Siku ya Mashoto Duniani: Wana JF wenzangu tunaotumia mkono wa kushoto tukutane hapa

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg

SIKU YA MASHOTO DUNIANI

LEO Agosti 13, ni siku ya Mashoto Duniani (International Lefthanders Day). Siku hii imekuwa ikisherehekewa kila mwaka toka Agosti 13, 1976 pale chama cha Mashoto (Lefthanders International) kilipoitangaza siku hii kuwa maalumu kuwathamini mashoto ambao wanatengeneza 10% hadi 15% ya idadi ya watu ulimwenguni huku idadi ya wanaume mashoto ikielezwa kuwa mara mbili ya idadi ya wanawake mashoto.

MADHUMUNI YA SIKU YA MASHOTO

1. Kuwakutanisha mashoto sehemu mbalimbali duniani na kufurahia upekee wao.
2. Lakini pia siku hii inalengwa kuifahamisha dunia juu ya ukweli kuhusu mashoto.

Naomba kukiri (declare interest) kuwa mimi ni mashoto pia. Ninajivunia kuwa mashoto. Lakini pamoja na kuwa kwangu mashoto, namkumbuka sana mwalimu wangu wa chekechea anayeitwa Ellyhoita mwaka 1990 pale kwenye kanisa la KKKT Kiruweni aliyenizuia kuandika kwa mkono wa kushoto. Jambo hili lilinifanya hadi leo kutumia mkono wa kulia katika kuandika.

MILA POTOFU KUHUSU MASHOTO

Kwa miaka mingi, jamii nyingi zimekuwa na mila potofu kuhusiana na mashoto. Wengi wamekuwa wakiita mkono wa kushoto kama mkono wa shetani. Jamii nyingi zimekuwa na kawaida ya kulazimisha kuwabadili watoto wao mkono wa kutumia pindi wagunduapo watoto hao ni mashoto (kama mimi nilivyozuiwa na mwalimu wangu wa chekechea).

Majina mengi mabaya yamekuwa yakitumiwa kwa miaka mingi yakionesha kuwadharau mashoto. Kwa mfano, hapa Tanzania mkono huo umekuwa ukiitwa ‘kono la mavi’. Katika Kilatini, mkono wa kushoto umekuwa ukitwa ‘sinitra’ ambayo humaanisha kitu kiovu.

Kumekuwa na imani kuwa mashoto wengi hukumbwa na vifo vya ajali. Lakini watafiti wamesema kuhusu hilo. Wanakiri kuwa mashoto wengi hukumbwa na ajali kutokana na ukweli vitu vyote vimetengenezwa kwa ajili ya matumizi ya mkono wa kulia. Mathalani, vyombo vya moto na vyombo vingine vya matumizi ya kila siku vinawapa upendeleo wanaotumia mkono wa kulia. Kwa maana hiyo mashoto hulazimika kufoji matumizi.

MTAZAMO CHANYA KUHUSU MASHOTO
Huko Peru, Amerika ya Kusini, kwenye jamii ya Inca, mashoto wanaaminiwa kuwa na uwezo mkubwa sana kiroho na uponyaji. Mtawala wa tatu wa jamii hiyo aliyekuwa mashoto alipewa jina la Lloque Yupanqui likiwa na maana ‘Mashoto aliyebarikiwa’.

Katika Ubudha, mashoto huhesabiwa ni wenye hekima zaidi.

Huko Urusi, mashoto ambao huitwa ‘Levsha’ huhesabiwa kuwa ni mafundi stadi zaidi wa kazi za mikono.

Uchina na Ujapani, mashoto huhesabiwa kuwa ni wabunifu na wachapa kazi zaidi.

UKWELI KUHUSU MASHOTO
Sababu za msingi hasa kwa nini watu huzaliwa mashoto hazijawa wazi hadi sasa. Lakini watafiti wengi wanasema mashoto hutokana na vinasaba (genetics) na sababu za kimazingira. Inaelezwa kuwa wazazi wote wawili wakiwa mashoto, upo uwezekano wa asilimia 50 kuzaa mashoto, wakati wazazi wote wawili kama si mashoto, wana uwezekano wa asilimia 2 kuzaa mashoto.

Mashoto, kwa mujibu wa utafiti, huongozwa zaidi na upande wa kulia wa ubongo, wakati wanaotumia kulia huongozwa zaidi na upande wa kushoto wa ubongo. Kwa kuwa mashoto huongozwa na upande wa kulia, watafiti wanasema mashoto ni watu wenye uwezo mkubwa zaidi kiakili. Pia wana uwezo mkubwa zaidi katika sanaa, muziki na ubunifu kwa ujumla. Mashoto wanaelezwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa utambuzi (perception). Watafiti wanaeleza pia kuwa mashoto wana mhemuko, mchomo wa moyo ama hisia (emotions) kwa kiasi kikubwa zaidi. Hivyo mashoto wanaelezwa ni watu wenye upendo na huruma kwa kiwango cha hali ya juu sana.

Kwa mujibu wa utafiti wa Dr. Alan Searleman wa Chuo Kikuu cha Mt. Lawrence huko New York, Marekani, mashoto wana uwezo mkubwa zaidi wa utatuzi (problem-solving skills).

Mashoto wana uwezo mkubwa sana wa kutunza kumbukumbu kiasi kwamba wengi wao hawatumii shajara (diary) na hawapendi kutumia notebooks wanapomsikiliza mtu akitoa mhadhara.

Mashoto wana mzio (allergies) zaidi (Hili linanihusu kwani nina mzio hasa kwa baadhi ya vyakula) .

Mashoto wana tatizo la kukosa usingizi (insomnia) (hili nalo ni tatizo ambalo hunipata mara kwa mara).

Mashoto huchelewa kupevuka ama kubalehe kwa miezi 4 hadi 5 ukilinganisha na wanaotumia kulia.

Mashoto wana uwezo mkubwa zaidi wa kufikiria na kutambua mambo hususani katika teknolojia.

Mashoto wana uwezo mkubwa zaidi wa kufanya mambo mengi sana (multi tasking). Utafiti wa Dr. Nick Cherbuin wa Chuo Kikuu cha London unaonesha kuwa mashoto wana uwezo mkubwa zaidi wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na ndiyo sababu ni wazuri zaidi hata kwenye video games.

Mashoto wana vipaji vingi zaidi. Mashoto mmoja anaweza kuwa mchoraji, mshairi, mcheza mpira, mchonga vinyago, mwandishi wa hadithi, mbunifu wa mitindo, mbunifu wa bustani, mcheza filamu, mpigapicha, mpambaji, mwanamuziki na vingine vingi.

Wastani wa umri wa kuishi wa mashoto ni miaka 9 pungufu ya wastani wa wanaotumia mkono wa kulia.

Mashoto wana uwezo mkubwa zaidi wa kuona chini ya maji.

Mashoto waliopo vyuoni hufanikiwa kwa asilimia 15 zaidi ya wanaotumia kulia. Na baada ya kumaliza vyuo, mashoto huwa na mafanikio kwa asilimia 26 zaidi ya wengine. Mtafiti Chris McManus katika kitabu chake cha ‘Right Hand, Left Hand’ amesema kuwa mashoto wameonesha kuwa ni watu wenye mafanikio kwa kiwango kikubwa zaidi.

Mashoto wengi baada ya masomo hufanya kazi za ubunifu zaidi kama uandishi, ushairi, muziki, uigizaji na sanaa yote kwa ujumla. Hata wanaofanya kazi zingine, huwa ni wenye kupenda ubunifu zaidi katika kufanikisha kazi zao.

Katika wabunifu watano wa kwanza wa kompyuta za Mcintosh, wanne kati yao walikuwa mashoto.

Mashoto ni wachoraji wazuri zaidi, lakini huchora michoro mingi ikiwa imeelekea upande wa kulia.

Katika marais wanne wa hivi karibuni wa Marekani, marais watatu ni mashoto. Tazama, George Bush mkubwa (mashoto), Bill Clinton (mashoto), George Bush mdogo (kulia) na Barack Obama (mashoto). Na, katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 1992, wagombea wote watatu wakubwa walikuwa mashoto. Uchaguzi wa Marekani wa 2008, wagombea wote wawili Obama na McCain ni mashoto.

Katika keyboards za QWERTY, mkono wa kushoto peke yake huweza kuchapa maneno 3400 ya Kingereza wakati mkono wa kulia peke yake huweza kuchapa maneno 450 tu ya Kingereza. Mfano wa maneno marefu ya Kingereza ambayo huchapwa na mkono wa kushoto peke yake katika keyboard ya QWERTY ni; desegregates, reverberated, watercress, aftereffects, na pia sweaterdresses.

Mashoto wana miandiko (handwriting) mizuri na yenye kuvutia mno. Na wanao uwezo mkubwa wa kuandika maandishi (herufi na tarakimu) kwa kinyume (toka kulia kwenda kushoto)

Mashoto wanapenda zaidi wanyama. Jambo la kusisimua ni kuwa dubu (bear) wote ni mashoto. Mashoto wa kiume huwapenda sana paka, na jambo la kushangaza zaidi paka wote wa kiume ni mashoto. (Naomba kukiri kuwa hili nalo pia linanihusu kwani mimi binafsi napenda sana wanyama hasa paka).

Asilimia 50 ya mashoto hutumia mouse za kompyuta kwa mkono wa kulia, asilimia 68 hushika mkasi kwa mkono wa kulia, na asilimia 74 hushika kitu cha chakula kwa mkono wa kulia na uma kwa mkono wa kushoto.

Watafiti wa Kikanada wanasema mashoto wanamudu kwa kiasi kikubwa zaidi kuyazowea mazingira yoyote yale. Ingawa vitu vingi vya utumizi kama milango, magitaa, visu, mikasi, magari na kadhalika vimewapendelea wanaotumia mkono wa kulia, ni mashoto ndio wanaovimudu zaidi.

Mashoto wanajiamini zaidi na ni majasiri zaidi.

BAADHI YA WATU MAARUFU DUNIANI AMBAO NI MASHOTO
Marais wa Marekani: James A. Garfield, Herbet Hoover, Harry S. Truman, Gelard Ford, Ronald Reagan, George H. W. Bush, Bill Clinton na Barack Obama.

Watu maarufu katika historia: Joan of Arc, Napoleon Bonaparte, Julius Caesar, Michelangelo, Leonardo da Vinci, Raphael na Hellen Keller, Alexander The Great, Malkia Victoria, Mfalme George II, Mfalme George VI, Prince Charles, Prince William, Henry Ford, Benjamin Franklin, Steven Forbes na Oprah Winfrey.

Wanasiasa maarufu: Benard Membe, Fidel Castro, Ross Perot, Bob Dole, John McCain, Robert S. McNamara, Benjamin Netanyahu, Ehud Olmert na Brig. Jen. Lee Hsien Look na Uhuru Kenyatta.

Wanamuziki maarufu: Phil Collins, Paul McCartney, Ringo Starr, Jimi Hendrix na George Michael.

Waandishi na washairi: James Baldwin, Bet Bowen, Samuel C. Warner, Viktoria Stefanov, Diane Paul na Richard Condon.

Wacheza filamu: Charlie Chaplin, Tom Cruise, Robert de Niro, Whoopie Goldberg, Bruce Willis, Kadeem Hadson, Angelina Jolie, Marilyn Monroe, Nicole Kidman, Cary Grant, Julia Roberts,

Wacheza soka maarufu: Pele, Diego Armando Maradona, Lionel Messi, Gareth Bale, Romario, Griezmann na Hugo Sanchez.

Wana JF watumia mkono wa kushoto:Mimi barafu na .........(jitajeni)

MWISHO
Natoa wito kwa wazazi na walimu wote kutokuwazuia watoto kutumia mkono wa kushoto katika kufanya mambo mbalimbali. Kwani kama tulivyoona mashoto wana vipaji vingi sana. Kumzuia mtoto kutokutumia mkono wa kushoto kunaweza kuchangia katika kudidimiza vipaji vyake. Tuache asili ifanye kazi yake, tusiizuie.

Credit to Fadhy Mtanga.......

HAPPY "MASHOTO DAY"
 
Babu yangu mzaa baba ni mashoto, baangu, baba wadogo zangu wawili ni mashoto.
Mimi na kakaangu ni mashoto.

Hivi wakuu nini husababisha tuwe mashoto wengi namna hii kwenye familia?
Bora nyie ni selective, sisi nyumbani anetumia mkono wa kulia ni baba tuu,
Sisi tuko tisa kutoka tumbani mwa mama yetu lakini sote ni mkono wa kushoto na miguu pia, kwani nakumbuka miaka ya mwishoni mwa tisini kaka angu alikua akicheza namba kumi na moja na mimi nilikuwa kipa wa timu pinzani nanyeye kunifunga alikuwa napata kazi sanaa
 
Mimi ni mashoto mpaka kula. Kwetu pia mashoto ni wengi sana
Mimi mpaka kula pia,nilichapwa sana mkono wa kushoto kuanzia shuleni mpka nyumbani nikawa sugu.
Mwalimu wangu wa mwandiko aliitwa Mwalimu Nyabi,ikafikia kipindi akaamua kuniacha,mpaka sasa ni mwendo wa kushoto kuanzia kula mpka kuandika...Halafu mambo ya mkono wa kushoto kwa wengi,mimi nafanya na mkono wa kulia....Bahati nzuri mpaka kutomasa kushoto kunakuwa na nguvu kuliko kulia
 
mimi
View attachment 380801

pia najivunia kuwa Mashoto na shuleni nilipitia changamoto kama hizo ispokuwa bado natumia mkono wa kushoto kuandika..niliandikia mkono wa kulia wakati wa kipindi ki
fupi nikiwa shule ya msingi baada ya kuumia mkono wa kushoto,,,nilipopona nikaendelea na mashoto yangu kama kina Uhuru Kenyata na Obama...viva mashoto!!
 
Bora nyie ni selective, sisi nyumbani anetumia mkono wa kulia ni baba tuu,
Sisi tuko tisa kutoka tumbani mwa mama yetu lakini sote ni mkono wa kushoto na miguu pia, kwani nakumbuka miaka ya mwishoni mwa tisini kaka angu alikua akicheza namba kumi na moja na mimi nilikuwa kipa wa timu pinzani nanyeye kunifunga alikuwa napata kazi sanaa
Hata sisi pia ni mashoto kuanzia miguu mpaka mikono
 
Back
Top Bottom