Siku watanzania wakijua umuhimu wa Katiba Mpya nini kitatokea?

NEW COVID

Member
Apr 13, 2021
38
35
Wakuuu najaribu kuwaza kwa mapana, Tanzania tunatumia KATIBA ya mwaka 1977 na huu ni mwaka 2021.

Malalamiko ni mengi mno kutokana na KATIBA ya OVYO.

Je, Watanzania siku wakifahamu hili suala ni muhimu nini kitatokea na ni lini watafahamu?
 
Unadhani watanzania hawajui umuhimu wa katiba mpya? Je katiba mpya ni muarobaini wa matatizo yetu wakati nyani ni wale wale na msitu ule ule wakicheza unyani ule ule? Afrika Kusini na Kenya wana katiba mpya na nzuri lakini je maisha yao yamebadilika? Mie nadhani tuwe na mfumo wa haki na huru hata kama ni bila katiba. Katiba sawa na bendera hailiwi.
 
Sasa huo mfumo wa haki si ndio unatokea huko huko kwenye katiba. Katiba ndo suluhisho la haya madudu yote tunayoyasikia.
 
Unadhani watanzania hawajui umuhimu wa katiba mpya? Je katiba mpya ni muarobaini wa matatizo yetu wakati nyani ni wale wale na msitu ule ule wakicheza unyani ule ule? Afrika Kusini na Kenya wana katiba mpya na nzuri lakini je maisha yao yamebadilika? Mie nadhani tuwe na mfumo wa haki na huru hata kama ni bila katiba. Katiba sawa na bendera hailiwi.
Africa Kusini imekuwa huru mwaka 1994, Tanzania ni Taifa huru tangu 1961. Katika kipindi kifupi cha kuwa huru SA imekuwa na demokrasia imara inayoheshimu haki za raia na kutoa uhuru mpana sana kwa raia wake.
 
Katiba ikisukwa vizuri Kwa asilimia kadhaaa ni mwarobaini Kwa mfano ,, Nafasi hizi anateuwa mtu mmoja 1.makamo WA rais 2.waziri mkuu 3.mawaziri wote na manaibu 4 .wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama 5.wakuu wa mikoa 6.wakuu wa wilaya 7.wakulugenzi 8.makatibu tawala 9.wakuu WA idara mfano uhamiaji 10.wakuu WA Tasisi mfano Tasisi ya kuzuia na kupambana 11. Mkaguzi na mdhibiti WA hesabu za serikali huyu Kwa asilimia 10 % yupo free sasa hii ni sawa Kwa akili ya kawaida ..haya uchaguzi ukifika mkurugenzi ndiye msimamizi anasimamia nn wakati ni kitu kimoja Kwa hyoo katiba MPYA ni mhimu na ikisukwa vizuri
 
Unadhani watanzania hawajui umuhimu wa katiba mpya? Je katiba mpya ni muarobaini wa matatizo yetu wakati nyani ni wale wale na msitu ule ule wakicheza unyani ule ule? Afrika Kusini na Kenya wana katiba mpya na nzuri lakini je maisha yao yamebadilika? Mie nadhani tuwe na mfumo wa haki na huru hata kama ni bila katiba. Katiba sawa na bendera hailiwi.
Katika kipindi cha miaka kumi ya Kenya kupata katiba yake mpya Kenya imepiga hatua kubwa kutoka utawala wa Urais wa Kifalme na Kiimla kwenda kwenye maendeleo yanayochochewa na raia kwenye ngazi za majimbo. Fahamu tu kwenye ukanda huu wa Africa Mashariki Kenya ndio taifa lenye maendeleo makubwa kuzidi wote katika kila sekta.
 
Mwanangu unaweza kutoa japo takwimu kidogo na kulinganisha na mataifa mengine kwenye ukanda wetu?
 
Africa Kusini imekuwa huru mwaka 1994, Tanzania ni Taifa huru tangu 1961. Katika kipindi kifupi cha kuwa huru SA imekuwa na demokrasia imara inayoheshimu haki za raia na kutoa uhuru mpana sana kwa raia wake.
Unaijua Afrika Kusini au unaongea tu? Kama katiba mpya imeleta faida basi ni kwa elites na wafanyabiashara ambao wengi ni wahindi na wazungu lakini si waafrika walio wengi mwanangu.
 
Siijui, kumbe katiba yao ya kabla ya mwaka 1996 chini ya utawala wa Ubaguzi wa Rangi ilikuwa na faida kwa Waafrika wengi!
Sasa kwa nini ANC na Mandela walitaka katiba mpya ambayo ilikuwa inatoa usawa kwa jamii zote za Africa Kusini ?!
 
Naona kama hujanielewa na kutaka kuniwekea maneno kinywani. Simaanishi kuwa katiba ya makaburu ilikuwa nzuri. Situations za Afrika Kusini na Tanzania ni tofauti. Katiba yetu siyo ya kikoloni kama ilivyokuwa ya Afrika Kusini. Kinachoongelewa ni matumaini ya wananchi kama yalivyokuwa yamewekwa kwenye katiba mpya. Ninachosema ni rahisi. Kuna njia ya kurekebisha mambo mojawapo ikiwa ni katiba mpya na njia nyingine kama mfumo mzuri wa kutoa haki.
 
Wakuuu najaribu kuwaza kwa mapana, Tanzania tunatumia KATIBA ya mwaka 1977 na huu ni mwaka 2021.

Malalamiko ni mengi mno kutokana na KATIBA ya HOVYO.

Je Watanzania siku wakifahamu hili SWALA ni muhimu nini KITATOKEA na ni lini watafahamu ?
Nimeona maono, siku si nyingi yatatumia. Yesu anakuja kulinyakuwa kanisa lake, wateule tukae tayari kumngojea Bwana Harusi
 
Wakuuu najaribu kuwaza kwa mapana, Tanzania tunatumia KATIBA ya mwaka 1977 na huu ni mwaka 2021.

Malalamiko ni mengi mno kutokana na KATIBA ya HOVYO.

Je Watanzania siku wakifahamu hili SWALA ni muhimu nini KITATOKEA na ni lini watafahamu ?
Katika watu wote wakumlaumu ni nyerere. Yeye ndio chanzo cha katiba mbovu ingawa watu wengi hawalioni hilo.
Hakutaka demokrasia alichagua uimla ndio huo unatitesapaka leo.
Gwaji boy na slaa wamechapwa na katiba mbovu, hakuna uhuru wa kujieleza ndani na nje ya vyama vyote vya siasa
 
Nyerere ni mtu hatari ,Kwa mfano Zanzibar aliinyima jeshi mengne akawapa
 
Wakuuu najaribu kuwaza kwa mapana, Tanzania tunatumia KATIBA ya mwaka 1977 na huu ni mwaka 2021.

Malalamiko ni mengi mno kutokana na KATIBA ya OVYO.

Je, Watanzania siku wakifahamu hili suala ni muhimu nini kitatokea na ni lini watafahamu?
Wengi wa Watanzania wanajua na kufahamu fika umuhimu wa Katiba hii hii ya mwaka 1977. Suala siyo muda wa Katiba, naambiwa kuwa Katiba za nchi nyingi ikiwa ni pamoja na za USA na UK na USSR zina miaka mingi kuliko hii ya mwaka 1977 na bado, kama hii ya kwetu ya mwaka 1977, zinafanya kazi na KUKIDHI matakwa na mahitaji ya wengi. Sasa kuna wale wachache, ambao hawakosi popote ikiwa ni pamoja na Mbinguni (si mnajua habari za Shetani na uasi wake kule Mbinguni), wenye kupinga ANYTHING kwa faida aidha yao au ya wale wanaowatuma na kuwatumia kwa maslahi yao binafsi. Rais SSH kesha sema apewe muda, aweke mambo nchini sawa then atakuja kwenye hili mnalotaka ambalo MNADHANI NDIYO MUAROBAINI NA DAWA YA MATATIZO NA KUSHINDWA KWENU!
 
Itafika tu huo wakati na ukifika watawala watajua na watasoma alama za nyakati watafanya kilicho mbele yao ili waendelee kuwa kwenye reli bila vurugu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom