Siku ya Karume...

Kibunango

JF-Expert Member
Aug 29, 2006
7,984
1,589
Tarehe 7/04 kila mwaka ni siku ya mapumziko kwa kusherehekea Siku ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume...

Wale wa ze laga huko bongo natumai wana long weekend...:D Anyway katika kusheherekea siku hiyo sio mbaya kujikumbusha mafaniko ya Rais huyo katika siasa za Zenj na Tanzania kwa ujumla...
  • Rais wa kwanza kutamka hadharani kuwa unaweza kwenda shule na usiambulie kitu.... Hii ni kutokana na kauli yake ya "Tumesoma hatukufahamu, tumejifunza tumeeleewa" Kauli hii ilitumika sana wakati wa Ujenzi wa Michenzani.
  • Aliweza kufanikisha ndoto za wengi..hasa weusi kwa kuwapa maisha bora mara baada ya Mapinduzi- ujenzi wa nyumba za Wajerumani, na Michenzani aidha aina za ujenzi huo karibu katika kila kitongoji katika visiwa hivyo.
  • Katika kujali ukuaji wa watoto katika uchangamfu na umakini na ubora unaokubalika, alitenga maeneo mengi ya wazi katika vitongoji kwa ajili ya michezo na burudani.. Zaidi ni kujenga sehemu maalum ya kujipumzisha kwa familia.."Kariakoo"
  • Kuanzisha elimu kwa njia ya televison... rekodi kubwa katika Afrika
  • Kuondoa tabaka za uarabu na uweusi kwa kuunganisha jamii hizo mbili kwa njia ya kifamilia
Nawatakia mapumziko mema watanzania wote, pengine itakuwa vema kuitumia siku hiyo kufanya usafi wa mazingira ya mtaani kwako na nyumbani kwako ili kuzuia uzaliaji wa mbu na hasa katika kipindi hiki cha masika ....
 

a.9784

Senior Member
Feb 19, 2008
145
4
Hizi sikukuu kwangu naona hazijakaa vizuri.Kwa hiyo hapo baadae tutakua na Mwinyi day,Mkapa day,Kikwete day,Komando day,Jumbe day,Karume 2 day,what this is?Is this materialism or idealism.Au tunaleta ushabiki tu.Nyerere day + Karume day,wachumi nisaidieni ni hasara kiasi gani nchi inapoteza.

At least tuwatengee one hour nasema hivyo kwa sababu hawa watu hakuna kiongozi yeoyete kwa sasa anae waenzi ila ni unafiki tu,waliyotufanyia wazee wetu ni makubwa sana kiasi kwamba wangeyafanyia kazi hawa viongozi wetu wasasa tungekua mbali sana.Lakini viongozi wetu wamepuuza misingi iliyowekwa na wazee wetu waasisi na wamekuja na yakwao.
 

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,547
776
Huyu ndie rais pekee Tanzania ambaye hakuwa na elimu kubwa lakini alifanya makubwa kuliko wote waliomfuata
 

Engineer Mohamed

JF-Expert Member
Jul 27, 2007
453
6
mtu wa pwani na kibunango

ahhhhhh bana nitakuwepo hom kwangu nikifanya usafi huku nasikiliza mambo haya
[media]http://www.youtube.com/watch?v=X7kzloYAwUQ[/media]
 

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
114
haya Mtu wa Pwani mimi najiandaa na xiuxi moja ya kufa mtu huku nikiwa na doufu zangu zilizokaangwa na chaofan niurou so nitakuwa navuta harufu za pwanipwani.
 

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,504
1,739
Ningefurahi Kama Tbc Wangeanza Kurusha Hotuba Zake Kila Siku......wosia Wa Karume...!
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,902
10,408
Kabisa wajua wa tz bara wengi hatujui hata...historia yake na mengineyo yaliyojiri wakati wa mapinduzi...matukufu ya zbar.nitafurahi sana kama tutajapatiwa historia ya zbar na mchakato mzima wa mapinduzi kwa kikazi hiki cha bongo flava na fm radio..la sivyo historia itaja potea
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom