe M TAG ni Yuda Iskarioti.Wanasheria wakiongea huwa wana quote vifungu vya sheria ulitaka wamu quote Lisu kwani yeye ni kifungu cha sheria
Jinga lao una za kuvukia barabara ya lumumba tu mkuu
Mimi nilitegemea kuwa wewe ni Jasiri kumbe BOGA kabisa, Taja aliyehusika kwenye tukio la Lisu. Mbona umefyata mkia ? Mbilinyi yeye alimgonga na gari mtoto Yatima tena kwenye Zebra Crossing na kumuua, mbona hili hauliongelei ?, badala yake unashupalia la Lisu kupigwa risasi, Je huyo mtoto tena Yatima kugongwa na gari kwenye Zebra crossing na kumuua lenyewe mbona huongelei ?
Nadhani aliyemgonga yule mtoto na kumuua ni dereva Wa mbilinyi wala sio mbilinyi mwenyewe.Mimi nilitegemea kuwa wewe ni Jasiri kumbe BOGA kabisa, Taja aliyehusika kwenye tukio la Lisu. Mbona umefyata mkia ? Mbilinyi yeye alimgonga na gari mtoto Yatima tena kwenye Zebra Crossing na kumuua, mbona hili hauliongelei ?, badala yake unashupalia la Lisu kupigwa risasi, Je huyo mtoto tena Yatima kugongwa na gari kwenye Zebra crossing na kumuua lenyewe mbona huongelei ?
Wanabodi,
Leo nimepata fursa kuangalia sherehe za maadhimisho wa siku ya sheria zilizokuwa zikitangazwa live na TBC. Chama cha wanasheria ni mdau muhimu wa maadhimisho haya ambayo huhutubiwa na rais wa chama hicho. Kwa vile rais wa TLS ni Tundu Lissu, na ameshindwa kuhudhuria kutokana na kuwa mgonjwa, jina la Tundu Lissu, halikutajwa popote!. Swali la kujiuliza, ni kutotajwa huku kutokana na kusahaulika tuu, Lissu amepuuzwa as if he doesn't exist, or ameepukwa kutajwa kwa makusudi?.
Kwenye ratiba ya maadhimisho hayo, kulionyesha kuna mahali rais wa TLS, angepaswa kutoa salamu. Kwa vile rais wa TLS, Mhe. Tundu Lissu, ni mgonjwa kwa shambulio la risasi, aliyekuja kuzungumza nafasi ya rais wa TLS, ni Makamo rais wa TLS, nikitegemea, alipoanza kuzungumza, kwa vile aliyepaswa kuzungumza sii yeye ni rais wa TLS, hivyo anaongea kwa niaba ya rais wa TLS, then, kistaarabu tuu, alipaswa kusema anazungumza kwa niaba ya rais wa TLS ambaye ni mgojwa. Huyu Makamo rais wa TLS, aliposimama kuzungumza, alisimama na kujitaja kuwa anazungumza kwa niaba yake!. Ratiba inasema mzungumzaji ni rais wa TLS, wewe sio rais wa TLS, unasimama kuzungumza badala ya rais wa TLS, ilibidi kumtaja rais wa TLS as an excuse ndipo uendelee!.
Naibu Spika, Tulia Akson, amemuwakilisha Spika ametajwa kuwa yupo anamuwakilisha spika. Naibu DPP ametajwa kumwakilsha DPP, Naibu Mwanasheria Mkuu ametajwa kumwakilisha Mwanasheria Mkuu, kwa nini huyu Makamo rais wa TLS akajitaja yeye ili hali kwenye ratiba aliyeandikwa ni rais wa TLS.
Aliposimama mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano, naye katika maelezo yake, akamtaja rais wa TLS na kujikwaa, akamtaja Makomo rais wa TLS.
Huku kutotajwa kabisa kwa rais wa TLS, Tundu Lissu. ni oversight tuu ya kusahaulika, au ni omission kuwa Tundu Lissu asitajwe popote.
Rais katika hotuba yake, akatoa pole kwa mhimiliwa mahakama kwa kifo cha Jaji Robert Kisanga ambaye aliishastaafu siku nyingi, kama mtu aliishastaafu siku nyingi na kufariki, mhimili huu unapewa pole, vipi kuhusu shambulio la rais wa TLS ambaye hadi sasa anauguza majereha ya shambulizi, hatajwi popote, wala hata kumtakia uponywaji wa haraka!.
Amini usiamini, kama Tundu Lissu, angekufa kwa shambulio lile, hotuba ya TLS ingemtaja, na kile aliyehutubia, angetoa pole kwa TLS kwa kuondokewa na rais wake, lakini kwa vile Lissu yuko hai, amenusurika, hadi marehemu wastaafu wanapewa pole, lakini walio hai wanaohitaji kuombewa tuu uponyaji wa haraka, wamesahaulika, kama sio kuepukwa!.
Kama huku sio kusahaulika, bali ni kuepukwa, then bandiko hili, ndio taarifa ya awali, kuwa urais wa Tundu Lissu kwenye TLS, unaofikia kikomo miezi miwili ijayo, Mwezi April, 2018, wanasheria watakutana na kumfuta rasmi kazi Tundu Lussu kama rais wa TLS, na inawezekana kabisa, jina la Tundu Lissu likaingia kwenye kumbukumbu za TLS kuwa Tundu Lissu ndie rais wa TLS ambaye he did almost nothing, tangu achaguliwe, kwa kudumu kwa miazi mitatu tuu TLS, ba baada ya hapo, akashambuliwa, hivyo kumaliza Kipindi chake chote cha urais akiwa hospitalini.
Pamoja na kwamba Tundu Lissu ni mgonjwa na yuko hospitalini, bado yeye ndie rais halali wa TLS!. Kuumwa hakumfanyi Tundu Lissu asiwe rais wa TLS, hivyo he was worth mentioned, na kutakiwa uponyaji wa haraka!.
Get Well Tundu Lissu, pole sana, umesahaulika mapema!.
Paskali
Waliokwapua Richmond umewasahau
Tangu nianze kukusoma hakika leo umetoa mchango bora kabisa.
Yesu unamuingizaje katika hili?Kwani angetajwa ndio Yesu angashuka?