Siku ya Saratani Duniani: Saratani ni Ugonjwa wa Pili kwa kuua Duniani huku asimilia 25 ya vifo vya Saratani husababishwa na Tumbaku

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Saratani ni kundi la Magonjwa yanayoweza kuanza takriban kwenye kila Kiungo cha mwili, seli zinapokua kuliko kawaida bila kudhibitiwa. Ukuaji huo unaweza kuvamia viungo vingine vya mwili vilivyo pembeni na kilichoathirika

Hadi mwaka 2018, Saratani ni ugonjwa wa pili kwa kusababisha vifo Duniani, ukiwa umeua takriban Watu milioni 9.6 au ukiwa sababu ya kifo 1 kati ya 6

Takriban asilimia 70 ya vifo vya Saratani hutokea kwenye nchi za kipato cha Kati au kipato cha Chini kutokana na nchi hizo kuwa na vifaa vichache vya Kupambana, Kugundua na Kutibu

Shirika la Afya Duniani limeeleza kuwa huduma za Saratani kwa nchi za Kipato cha Chini na Kati zinatakiwa kuongezwa na iwapo hali itaendelea kama ilivyo, kutakuwa na ongezeko la 60% za Waathirika wa Saratani kwa miongo miwili ijayo

Changamoto zitakuwa kwa Nchi kuchagua aina ya matibabu zikiangalia uwiano wa gharama, uwezekano na ufanisi. Serikali zina jukumu la kuanzisha matibabu fanisi na ambayo Wananchi watayamudu. Itasaidia mapambano ya #Saratani bila ughumu wa Kifedha

ABC5BFCA-41CE-455E-81AC-0D4542D33C64.jpeg


WHO inaangazia hatua za kuzuia Wagonjwa wapya kwa kuzuia Utumiaji wa tumbaku inayohusika na 25% ya vifo vya Saratani. Kutoa chanjo ya Hepatitis B ili kuzuia Saratani ya Ini, kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa kutoa chanjo ya HPV

Aina ya Saratani zinazowakumba sana Wanaume ni Saratani ya Mapafu, Utumbo, Tumbo na Ini

Saratani zinazowasumbua zaidi Wanawake ni Saratani ya Matiti, Utumbo, Mapafu, Mlango wa Kizazi na Shingo (Goita)

Saratani zinazoathiri watu zaidi ni Saratani ya Mapafu (Watu milioni 2.09), ya Matiti (Watu milioni 2.09), ya Utumbo (Watu milioni 1.8). Saratani ya Kibofu (Watu milioni 1.28), ya Ngozi (Watu milioni 1.04) na ya Tumbo (Watu milioni 1.03)

Aina za Saratani zinazoua watu zaidi ni Saratani ya Mapafu (Vifo milioni 1.76), Saratani ya Utumbo (Vifo 862,000), Saratani ya Tumbo (Vifo 783,000). Aina nyingine ni Saratani ya Ini (Vifo 782,000) na Saratani ya Matiti (Vifo 627,000
 
Mkuu wangu MziziMkavu Dr. Sebi namkubali sana, na mimi ni moja ya watu wanaofuata nadharia yake ya alkaline foods and mucus less diet! Ila connection ya kifo cha Nipsey Hussle ndio imekaa kama conspiracy theory zaidi.
 
Back
Top Bottom