comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Wana jamvi
Salaam
Mh Rais Magufuli anazungumza na Mahakama na vyombo vya kutoa haki, Mh Rais ameanza na kuipongeza Mahakama, Majaji, Wanasheria na Mawakili.
Aidha, anaongelea changamoto za vyombo vya utoaji haki changamoto kama Mishahara midogo, posho, marupurupu, nyumba na vitendea kazi.
Rais amehoji uhalali wa mahakimu 28 waliokua na kesi ya rushwa na wote wakashinda kesi zao, vilevile amemuomba Kaimu jaji Mkuu Professa jaji Ibrahim Juma amsaidie namna ya kuboresha utumishi wa mahakama kwa kuzingatia Weledi na kubana matumizi.
Mh Rais amesema haoni haja ya watu wengi wanaofanya kazi zinazofanana waendelee kufanya kazi hizo na badala yake ameomba kazi za aina hiyo zingefanywa na watu wachache na walipwe vizuri.
Pia amekemea ucheleweshwaji wa kesi amesema kuna mtindo wa kuchelewesha kesi au kwa lugha fulani unaitwa kupark kesi, na kuna kesi ya kukwepa kodi jumla ya pesa sh tril 7.5 amesema uharaka unahitajika uharaka katika kumaliza kesi hizo hasa za kukwepa kodi na kesi nzito nzito
Aidha, Rais ameishukia ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu DPP na Mwanasheria Mkuu kwamba ana taarifa za migogoro yao na kwanini wagombane wakati wote wanahusika na kutoa haki na amemuomba Waziri wa Sheria na Katiba, Mh. Harrison Mwakyembe atafute suluhu katika mgogoro huo kati ya ofisi ya DPP na ofisi ya Mwanasheria Mkuu amesema kama ni madaraka au ni kasma ya pesa ni bora waandae utaratibu mzuri na wamjulishe kama kuna namna bora ya kugawa hayo madaraka kuliko kugombana.
Vilevile amelishukia Jeshi la Polisi hasa ofisi ya Mkurugenzi wa upelelezi na Makosa ya Jinai kuwa wao ndio wanaochelewesha kesi kwa kusingizia kutokamilika upelelezi wa kina.
Mh. Rais amesema "Haiwezekani mtu anakamatwa na meno ya tembo hapohapo kila kitu anacho na bado wapelelezi wanadai bado upelelezi haujakamilika hili haliingii akilini hata kidogo" na amewataka kufanya kazi kwa weledi, wepesi na waache mchezo katika suala la kutoa haki, wafanye upelelezi wa haraka ili kurahisisha haki itolewe kwa muda muafaka
Amesisitiza kuhusu adhabu kwa wakwepa kodi na hata kubadili sheria kuhusu adhabu kwa wakwepa kodi, analipa kodi anayodaiwa na kufungwa, na kama kosa lina adhabu ya faini, kifungo au vyote basi mahakama iwe inatoa adhabu zote kwa pamoja.
Katika tukio lisilotegemewa kuna mama mmoja kutoka Tanga aliibuka na kuwasilisha malalamiko yake katika kesi ya mirathi na jinsi anavyozunguushwa na na ofisi za mwanasheria, polisi na Mahakama vilevile anasema anatishiwa maisha kwa kutumiwa message za kuuawa.
Mh Rais alimsikiliza na kuagiza tatizo lake lishughulikiwe kesi iende haraka kutoka Tanga, vilevile ameagiza huyo mama apewe ulinzi wa polisi popote pale atakapokuwa na amemhakikishia hatauawa
Chanzo: TBC
=========
- Habari hii ni moja kati ya zilizojumuishwa kwenye kipindi cha Jamii Leo katika chaneli yetu ya YouTube.
Kuona habari nyingine zaidi, tazama video hii hapa chini: