Siku Ya Jumamosi Mayahudi Walifanya Nini Hata Wakageuzwa Manyani?

Mahmood

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
7,909
2,477
Siku Ya Jumamosi Mayahudi Walifanya Nini Hata Wakageuzwa Manyani?


SWALI:


Ass-salamu allaiqum warahmatulwah wabarakatu, ndugu yangu ninataka msada wako au wenu juu ya maelezo yangu haya. Nimesoma ktk tafsiri ya Quraan juzuu ya 1 Surat al-baqarah ayaa ya 65, M/Mungu alisema kuwaambia Mayahudi watu wa Nabii Mussa (A S), Walishindwa kuihishimu siku wa Jumaamosi basi Allah (S W) akawambia kuweni manyani wadhalilifu. ndugu yangu muislam nnataka unisaidie hapa ktk hii siku ya J'mosi binaadamu hawa walifanya nini?
 
Ndugu zangu Nimepata jibu (Kama kuna mtu anazaidi tunaomba atuwekee hapa)


Sheikh kanijibu hivi,


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'ala) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Mtume. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea au kivivu. Pia hiyo ni ibada, na ibada inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza au kupunguza. Hali kadhalika Maswahaba walikuwa wakiandikiana barua na hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.

Katika kusoma tafsiri ya Qur-aan na kuweza kupata msaada wa kuielewa vizuri hivo tafsiri ni kujaribu kungalia maelezo ya Mfasiri ambayo huwa ima pamewekwa Aayah nyengine inayoitafsiri hiyo Aayah; kwani Qur-aan inafasiri Qur-aan na ndio kitu cha mwanzo katika kutafsiri Qur-aan ni Qur-aan yenyewe; au pamewekwa Hadiyth za Mtume ya (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yenye kuitafsiri hiyo Aayah au maelezo ya Swahaba yenye ufafanuzi wa Aayah; au pamewekwa ishara ya kukueleza wapi kumetajwa kinachozungumzwa na Aayah hii kwa ufafanuzi au kwa urefu; kama ilivyokuwa katika Aayah hii.

"Na hakika mlikwishayajua ya wale miongoni mwenu walioivunja Sabato, (siku ya mapumziko, Jumamosi) na Tukawaambia: Kuweni manyani wadhalilifu. Kwa hivyo Tukayafanya hayo kuwa onyo kwa wale waliokuwa katika zama zao na waliokuja baada yao, na mawaidha kwa wacha Mungu." Al-Baqarah: 65-66.

Umeuliza, ‘hii siku ya J'mosi binaadamu hawa walifanya nini?' Kwa faida ya wengi tutakujibu. Ni kuwa siku ya Jumamosiilikuwa ni siku ya ibaada tu kwa Mayahudi wa zama hizo na katika walichotakiwa ni kuiheshimu siku hiyo kwa kutojishughulisha na aina yoyote ile ya kazi, na miongoni mwao walikuwa wavuvi wa kijiji kimoja kilicho kuwa karibu na bahari, hivyo Allaah kwa hekima na uadilifu wake na kuelewa fika kuwa uvuvi ndio kipato chao na ndio kitu wanachopenda Alitaka kuwaangalia utiifu wao Kwake kwa kuwakataza kuvua katika siku hiyo ili Awapambanuwe walioamini na wale wenye kujidai kuwa wameamini; na hivyo ndivyo ilivyotokea; kwani miongoni mwao walikuwemo walioamini na kwa kuelewa yanayowapata kila mwenye kuthubutu kuhalalisha Alichokiharamisha Allaah.
Waliwakataza wenzao (ni watu wa kijiji kimoja lakini kila mmoja na imani yake, wengine wanakwenda darsa na wengine wanaona hakuna haja, kwani wanaelewa kila kitu katika dini) kundi lililokuwa linataka kuvunja amri ya Allaah kwa kwenda kuvua (na hivi ndivyo wanavyotakiwa Waislamu kuamrishana mema na kukatazana mabaya sio kusema, kwani hawaelewi?!); kundi jingine likaona hakuna haja ya kuwakataza kwani wanaelewa uharamu na yatakayokuja kwa kuvunja amri ya Allaah; hivyo wale wakaidi baada ya kukumbusha na kuwaidhiwa hawakufaidika na mawaidha wala hawakuona umuhimu wa kukumbushana, matamanio yao yakawa ndio mungu wao hivyo wakamua kuivunja amri ya Allaah ya kutovua samaki siku ya Jumaamosi, kwani ni siku pekee wanayoweza kupata kipato kikubwa na bila ya kupata taabu kwani siku hii iliyokatazwa kuvua samaki walikuwa wakiwajia vururu juu ya maji, wakati siku isiyo kuwa Jumaamosi samaki hawaji kama hivi (hii ni katika mitihani wa Allaah), kama ilivyoweka wazi Qur-aan kwa kusimulia:

"Na waulize khabari za mji uliokuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko yao, na siku zisiokuwa za kupumzika hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu. Na kikundi kati yao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu Atawateketeza au Atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola Mlezi wenu, na huenda nao wakamcha Mungu... Basi walipoyasahau waliyokumbushwa, tuliwaokoa waliokuwa wakikataza maovu, na tukawatesa waliodhulumu kwa adhabu mbaya kwa vile walivyokuwa wakifanya upotovu. Walipojifakharisha katika waliyokanywa Tuliwaambia: Kuweni manyani wa kudharauliwa." Al-A'araaf: 163-166

La muhimu hapa ni kuelewa kuwa kilichowafika waliovunja amri za Allaah katika zama zile kinaweza kuwafika wanaozivunja na kuzikejeli wa zama hizi kama hakutokuwa na wenye kuamrisha mema na kukataza mabaya katika jamii; kwani kilichowafika ni kama funzo na onyo kwa wengine (tukiwemo sisi), kilichowafika ni zingatio kwa watu wa zama ile na watakaokuja baada yao.

Na Allaah Anajua zaidi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom