Siku ya Kimataifa ya Wanawake - Naomba kuuliza

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Messages
2,404
Points
1,225

MwanaHaki

R I P
Joined Oct 17, 2006
2,404 1,225
Naomba kuuliza maswali mawili tu!

1) Leo ni kilele cha Siku ya Kimataifa ya Wanawake (International Women's Day). Je, Siku ya Kimataifa ya Wanaume ipo? Na kama ipo inaadhimishwa lini? Na kama haipo ni kwa sababu gani?

2) Nchini Tanzania kuna sheria inayoitwa Sexual Offences Special Provisions Act (SOSPA), ambayo inahusiana na masuala yote ya udhalilishwaji, unyanyasaji na makosa mengine yanayotokea, hususan wanapoathirika ni wanawake. Ni nadra sana kusikia wanaume wakiathirika na unyanyasaji au udhalilishwaji wa kijinsia.

Mara nyingi wanaoathirika huwa katika ndoa, lakini inapotokea anayeathirika ni msichana ambaye ananyanyaswa na mwenza (boyfriend) wake, na haswa kama mwenza huyo ni mtu mwenye uwezo kifedha, mara nyingi anayenyanyaswa huwa na hofu kiasi cha kumkimbia na hata kuhama nchi.

Kimenitokea kisa ambacho nimekutana na binti mdogo, miaka 24, ambaye hata chuo kikuu amesitisha masomo yake kwa sababu ya unyanyaswaji anaokutana nao kutoka kwa boyfriend wake huyo, ambaye analazimisha mapenzi... anatamba kwamba ana uwezo mkubwa, amewaweka maofisa wa polisi mfukoni, na kadhalika!

Je, kuna sheria gani ya kuwabana watu kama hawa? Au nini kifanyike kuwasaidia dada zetu wasinyanyasike?

./mwana wa haki
 
Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Messages
4,155
Points
1,250

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2006
4,155 1,250

mwana haki jibu la swali la kwanza limo kwenye maelezo yako ya pili. mara nyingi mnyanyasaji ni mwanaume kwa hio hakuna haja ya kuwa na siku ya wanaume.

pili shida wanazokumbana nazo wanawake na mchango wao ktk jamii nyingi ulidharaulika na kutoonekana kama ni mchango muhimu kwa hio kuwepo siku hio ni moja ya kujiliwaza na kujipa moyo kina mama ktk harakati zao za kujikomboa.

pia kuipa nafasi jamii kuelewa na kuthamini mchango wa wanawake ktk jamii zetu.

ama kuhusu maelezo ulioeleza ya huyu msichana anapaswa aende ktk vikundi vya kinamama kama tamwa na wengine watamsaidia
 
Siao

Member
Joined
Jan 4, 2008
Messages
96
Points
0

Siao

Member
Joined Jan 4, 2008
96 0
Wanawake wajanja wanatumia nafasi hii ya "tunanyanyaswa" kula na kushiba.

Wakiwaacha wale wanaonyanyaswa wakiendelea kunyasika...!

In other words,

mbona wanawake hawawaonei huruma wanawake wenzao...! Awe tu mwenyekiti wa hicho chama chao azile basii..!

Kazi kwelikweli!!
 
Ome

Member
Joined
Jan 2, 2008
Messages
79
Points
95

Ome

Member
Joined Jan 2, 2008
79 95
Mi bado sielewi hii siku ya wanawake duniani wanapresent kitu gani ikiwa wanawake wenyewe ndio wa kwanza kwa kuwanyanyasa wafanyakazi wao wa ndani, au wao kwa kuwa hawana pa kukimbilia ukizingatia wanachukua watoto wadogo ili wawanyanyase vizuri sio bomba inatakiwa kwanza wanawake wenyewe waache kunyanyasana.
 
Masatu

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2007
Messages
3,284
Points
1,195

Masatu

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2007
3,284 1,195
Mi bado sielewi hii siku ya wanawake duniani wanapresent kitu gani ikiwa wanawake wenyewe ndio wa kwanza kwa kuwanyanyasa wafanyakazi wao wa ndani, au wao kwa kuwa hawana pa kukimbilia ukizingatia wanachukua watoto wadogo ili wawanyanyase vizuri sio bomba inatakiwa kwanza wanawake wenyewe waache kunyanyasana.

U have a BIG point there...
 
Forum statistics

Threads 1,363,916
Members 520,595
Posts 33,301,049
Top