Siku Watanzania watakapoamua kujibu mapigo kwa Jeshi la Polisi

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Kuna kila dalili kwamba Watanzania wameanza kuchoshwa na hii tabia ya Jeshi la Polisi la kupiga watu mabomu na risasi za moto hata mahali ambapo hakuna ulazima na hivyo kupelekea vifo kwa Watanzania wasio na hatia. Kuna msururu mrefu sana wa Watanzania waliouawa na Polisi wakiwa kwenye maandamano,mikutano ya hadhara,chini ya ulinzi au mahabusu!

Matukio ya hivi karibuni ambayo yemehusishwa na mauaji ya kisiasa yamezidi kuchafua rekodi za Jeshi la Polisi na hasa baada ya kumwua mwandishi wa habari kule Iringa. Watanzania wamechukizwa sana na tabia hii na kuna tetesi kwamba karibu wataanza kujibu mapigo kutokana na unyama huu.

Ikumbukwe kwamba hawa wanaouawa au kujeruhiwa kwenye maandamano au mikutano ya hadhara mara nyingi imetokea kuwa si wanachama wala wafuasi wa vyama au taasisi husika. Kinachoonekana hapa ni mauaji yanayokuwa yamepangwa makusudi ili kuwazuia,kuwatisha au kuwakatisha watu tamaa kufikia malengo ya kile wanachokikusudia kwenye maandamano husika. Mara zote ambazo mauaji yametokea serikali imekuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua madhubuti za kisheria ili kuzuia hali hii isiendelee. Polis wameua na mwisho wa siku wameishia kupandishwa vyeo au kuhamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine!

Watanzania wamesha anza kuchoka na wanasema wataanza kuchukua hatua wenyewe kwa kuwashughulikia Polisi wanaohusika na mauaji hayo. Kwa vile Polisi wengi wanaishi uraiani pamoja na familia hizi zinazoasiriwa na mauaji haya zitajibu mapigo huko huko uraiani. Hakuna Mtanzania atakubali kuona Polisi ambaye ni jirani yake akiishi kwa amani na huku akituhumiwa kamwua ndugu yake kwenye maandamano ya CHADEMA bila ya sababu za msingi. Lazima atajibu mapigo tu kama dola itaendelea kumlinda! Polisi hawawezi kujifanya miungu watu wa kutoa roho za watu halafu wao wakaendelea kufurahia maisha kana kwamba wako juu ya sheria. Hili halikubaliki na halitakubalika kwa Tanzania ya sasa na itakayokuja.

Hizo ndiyo salamu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Nchimbi,IGP Mwema na Makamanda wake wote wa Makao makuu na Mikoani.
 
tii sheria bila shuruti. full stp

Wewe ***** nini!

Ni sheria ipi inayosema mtu akiandamana apigwe bomu la machozi kwenye tumbo??Hivi wewe kama Daudi Mwangosi angelikuwa ni kaka yako,mdogo wako,shemejiyo au ana uhusiano wowote wa karibu na wewe ungelikuwa unaongea ujinga huu wa kutii sheria bila shurti???Hiro riafande ririlomuua Mwangosi mbona liko rokapu sasa kama lilikuwa rinatimiza wajibu kwa mujibu wa sheria?

Acha ujinga pse. Yawezekana nawe ni mmoja wa wauaji wa Mwangosi. We'll get you soonest! Kazi ndiyo imeanza. Tunataka kusikia RPC Kamuhanda na IGP Mwema wakifikishwa kwa pilato haraka kadri itakavyowezekana. Tumeshachoka!
 
Ipo siku watapata wanacho kitafuta

CCM na serikali yake wanatumia Polisi na vyombo vingine vya usalma kuendelea kujikita kwenye utawala. CCM wanajidanganya kwamba Watanzania wa miaka ya 1960s ya enzi za mwalimu ndiyo hawahawa wa leo. Wanajidanganya!

Something is very burning deep in the hearts of all Tanzanians and very soon they gonna retaliate! Halafu tuone kama Polisi wataweza kuzuia moto wa watu zaidi ya 40 milioni! Wasitake kutumia upole na uungwana wa Watanzania luwafanya kuwa mazezeta wasiojua lolote.

Tatizo hapa ni ulevi wa madaraka kwa hawa Magamba. Kwa vile wako madarakani kwa zaidi ya 50 years basi they do think wana hati miliki ya kutawala Tanzania milele hata kama ni kwa kumwaga damu! Pumba zao!
 
Polis wetu wanahitaji maombi.., wameacha kazi yao na sasa wamechagua kuwa vikaragosi wa wanasiasa
 
hawa wanatakiwa tuwe tunajitayarisha ikifika mahala tukiwaona hawaachi tabia hii tunaanda mawe,maji ya pilipili,chupa,***** na kila dhana ya jadi tuwaoneshe kuwa hatutaki na tumechoka kuonewa.wakitukorofisha nao tunawakorofisha.
 
Polis wetu wanahitaji maombi.., wameacha kazi yao na sasa wamechagua kuwa vikaragosi wa wanasiasa

hawa hawaitaji maombi wanahitaji nao kufeel maumivu makubwa kama wanayowapa wananchi ili wakipewa amri za kipuuzi wasiwe wanakubali.
 
Wewe ***** nini!

Ni sheria ipi inayosema mtu akiandamana apigwe bomu la machozi kwenye tumbo??Hivi wewe kama Daudi Mwangosi angelikuwa ni kaka yako,mdogo wako,shemejiyo au ana uhusiano wowote wa karibu na wewe ungelikuwa unaongea ujinga huu wa kutii sheria bila shurti???Hiro riafande ririlomuua Mwangosi mbona liko rokapu sasa kama lilikuwa rinatimiza wajibu kwa mujibu wa sheria?

Acha ujinga pse. Yawezekana nawe ni mmoja wa wauaji wa Mwangosi. We'll get you soonest! Kazi ndiyo imeanza. Tunataka kusikia RPC Kamuhanda na IGP Mwema wakifikishwa kwa pilato haraka kadri itakavyowezekana. Tumeshachoka!

Siyo kila mahali panataka usataarabu umjibu mpumbavu sambamba na upumbavu wake SEMA HIVI: Marehemu Mwangosi angekuwa shemaji yake mpenzi wake dada yake angesema atii sheria bila shuruti? Hata kwa amri ya polisi waliotakiwa kutii sheria ni CHADEMA siyo Mwangosi kwakuwa yeye hakuwa mwanachadema wala hakuenda pale kufanya kazi za chadema bali alikwenda pale kuujulisha umma wa TZA nini kinafanyika katika eneo hilo la TZ
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom