Siku ya 5 leo tangu Mugabe 'apigwe' chini Zimbabwe, CCM chama rafiki wa ZANU-PF wako kimya!

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,384
Hivi hawa CCM siku hizi wakoje, Mzee Mugabe rafiki mkubwa wa CCM 'amedhibitiwa' huko Zimbabwe lakini maCCM wako kimya tu, ina maana hawajasikitishwa na kilichofanyika Zimbabwe?

Wamefurahishwa na kitendo cha jeshi kumwondoa madarakani rafiki yao ambaye majuzi hapa hata Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu walitoa taarifa ndefu kuonesha furaha waliyokuwa nayo baada ya Askofu wa Zanzibar kusifia kuwa utendaji na tabia za Mwenyekiti wa CCM ni sawa na za Rais wa ZANU-PF, Dr.Mugabe? Imekuwaje leo wakati wa dhiki CCM wamemwacha Dr.Mugabe akihuzunika peke yake, CCM mbona wamekuwa wasaliti hivi siku hizi?​

[HASHTAG]#Polepole[/HASHTAG] please, toa basi vile vitamko vyako, tafadhali sana!
 
Kiongozi; hakuna wasaa ambao Shetani anapata raha kama unapoaibika hadharani. Ukombozi pekee unapatikana kwa Bw. Yesu; nenda ukapate pumziko la kweli.
 
Mzee Mugabe amekomaa na wajeda mpaka wanamchonganisha na wananchi wake.hajapigwa chini.
 
Mkuu, hata mimi nilikuwa nawaza kama wewe! tatizo ninaloliona kwa nchi ya Tanzania ni kupoteza ushawishi wake kwenye diplomasia ya Kimataifa. kadri siku zinavyokwenda, nchi inakuwa zezeta na mfu. pia kuna factors nyingine kuwa na viongozi wasiojielewa na wanao-reason kwa urefu wa ncha ya pua zao. hii imezorotesha urafiki na ushirikiano ulioasisiwa na watangulizi kama Mwl. nyerere nk. kuna speech moja Mugabe aliongea kwa uchungu na hisia kubwa akishangaa nini kimeipata Tanzania...akimaanisha aina ya viongozi tulionao. kama hiyo haitoshi, kuna kipindi balozi wa Zimbabwe alitishia kuondoka akiituhumu serikali( viongozi kumsema vibaya Mzee Roberto Mugabe). kuna madhila mengi sana kwenye uhusiano wa tz na nchi zilizowahi kuwa rafiki zetu hasa ukanda huu wa SADC......
 
Hivi hawa CCM siku hizi wakoje, Mzee Mugabe rafiki mkubwa wa CCM 'amedhibitiwa' huko Zimbabwe lakini maCCM wako kimya tu, ina maana hawajasikitishwa na kilichofanyika Zimbabwe?

Wamefurahishwa na kitendo cha jeshi kumwondoa madarakani rafiki yao ambaye majuzi hapa hata Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu walitoa taarifa ndefu kuonesha furaha waliyokuwa nayo baada ya Askofu wa Zanzibar kusifia kuwa utendaji na tabia za Mwenyekiti wa CCM ni sawa na za Rais wa ZANU-PF, Dr.Mugabe? Imekuwaje leo wakati wa dhiki CCM wamemwacha Dr.Mugabe akihuzunika peke yake, CCM mbona wamekuwa wasaliti hivi siku hizi?​

[HASHTAG]#Polepole[/HASHTAG] please, toa basi vile vitamko vyako, tafadhali sana!
Mbona hujui usemalo? ZANU PF ndiyo imemkataa Mugabe. Na mbona husemi ya Kenya, kutii sheria bila shurti. Raila ngangari dhidi ya Jubilee ya Lowassa!
 
Zamu yao inakuja Fisiemu wajiandae na SMG

Umma unaungana kuitafuta nguzo ya uswezi

Tunaongoza mapambano ya wafanyakazi na wakulima hadi ushindi upatikane

Wakati unanena si wakati wa Fisiemu tena

Tunakuja tunakuja fisiemu tunakuja fisiemu tunakuja ss ni vivuli vya mliyowateketeza bila hatia

Tunakuja Kwa nguvu za miungu mungu na mizimu yote tunakuja vijana kuwang'oa fisiemu
 
Nafikiri nk mambo ya kidiplomasia tu. CCM lazima iwe neutral kwenye hili otherwise itakua changamoto.

Ushawishi wa tz sadc binafsi naona umekaa kivyama zaidi
Mf. Mozambique, Zimbabwe, SA na Namibia
Hizi nchi siku vyama vyao vikitoka madarakani itakua ndio mwisho wa ushawishi maana historia inaonesha mahusiano yamekaa kivyama zaidi
 
CCM Rafiki yake ni ZANU PF sio Mugabe

Hata akiondoka Mugabe kitasalia Madarakani ni ZANU PF sasa Tatizo liko wapi?
 
Ukiangalia Tanzania kwa jicho la tatu hadhi yake imeshuka na imekiuka misingi ya utawala bora na demokrasia.Ndio maana hata marafiki zetu ni wale wanaotiliwa shaka au wasiokubalika aidha kimataifa au ndani ya nchi zao kuna misigano mfano Uturuki,Morroco,Uganda nk!Ndio maana hata la ZANU PF japo inatuuma kipenzi kuonyeshwa mlango wa kutokea na kwasababu ndiye role model wetu tunabaki kugumia tu!
 
Zanu-PF kitasonga mbele,mzee Mugabe atabaki kuwa baba wa taifa la Zimbabwe na mwanamapinduzi,mpigania uhuru wa waafrika.
 
Hivi hawa CCM siku hizi wakoje, Mzee Mugabe rafiki mkubwa wa CCM 'amedhibitiwa' huko Zimbabwe lakini maCCM wako kimya tu, ina maana hawajasikitishwa na kilichofanyika Zimbabwe?

Wamefurahishwa na kitendo cha jeshi kumwondoa madarakani rafiki yao ambaye majuzi hapa hata Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu walitoa taarifa ndefu kuonesha furaha waliyokuwa nayo baada ya Askofu wa Zanzibar kusifia kuwa utendaji na tabia za Mwenyekiti wa CCM ni sawa na za Rais wa ZANU-PF, Dr.Mugabe? Imekuwaje leo wakati wa dhiki CCM wamemwacha Dr.Mugabe akihuzunika peke yake, CCM mbona wamekuwa wasaliti hivi siku hizi?​

[HASHTAG]#Polepole[/HASHTAG] please, toa basi vile vitamko vyako, tafadhali sana!
Kuwakubalia ujinga ule ni kumtumia e-mail general Mabeyo 'usiwe mjinga'

Hata kama simuungi mkono Magufuli lakini nakubali kuwa ndiye Rais wangu, Sitakubaliana na ujinga wa mtu yeyote kutaka au kumtoa madarakani Rais wangu (taasisi ya Urais iheshimiwe)
 
Zanu-PF kitasonga mbele,mzee Mugabe atabaki kuwa baba wa taifa la Zimbabwe na mwanamapinduzi,mpigania uhuru wa waafrika.
Keshachokwa nchini kwao. Hata majeshi ambayo ndio ilikuwa nguvu yake yamemchoka. Nchi anaharibu yeye na mkewe halafu anasingizia wazungu. Wanaompa ukweli, kama ilivyo 'huku', wanaitwa vibaraka, wasaliti. Maigizo, mazingaombwe yamechokwa, uchumi umekufa, hakuna maendeleo.
 
Back
Top Bottom