Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Oct 10, 2009.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Salaam,

  Leo ni siku ya kimataifa ya kupinga adhabu ya kifo.
  Maadhimisho ya kitaifa yameandaliwa na Mtandao wa Mashirika ya Utetezi wa Haki za Binaadamu kwa nchi za Kusini mwa Afrika tawi la Tazania-SAHRINGON na yafanyika ndani ya ukumbi wa Saba Saba, Kilwa Rd.

  Hii ndio ratiba yake

  MARKING THE WORLD DAY AGAINST DEATH PENALTY IN TANZANIA


  PROGRAMME, OCTOBER 10, 2009  Sabasaba International Trade Fair grounds, Ngorongoro hall, Dar es Salaam


  07:00-Arrival and registration-Secretariat
  08:30-Peaceful Match from Kituo cha Uhasibu to Viwanja vya Sabasaba-Participants
  09:30-The Guest of Honour Welcomes Matchers-Hon. Chief Justice Barnabas Samatta (Retired)
  09:45-Introductory remarks-Chairperson Board of Directors of SAHRiNGON Tanzania Chapter
  09:55-Objective of the Day against Death Penalty-Executive Director - LHRC
  10:05-Statement on Death Penalty in Tanzania-Hon. Chief Justice Barnabas Samatta (Retired)
  10:25-Launching of NGO Report on the Implantations of the International Covenant on Civil and Political Rights in Tanzania & Concluding observations of the UN Human Rights Committee -Hon. Chief Justice Barnabas Samatta (Retired)
  10:35-Testimony-William Mwaikambo Kaleba
  10:45-Discussion and Sharing of Experience from Abolitionists-All
  11:00 -Break
  12:00-1st Presentation; Status of Implementations of International Instrument in Tanzania -Ms. Juliana Masabo
  2nd Presentation; Challenges for Abolishing Death Penalty in Tanzania-Mr. Harold Sungusia
  13:10-Discussion-All
  13:40-Closing Remarks-National Coordinator SAHRiNGON Tanzania Chapter-Mrs. Martina M. Kabisama

  NB. Pia nimepata statement ya EU Naiambatanisha
   

  Attached Files:

 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Kundi kubwa la wapinga adhabu ya kifo, limekusanyika kituo cha daladala cha Taasisi ya Uhasibu, TIA, Kilwa Rd huku wamevalia t-shirt nyeupe zenye chater ya SAHRINGON, idadi kubwa ya washiriki wa maandamano nawaona kama ni vijana wadogo au wanafunzi fulani hivi...
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Maandamano ya amani yamejipanga tayari kuanza, kwa sasa waandamanaji angalau wamekuwa wengi wengi, ile sura ya vijana wadogo na watoto wa kishule-shule imefutika, sura za kuiuuuzima zimetanda tanda. pia naiona bendi ya polisi iko mkao wa kuongoza maandamano haya.
   
 4. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni matumaini yangu kuwa hawa wanaopinga adhabu ya kifo watawahakikishia albino wa Tanzania usalama wao . Bila kutishia kunyongwa kwa wanaowakata viungo albino, naamini hatutaondokana na hii aibu ya kishirikina na ujinga.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nadhani most of those participants watakuwa ni watu ambao kwa namna moja ama nyingine wameumizwa na adhabu hii, directly au indirectly.

  Mimi mwenyewe bado nina tug-of-war kichwani mwangu whether adhabu hii iendelee kuwepo ama la! Najua wengi pia mpo hivyo.

  Hakuna mtu kati yetu ambaye hajaathiriwa na watu hawa wanaohukumiwa kwa adhabu za vifo! Aidha wamewapoteza ndugu zetu ambao tuliwapenda sana, ama kutudhuru kwa namna nyingineyo!

  Kila la heri kwao!
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  muda wote nimekuwa nawashangaa sana hawa wanaharakati......wanapinga adhabu ya kifo wakati vibaka kila kukicha wanapigwa hadi kufa na kuchomwa moto lakini sijawahi kumsikia hata mwanaharakati mmoja akipinga vitendo vya watu kujichukulia sheria mkononi.....wanapinga adhabu ambayo kimsingi huwa haitekelezwi.............
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  hata
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Maandamano yanaongozwa na bendi ya polisi, yanaingia, yanapokelewa na mgeni rasmi, Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Barbabas Samatta.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  National Co-ordinator wa Saharingon Tanzania Chapter, Bibi Martha Kabisama Aametoa makaribisho rasmi na kutambulisha wageni mbalimbali, miongoni mwao ni Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya, balozi Tim Clarke na Balozi wa Sweeden nchini, jina gumu gumu kuliandika, pia wako wawakilishi wa taasisi mbalimbali za haki za binaadamu.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi wa Legal and Human Rights Center ndiye amemkaribisha mgeni rasmi kuzungumza. Hivi sasa Jaji Samatta ndio anazungumza sasa.
  Jaji Samatta amekiri kuwa majaji wanatoa adhabu ya kifo kwa mujibu wa sheria za nchi.
  Amekiri kunauwezekano mtu asiye na hatia kuhukumiwa kifo bila hatia, na imeshatokea na kuna wengine wanakutikana na adhabu hiyo na baada ya utekelezwaji, ndipo ukweli unakuja kujulikana kuwa aliyeuwawaw hakuwa na hatia.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Jaji Samata ametoa wito kwa Bunge kuifutilia mbali adhabu ya kifo na zitungwe adhabu mbadala, Tume ya Kurekebisha sheria ilishatoa ripoti yake kuhusu adhabu ya kifo ila serikali imeikalia. Jaji Samatta ametoa ombi kwa serikali kuitoa ripoti kwa mujibu wa sheria, amecite kifungu cha sheria kinachompa raia haki ya kupata habari na hivyo serikali ni lazima iitoe ripoti hiyo kwa public.
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Hii hotuba ya Jaji Samatta ni kama mwiba mchungu kwa serikali, wanahabari waioko hapa wataishusha magazetini kesho, naona pia na tv zote wapo, hivyo leo jioni na kesho asubuhi itashushwa kwenye taarifa za habari. Nadhani tasnia ya judiciary watamuhukumu kama ule ukosoaji wa Kitine.
  Swali hivi hayo aliyoyasema jaji Samatta leo, hakuyaona wakati akiwa kwenye kiti, katoka sasa ndio anaona kiti kina matobo!.
  Nadhani kwa mujibu wa shria zetu, majaji wanauwezo wa kutunga sheria kwa utaratibu wa ruling bmbalimbali ama wana power za kuzi scrap from the books of laws all bad laws.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi kuna igizo la adhabu ya kifo, ila pia lazima tukubali, adhabu ya kunyongwa ni barbaric, japo Sdan alifanya maovu mengi Iraq, wananchi wake walimpenda, mimi binafsi sikufurahishwa na utekelezaji wa haraka haraka hukumu ile na kukimbilia kumnyonga mbio mbio. Kunyonga ni mateso na udhalilishaji, afadhali wenzetu wamerekani, wao wanaitekeleza kwa electrical chair au lether dose, sumu ya cynide ambayo inauwa haraka bila mateso.
  Tena sisi tunaonyonga ni afadhali kuliko waarabu wao wanachinja kichwa hadharani siku ya Ijumaa baada ya Swala ya Ijumaa.
  Ichi za kijeshi inatekelezwa na firing squad.
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Kujichukulia sheria mikoni kumepingwa sana
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Bwana William Mwaikambo Kaleba anatoa ushuhuda wa ajabu sana kuhusiana na utekelezaji wa adhabu ya kunyonga. Yeye alihukumiwa kunyongwa amekaa gereza la Isanga kwa miaka kadhaa, anadai ameshuhudia wafungwa 35 wakinyongwa!.
  Anasimulia morbid curiosity na ghastly graphic details jinsi bwana nyonganyonga anavyotekeleza adhabu hiyo.
  Kwa kweli ni unyama wa ajabu'''
  Inatisha na Inasikitisha...
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Kumbukumbu rasmi zinasema Nyerere alinyonga 2 akiwemo Mwamwindi. Mwinyi alinyonga 8. Mkapa hakunyonga, JK bado hajanyonga. Sasa hawa 35 aliowashuhudia ni wapi?. Hii inamaana adhabu hii huwa inatekelezwa off the record.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Mingoni mwa mateso ya wanaohukumiwa kunyongwa, ni pamoja na kufungwa minyororo mikononi na miguuni, kukaa chumba vyomba vya peke yao, kutengwa kutoongea na watu, wanapata dhihaka kwa mabwana jela.
  Siku ya kunyonga huwa ni Jumamosi asubuhi, Ijumaa ndio huletewa taarifa kuwa siku yako ni kesho, huja daktari kukupima afya yako ili unyongwe ikiwa fit, kama ukikutwa unaumwa kunyongwa kwako kunaahirishwa.
  Kwa wafungwa wa kunyongwa wengine huwa ni siku ya huzuni, na wengine waliojichokea na mateso ya kusubiri kunyongwa, huwa na furaha kukubali bora wanyongwe yaishe.
  Kumbe ukihukumiwa kunyongwa, mwili wako haurushwi kwa ndugu zako, ni serikali ndio huwa inakufukia mahali kusikojulikana bila kuweka alama yoyote .
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Ushuhuda wa huyu jamaa William Mwaikambo Kaleba, ni very controversial, anesema amekaa Isanga miaka 15 na kushuhudia watu 35 wakinyongwa!. Ametoka jela mwezi April Mwaka huu kwa msamaha wa rais wa Sikukuu ya Uhuru Desemba 9, 2008.

  Ninachofuhamu mimi, msamaha wa rais huwa hauwahusishi waliohukumiwa kifo wala wafungwa wa kifungo cha maisha, kitendo cha jamaa huyu kulamba msamaha ni issue.
  Alipokuwa akieleza jinsi watu wanavyonyongwa, ni total morbid sensetional, yaani unayaeleza matukio ya ukatili wa ajabu in a sensesional manner, it was too much for public consuption, kama wapenzi wa horor, ni really horific experience.
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Yote ni tisa, kumi ni hii ya kushuhudia live kwa macho yake watu 35 wakinyongwa!. Kwa vile jamaa kakaa jela miaka 15. 2009-15 unabaki na 1994.
  Hii maana yake aliwashudia wale wote 8 waionyongwa kipindi cha Mwinyi. Hii maana yake wote walionyongwa kipindi chote cha miaka 10 ya Mwinyi, walinyongwa mwaka wa mwisho wa Mwinyi yaani 1994-5.
  Kama ni kweli hao 35 aliowashuhudia, 8 ndio wale wa Mwinyi, wanabaki watu 27. Hii inamaana hao 27 amewashudia wakinyongwa kipindi cha Mkapa!. Records zinaonyesha Mkapa hakusaini death sentence hata moja. Hizi taarifa za huyu bwana ama ni uwongo, kama ni kweli ina maana mbili, 1.Rais alisaini death warrants zao na hukumu ikatekelezwa lakini hawakuweka kwenye record ili ionekana Mkapa ni Mr. Clean. 2. Ni kweli Mkapa hakusaini death warrant yoyote, hawa 27 wamenyongwa awamu ya JK tangu alipoingia 2005 mpaka hiyo April 2009 jamaa alopoachiwa.

  Kwa vile maadhimisho yanaendelea, nitajaribu kumsaka jamaa huyu kwa ufafanuzi kidogo.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  .
  Hakuna uthibitisho kuwa kutoa adhabu ya kifo kwa wauaji wa Albino kutapunguza vifo vya Albino, dawa sio adhabu ili kutoa vitisho, dawa ni kudeal na the motive behind mauaji hayo. Uhamasishaji ufanyike kuondokana na sababu zinazopelekea mauaji hayo.

  Uingereza na nchi za Ulaya hakuna adhabu ya kifo, Marekani bado ina adhabu ya kifo, utafiti umethibitisha kuna vitendo vingi zaidi vya mauji nMarekani kuliko Ulaya, hivyo adhabu ya kifo haizuii vitendo vya mauaji.

  Utekelezaji wa adhabu hii ni mauaji pia, hivyo huna sababu ya kutoa adhabu ya kifo kwa muuaji kwa kumuua sio adhabu bali ni kulipiza kisasi au kumkomoa, hamsaidii kitu muuaji, wala haiwasaidii waliofiliwa ndugu yao kwa sababu haiwarudishii uhai wa ndugu yao, sana sana ni kujiplease tuu, 'kamuua ndugu yetu, nae kauliwa'
   
Loading...