Siku ya kufa kwangu!

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165
Naomba wakati unasoma hii habari uwe peke yako na uwe umetulia, bila kubughudhiwa.
Hakikisha hakuna unaloliwaza wakati unapoanza kusoma kwani hiyo itakusaidia kung'amua kile ninachomaanisha katika habari hii.

Naomba usiwe mwoga, kwani ni habari ambayo itakufunza jambo fulani katika maisha.
Haya ungana nami katika kusoma habari hii.

Katika akili yako hebu hisi kama vile unajiona, yaani tengeneza taswira kama vile unajiona ukiwa unaenda kuhudhuria mazishi ya mtu umpendae na unayemfahamu. Jione ukiwa unaendesha gari kuelekea kanisani ambapo ndipo mahali watu wanapokusanyika kuuaga mwili wa marehemu kabla ya mazishi.

Unapofika pale unapaki gari lako na kutoka kuelekea ndani ya kanisa, unapoingia ndani ya kanisa unaona kumepambwa na maua mazuri yenye kunukia na huku ukisikia ala za muziki mororo. Wakati ukielekea kwenye eneo ulilopangiwa kukaa unawapita ndugu, jamaa na marafiki wakiwa na nyuso zenye huzuni na majonzi yenye kuashiria kusikitishwa na kuondokewa na mtu waliyempenda sana.

Unapokaribia kufika kwenye nafasi uliyopangiwa kukaa, unapita karibu kabisa na sanduku lenye mwili wa marehemu na unapotazama mwili ulioko ndani ya sanduku hilo unastuka kuona mwili ulioko ndani ya sanduku hilo ni wa kwako!
Mara kuna sauti inakwambia "haya ni mazishi yako yatakavyokuwa miaka mitatu ijayo kuanzia sasa"
Watu wote walioko pale wamekuja kuonyesha mapenzi yao kwako na kukupa heshima kwa kuuaga mwili wako ili ukapumzike kwa amani.

Duh! Unashusha pumzi na kuketi, ili kusubiri ibada ianze. Unapoangalia ratiba ambayo ulipewa wakati unaingia pale kanisani unakuta wamepangwa wazungumzaji wanne, wazungumzaji wa kwanza wanatoka katika familia yako, mmoja wa watoto wako, mmoja wa kaka zako, dada zako, binamu, shangazi, mjomba, baba mdogo, mama mdogo, bibi, babu na ndugu wengine wa karibu ambao walisafiri maili nyingi ili kuja kushiriki mazishi yako.

Mzungumzaji wa pili ni mmoja wa marafiki zako ambaye mlishibana sana, mzungumzaji wa tatu ni kutoka katika mahali pako pa kazi na mzungumzaji wa nne ni kutoka katika kanisa unalo Sali au kutoka katika taasisi ya kijamii ambayo ulikuwa ukishiriki katika kuihudumia jamii baada ya muda wako wa kazi.

Sasa hebu fikiria kwa makini sana. Ungependa wazungumzaji hawa wazungumze nini juu ya maisha yako hapa duniani? Wewe ni mume, mke, baba au mama wa aina gani? Wewe ni mvulana, msichana, binamu, wa aina gani? Ni rafiki wa aina gani? Ushirikiano wako na wafanyakazi wenzako ulikuwaje?

Ungependa wakuzungumzieje? Ulikuwa ni mtu mwenye tabia gani kwa ujumla? Uliisaidiaje jamii, ulifanikiwa katika lipi? Ungependa wakukumbuke kwa lipi? Hebu waangalie kwa makini watu waliokuzunguka. Kama ungepewa nafasi, ungeyabadili vipi maisha yao?
Kama umesoma kwa makini habari hii naamini kuna jambo utakuwa umejifunza.
Nimegundua kuwa ili ujue kuwa wewe ni mtu wa namna gani ni vyema ukahudhuria mazishi yako mwenyewe………………


Tafakari…………….

Habari hii nimeitoa katika kitabu cha The 7 habits of highly effective people cha Stephen R Covey.
 
Kama ungepewa nafasi, ungeyabadili vipi maisha yao?
kwakweli nimelia kwani story hii imenikumbusha siku niliyompoteza best yangu! niliingia kanisani nikasema dah jamaa ndiyo amelala hivyo! what if I was I? Je, yeye angelia? Watu ndiyo wangelia kama hivi? Maisha ya mwanadamu ni mafupi sana! Lets do good always!
 
siku ya kufa kwangu mm siifaham,hivyo yabidi sasa niyatengeneze maisha,mwili wangu ukiwekwa kaburini ndugu zangu wakinizunguka kwa uzuni kila mmoja na lake moyoni wengine wakiuzunika na wengine kufurahi,baad ya kufukiwa sijui ni mchwa,mafinyofinyo,nyoka etc eeh Mungu!
 
siku ya kufa kwangu mm siifaham,hivyo yabidi sasa niyatengeneze maisha,mwili wangu ukiwekwa kaburini ndugu zangu wakinizunguka kwa uzuni kila mmoja na lake moyoni wengine wakiuzunika na wengine kufurahi,baad ya kufukiwa sijui ni mchwa,mafinyofinyo,nyoka etc eeh Mungu!

wengine wakiwaza kukosa ucheshi wako wengine wanalia deni lao umekwenda nalo,wngine watalia misaada ulokuwa unawapa ndo basi tena,wengine watafurai kimoyoyo japo awajui nao watakufa lini. ila unajua nn usiogope kifo kwani akikwepeki kikubwa jua kusudi la mungu juu ya maisha yako na kulisimamia na kutenda mema kwa watu wote
 
acheni kuongelea ongelea vifo!ni dalili za depression,kwanza mtu ukifa hao watu walioteuliwa kusoma risala watasema maneno mazuri tu as if u were an angel,na wengine watalia machozi yasiyotoka moyoni,cha msingi tenda mema,tafuta maendeleo az if hakuna kifo,hayo ya watu watasema nini tayari tunajua yanayosomwa ktk risala za mazishini,mi sijawahi kusikia risala ya mazishi ikisema"tunasikitika kumpoteza lkn alikuwa hatari sana kwa kuiba waume za watu".
 
Nimeshindwa hata cha kuandika! nimekumbuka kifo cha wapendwa wangu ahh ahhh ngoja niendelee kulia!
 
acheni kuongelea ongelea vifo!ni dalili za depression,kwanza mtu ukifa hao watu walioteuliwa kusoma risala watasema maneno mazuri tu as if u were an angel,na wengine watalia machozi yasiyotoka moyoni,cha msingi tenda mema,tafuta maendeleo az if hakuna kifo,hayo ya watu watasema nini tayari tunajua yanayosomwa ktk risala za mazishini,mi sijawahi kusikia risala ya mazishi ikisema"tunasikitika kumpoteza lkn alikuwa hatari sana kwa kuiba waume za watu".

im behind you....er i mean nakuunga mkono 100%
 
Mtoto anapozaliwa huwa analia wakati waliomzunguka wanatabasamu, yatupasa tuishi maisha yetu vizuri ili siku tutakapokufa tuwe tunatabasamu wakati waliotuzunguka wanalia kwa uchungu wa kutupoteza.
 
Nijuavyo mimi, maongezi yote rasmi ya shughuli za mazishi hayamsaidii kitu yule marehemu!

Chukua kioo(morror) ukitazame, unaona sura yako mwenyewe...hii ni sawia na maongezi ya mazishini, yanamlenga marehemu, lakini yanatakiwa yakutengeneze wewe uliyebaki!

Kuna mtumishi wa Mungu mmoja alipata kusema kuwa Mungu anafanya kusudi kumtwaa mtu wake, ili kupitia huyo mfu, basi alete ujumbe kwa wanaobaki!..
Namnukuu,.."tazama ndugu zangu, panapo mzoga ndipo pakusanyikapo tai(ndege)"..., akimaanisha kuwa cha maana hapo ni kusanyiko la tai, yaani wale watu wanaokuja kumuomboleza marehemu! Hawa ndio wanaopaswa kufaidika na kutwaliwa kwa mwenzao!

Tubadili maisha na kujiandaa brethren!
 
"Maisha ya mtu yana hatua tatu: binadamu, punda, na mbwa" -- M. C. Tito, Novemba 19 2007.

1. Hatua ya binadamu: - utotoni mpaka ulipofikia hatua ya punda. Utoto ni furaha tupu, tabu itoke wapi?
2. Hatua ya Punda - mtu mzima majukumu. Somesha huyu, lisha yule, suluhisha mgogoro huu, patanisha wale, ozesha huyu, zika yule... 'jamii inakutegemea'. Kila kukicha afadhali ya jana.
3. Hatua ya Mbwa - umezeeka, hata kukimbia huwezi tena. Ile mizigo uliyoibeba ukiwa 'punda' ushaikabidhi kwa wengine. Wewe unabaki "kubweka" tu, maana unahitaji kusaidiwa karibu kila kitu. Grumpy old person.

AYUBU 14:1-2, "Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke,. siku zake za kuishi si nyingi, nazo hujaa taabu."

Mpe Yesu Maisha kujiandaa na Umilele baada ya kifo...maisha yako utayatumia wapi milele?

Mlenge
 
Back
Top Bottom