Siku ya Maalim Seif, nyongeza yangu kwa Mohamed Ghassani

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,205
Somo yangu Mohammed Ghassani kaandika anasema, ''Japokuwa aliondoka duniani akiwa hajawahi kuwa rais wa serikali, hilo halikumnyima nafasi yake ya kuwa baba wa utaifa wa Zanzibar - alama kamili ya Uzanzibari na shujaa wa Wazanzibari.''

Ningependa nami niongeze kitu kidogo katika hayo maneno yake.

Maalim katika uhai wake kagombea jumla ya chaguzi sita na inasemwa ''hakushinda.''

Hapa ndipo kilipo kitendawili na swali zito kuhusu ''ushindi,'' wa marais wote waliotawala Zanzibar baada ya kugombea urais wa Zanzibar na Maalim.

Hili ni somo bora likaachiwa wanahistoria wa kesho waje walifanyie utafiti.

Lakini kwa leo ukweli hakuna asiyeujua.

Waingereza wanamsemo, ''Hearts of hearts,'' yaani unadhani unajua lakini ukijuacho si kweli.

Marais wa waliotawala Zanzibar iko siku labda wataandika kumbukumbu zao na naamini katika mambo ambayo wasomaji watataka kujua ni vipi marais hawa, ''walimshinda,'' Maalim.

Nilikuwapo Zanzibar uchaguzi wa kwanza mwaka wa 1995.

Nimeandika mengi kuhusu uchaguzi huu katika shajara yangu kwa niliyoona kwa macho yangu na kushuhudia na yale niliyosikia.

Lakini kubwa ambalo hadi leo bado sijaweza kusahau ni barua ya Ali Ameir kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar akikataa matokeo.

Ali Ameir alikuwa anapinga ushindi wa Maalim.

CCM Zanzibar kutokana na uchaguzi ule wa mwaka wa 1995 ilikuwa imesomeshwa somo muhimu sana.

Chaguzi zote zilizofuatia ni nakala ya huu uchaguzi wa kwanza mwaka wa 1995.

1644468312566.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom