Siku ya 7 baada ya CCM kurusha "kete"... Wamefanikiwa asilimia ngapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku ya 7 baada ya CCM kurusha "kete"... Wamefanikiwa asilimia ngapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Mar 19, 2013.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Mar 19, 2013
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,191
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  Ni wazi kwamba dhumuni kuu la CCM kutengeneza skendo hii ya "Lwakatare" ni kuichonganisha CHADEMA na waandishi na vyombo vya habari. Kwa miaka ya karibuni tishio kubwa kwa CCM limekuwa ni vyombo huru vya habari kuripoti habari za CHADEMA 'kama zilivyo', hivyo kuwa chachu kubwa ya kukieneza chama hicho nchini.
  CCM walidhani kwa kufanya haya watawafanya waandishi wa habari waichukie na kuisusia CHADEMA. Mkakati wao ulianzia kwa Mwangosi (rejea fast response ya polisi makao makuu kabla hawajaumbuliwa na picha na mashuhuda), lakini kwa bahati mbaya ulikwama, tena uka back fire kwa kiasi kikubwa. Hawakukata tamaa, wakaja na la Kibanda, likipewa nguvu na ushahidi wa video ya Lwakatare. Je kwa hili wamefanikiwa au watafanikiwa? Jibu la wazi kabisa ni HAPANA, waandishi wataendelea kuwa huru kwa CHADEMA, na upo uwezekano wakaongeza chuki kwa CCM.

  Kuna mambo manne ambayo CCM ama hawakuyaona kutokana na ufinyu wao wa mawazo, au waliamua kuyapuuzia, lakini ndiyo yanayosabisha kushindwa kwa mpango wao huu:

  1. CHADEMA ina mtaji mkubwa wa kisiasa. Ukitaka kung'oa mti, ung'oe ukiwa mchanga, ukitaka kumkunja samaki, mkunje angali mbichi. CHADEMA kwa sasa inao mtaji mkubwa sana kisiasa, kiasi kwamba umaarufu wake hauwezi kutikiswa kwa mbinu dhaifu kama hii

  2. CHADEMA kuwa na buffer zone nene. Siku zote kukubalika kwa chama kisiasa kuna-percolate kutoka kada ya juu ya watu (in terms of uelewa), kwenda kada za chini. Kwa sasa CHADEMA inakubalika pengine mara 5 au zaidi katika kada ya juu na ya kati kuliko CCM. Hata hivyo wapiga kura wengi wapo kada za chini. Kukubalika kwa chama chochote kunategemea sana Layer hii ya juu na ya kati ambayo inaact kama buffer zone, ikiregulate yote yanayoelezwa na chama fulani, kabla hayajafika chini. Unaweza kuona hapa ndipo CCM ilipopotea, kwani kete yao hii imekuwa neutralized kwa kiasi kikubwa sana na watu waliopo kwenye layer ya wasomi na vijana kabla haijafika kwa majority voters. CHADEMA kwa sasa inaungwa mkono na wazalishaji, wasindikaji na walaji wengi zaidi wa habari kuliko CCM

  3. Matumizi ya jeshi la polisi. Kama ilivyo vyama vingi vikuu vya upinzani kuwa chama na wafuasi wake ni maadui wa polisi. Hali hiyo kwa hapa Tanzania ipo juu zaidi. Sasa CCM kuamua kuitumia polisi kuhalalisha uhalifu wa CHADEMA, wanajua kabisa hata ingekuwa kweli, CHADEMA wangeenda kwa watu na kusema 'huu ni mpango wa polisi kutuhujumu', kwa sentensi moja tu wangeaminika kwa asilimia 100. Kwa hiyo hakutakuwa na significant impact kwa matokeo yeyote ya uchunguzi au kesi hii (hata wakithibitisha kwa 101% kwa sababu yatakuwa influenced completely na imani ya watu kuwa polisi huwa inahujumu CDM

  4. Kudhoofika kwa CCM. Asilimia kubwa ya supporters wa CHADEMA kwa sasa ni watu waliowahi kuwa supporters wa CCM, lakini kutokana na kudhoofika kwake, wakaamua au kujikuta wakiunga mkono CHADEMA. Ubovu wa CCM ni rahisi kuwa published kutokana na CCM kushikilia serikali, lakini hawana uwezo wa kuiwajibisha serikali hiyo. Kwa hiyo juhudi zozote CCM inazoweza kufanya kuihusisha CHADEMA na madhaifu machache, ambayo tena kwa kiasi kikubwa hayawagusi wananchi moja kwa moja, itakuwa ni kazi bure dhidi ya uwanja mpaana walio nao wapinzani kuihusisha CCM na matatizo ya Watanzania, kwa kisingizio cha serikali kutowajibika kikamilifu...


  CCM wana njia moja tu na rahisi kuiwezesha ikubalike na wananchi na iendelee kutawala miaka na miaka.... hata hivyo sitaitaja kwa sababu sio maudhui ya thread hii...
   
 2. monakule

  monakule Member

  #2
  Mar 19, 2013
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 83
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  wanaccm karibu wote wlimaliza darasa la nane
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2013
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,865
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  viva m4c! CCM ni chama kilichokufa zamani sana! Ili ku survive wanatumia vyombo vya dola kuhang on! 2015 ni fainali uzeeni ya ccm. Tena naomba kutoa kauli mbiu kwa chama changu kitukufu cha CHADEMA. Katika kampeni zetu hakikisha unataja ccm fainali uzeeni 2015.
   
 4. L

  Lwesye JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2013
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 5,296
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sijui kama watakuelewa lakini analysis yako ni sahihi kabisa fanya kautafiti ka kwako binafsi,shuleni,vyuoni,sokoni,stand uliza je jamani hivi haya mambo ya lwakatare vipi hawa chadema nao wameharibikiwa ,haki ya mungu mvua ya matusi,mashambulizi,kebehi,dharau,vijembe utakavyovipata utachoka
  Walinzi wa chadema ni wananchi wa ngazi zote CCM itafakari njia zingine za propaganda
   
 5. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2013
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Propaganda za masisiem ni za kishamba sana,ndio maana wale wanaosema masisiem yana mchoko wa akili na mwili kama mzee wa gombe wapo sahihi kabisa!!!rest in hell masisiem....
   
 6. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2013
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Masikini chama chetu kinajiua na kujitafuna chenyewe,jamani hawa viongozi tuliowapa dhamana ya kutuongoza mbona hawaendi kisayansi?hivi hawana mbinu nyingine au ndiyo mufilisi kichwani,hizi mbona za kizamani yaani zilitumiwa na Hitler enzi hizooo,sasa wanaujenga upinz......... ,hawajiulizi wakishinda kesi si itakuwa mtaji wao wa kisiasa?angalia kule Iringa sasa hawakijui chama chngu kule mwanza,shinyanga mbeya Arusha ndiyo kabisaa,kwa staili hii maisha ni magumu hiyo15,jamaniiii iiii i badilisheni mbinu hizi hazifai siku hizi kuna utandawazi!!!mnanisikitisha kwelikweli jamani baaaasi!!!1.
   
 7. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2013
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mchanganuo mzuri na makini lakini kwa CCM kuwaambia maneno kama hayo ni sawa na kuchukua chakula cha mtoto ukampa mbwa.
   
 8. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2013
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,116
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  CCM wanategemea propaganda kama turufu yao kisiasa. Wanasahau kuwa cdm imewekeza katika hali ya wananchi badala ya porojo. Lakini sishangai kwani hakuna kiongozi yoyote wa CCM anayeweza kusimama na Dr Slaa kwa hoja na akashinda. Au mmesahau Rais alivyokimbia mdahalo mwaka 2010? Huyu ndiye mwenyekiti wa hicho chama unategema nini kama sio mipango iliyochoka kama hii? Fainali uzeeni mwaka 2015
   
 9. master peace

  master peace JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 1,451
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  2015 mbali sana ni vyema hawa magambaz tukawaondoa hata leo, tukisubiri hadi 2015 nchi hii itakuwa imebakiwa na mashimo tu.
   
 10. m

  malaka JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2013
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Aisee mimi ndio najishangaaa. Yaani mapenzi na CDM ndio yamezidi ghafla sijui kwa nini aisee.
   
 11. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2013
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wengi wetu tumeelemea upande wa kushikiliwa kwa Wilfred kuwa ni mkakati uliyofanywa na CCM ,tujalie iwe hivyo lakini cha muhimu hapa tujiulize pia hivi hakuna uwezekano wa Rwakatare ameshawishiwa na amekubali kuwatumikia tunaowashitumu kuwa wanamkakati wa kukihujumu chadema ?Wilfred inawezekana (I hope I m wrong )amefanya hayo kwa kujuwa na kwa ajili ya maslahi yake binafsi?
   
 12. F

  FUSO JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 12,684
  Likes Received: 3,049
  Trophy Points: 280
  mfano mzuri wa CCM kujiokoa ilikuwa ni kutumia Bunge ambalo majority ni wabunge wa CCM kuisimamia na kuiwajibisha serikali, badala ya kutetea haki za wananchi wao wanajiua kwa kuitetea serikali waliyoiunda. Hii ni pamoja na kuzifuta hoja za wapinzani kwa mfano ile hoja ya Elimu ya Mbantia na ile ya Maji ya Mnyika imewashusha vibaya mno.

  Kama CCM wangekubali hizi hoja zijadiliwe na serikali kupitia wizara iwajibike basi CCM ingepata pa kuanzia towards 2015, lakini jinsi mambo yalivyo wana hali mbaya sana kisiasa kuanzia ndani ya chama chenyewe hadi nje.

   
 13. Nokla

  Nokla JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2013
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 2,121
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  walishaambiwa hapa kama ile video imetendenezwa basi wataalam wa IT toka CHADEMA watengene nyingine ya mswahili ili tuione na tuamini maneno yao ila wao wamebakiwa kutukana matusi tuu!
   
 14. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2013
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,470
  Likes Received: 3,364
  Trophy Points: 280
  Hili nalo tushashinda make ndo kwanza hata wateja wa CCM wanaitetea CDM mtaani ..league inaisha mapema kabla ya 2015
   
 15. Nokla

  Nokla JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2013
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 2,121
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CDM tengenezi VIDEO ya kuwachonganisha CCM na wananchi ili wasiichague tena mwaka 2015, ndio dawa yao!
   
 16. c

  cha arusha Member

  #16
  Mar 19, 2013
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka uko vizuri, ukweli ni kwamba ccm wakishinda kesi au wakishindwa kesi yote inawapunguzia umaarufu. Cdm watarudi kwa wananchi na kuomboleza wanaonewa. Ccm bado wanatumia mbinu za kizamani mno!
   
 17. Chigwiyemisi

  Chigwiyemisi JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2013
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 531
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  CCM kuanzia viongozi wake hadi wabunge wote wamepigwa upofu, unategemea nini. Wabunge wake achilia mbali uwezo mdogo walionao, hata adabu hawana sasa unategemea nini hapo. Wakiwa bungeni kazi ni moja tu, kujikomba kwa serikali na kujipendekeza kwa wakubwa wao, basi. Wakati wabunge wa upinzani wanasoma na kuchambua kila hoja inayokuwa mbele yao, wabunge wa CCM wanapwaya kwenye kila hoja. Unafikiri kwa nini imefikia hatua wanataka bunge lisionyeshwe live!!? Chezea CDM weye..


   
 18. m

  mwakibete JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2013
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,626
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280


  Old pirates, yes, they rob I;
  Sold I to the merchant ships,
  Minutes after they took I
  From the bottomless pit.
  But my hand was made strong
  By the 'and of the Almighty.
  We forward in this generation
  Triumphantly.
  Won't you help to sing
  This songs of freedom
  'Cause all I ever have:
  Redemption songs;
  Redemption songs.

  Emancipate yourselves from mental
  slavery;
  None but ourselves can free our minds.
  Have no fear for atomic energy,
  'Cause none of them can stop the time.
  How long shall they kill our prophets,
  While we stand aside and look? Ooh!
  Some say it's just a part of it:
  We've got to fullfil the book.
  Won't you help to sing
  This songs of freedom-
  'Cause all I ever have:
  Redemption songs;
  Redemption songs;
  Redemption songs.

  Emancipate yourselves from mental
  slavery;
  None but ourselves can free our mind.
  Wo! Have no fear for atomic energy,
  'Cause none of them-a can-a stop-a the
  time.
  How long shall they kill our prophets,
  While we stand aside and look?
  Yes, some say it's just a part of it:
  We've got to fullfil the book.
  Won't you have to sing
  This songs of freedom? -
  'Cause all I ever had:
  Redemption songs -
  All I ever had:
  Redemption songs:
  These songs of freedom,
  Songs of freedom.
   
 19. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #19
  Mar 19, 2013
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,191
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  Unajua wanaoshabikia hii filamu hawapandi daladala labda...

  Ukipanda daladala siku hizi utajua kibao kishageuka zamaaani!
   
 20. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #20
  Mar 19, 2013
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,191
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  Kulia na kucheka zote ni kelele mkuu...
   
Loading...