Siku ya mashujaa,je wanaenziwa kwa dhati??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku ya mashujaa,je wanaenziwa kwa dhati???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bajabiri, Jul 24, 2011.

 1. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tarehe 25 julai itakuwa ni siku ya Mashujaa,ambapo mashujaa waliomwaga damu kwa ajili ya Tanganyika yao wanaenziwa,mashujaa hawa walipinga ujio wa utawala wa wakoloni kama vile wajerumani na waingereza,pia baada ya kupambana wakolon walishinda na kutawala,pamoja na hayo wakoloni walipoanzisha uchumi wa kikoloni mashujaa hawa walianzisha vita tena,huko songea MAJIMAJI WAR iliibuka,sababu za vita hiyo ni UPORAJI WA ARDHI,KODI KUBWA NA MANYANYASO YA WAKOLONI..........
  Miaka zaid ya 50 baada ya mashujaa hao kuonesha dhamira yao ya kupinga ukoloni,lakini viongoz wa Tanzania sasa wanaonesha kuwa wale wazee walikuwa hawajui walifanyalo,kwa sasa si jambo la ajabu kumuona mtanganyika anapokonywa ardhi,anapigwa na kunyanyaswa na hao wanaoitwa wawekezaji.......

  swali;JE WATANGANYIKA WA SASA HASA HAWA WATAWALA WANAWAENZ VIPI MASHUJAA????

  NAWASILISHA
   
Loading...