Siku ya ndoa; Waliooa/kuolewa huwa inakuwaje.........ambao hawajaoa/kuolewa mnataka iweje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku ya ndoa; Waliooa/kuolewa huwa inakuwaje.........ambao hawajaoa/kuolewa mnataka iweje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by M'Jr, Jun 18, 2012.

 1. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Hii ni siku moja ambayo naamini kwa wale ambao wamekwishapitia siku hii wanaweza kutupa uzoefu wao kidogo wa namna inavyokuwa. Kwa mfano, siku hizi ndoa nyingi zinafanyika wakati binti ni mjamzito so inakuwa kama jamaa kalazimishwa vile.....so wanawake huwa wanahisi vipi hasa ikitokea kwa bahati mbaya bwana harusi akachelewa kufika kanisani, au wanaume huwa mnajihisi vipi pale bi harusi anapochelewa kufika kanisani au hata kuwa na mawazo ya je kama asipotokea au akitokea akasema "hapana"

  Nimezungumzia makanisani kwasababu mfumo wa ndoa za kiislam uko tofauti kidogo na huu wa kikristo wa kusubiriana church. Lakini hata zile za kiislam huwa unahisi vipi pale anapokuwa kaenda kuulizwa mwenzio na we kusubiri jibu kama amesema ndio au hapana?

  Kwenye reception party huwa mnakuwa na feelings gani? Maana kuna wakati kama ni mwanaume wanakuja vidumu vyako au kama ni mwanamke the same, huwa inakuwaje katika kipindi kile cha masaa machache ya reception party?

  Wale ambao hawajaoa/kuolewa mnapenda siku yenu hii iweje?
   
 2. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,852
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Me binafsi napenda iwe kawaida mno.... ikitokea tukakubaliana kwenda church siku ya ibada baada ya ibada tunakwenda kwa mchungaji anatufungisha ndoa co lazima sherehe kuuuuuubwa..... ni mtazano wangu
   
 3. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Niliwahi kuwa na mawazo kama yako, nikawaambia watu siku nikifunga ndoa i want only 50 people kwenye sherehe yangu. One person akanambia dah you wish it was that simple, bahati mbaya that day isnt yours to say what to happen ni watu wengine kabisaaaaa
   
 4. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,852
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280

  Si ndo hapo ndugu yangu, i wish kama maamuzi yangekwua yanatoka kwangu ningefanya ninachotaka co watu wanachotaka, tena utasikia wazazi na ndugu ndo kwanza wanapanga itakavyokuwa co wewe tena... hapo ndo nachoka kabisaaaaaaa
   
 5. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mi huwa nachukia kwasababu 75% ya harusi nilizohudhuria hata huwa siwajui maharusi wenyewe
   
Loading...