Siku wananchi wakichoka kunyanyaswa nani atalinda usalama wa Askari Polisi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku wananchi wakichoka kunyanyaswa nani atalinda usalama wa Askari Polisi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, Jan 11, 2011.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu wanaJF, ninavyofahamu mimi polisi wanatakiwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria na kanuni zilizopo. Lakini cha kushangaza jeshi hilo limekuwa likitetea maslahi ya CCM na Mafisadi hata kama ni kwa gharama ya kuwapiga risasi wananchi.

  Mfano mzuri ni wakati wa uchaguzi ambapo jeshi la polisi na askari wake wamekuwa wakitimiza majukumu yao kwa kuipendelea CCM hata hata kama ni kutofuata sheria na kanuni kama vile kukataa kulinda helicopter aliyokuwa akiitumia Dr. Slaa wakati wa kampeni na kuwaachia wanaCCM wakifanya vurugu kwenye mikutano ya CDM.

  Ni jambo la kusikitisha hasa pale unapokuta polisi wanahatarisha usalama na maisha ya mwananchi badala ya kulinda usalama.

  Swali langu kubwa ni kwa jinsi tunavyofahamu idadi ndogo ya jeshi hilo ukilinganisha na idadi ya wananchi, Siku wananchi wakichoka kuvumilia je ni nani atalinda usalama wa polisi mitaani? maana tuko tunakaa nao mtaani.

  Ushauri wangu kwa jeshi la polisi ni kwamba wafanye kazi zao kwa kufuata sheria na si maagizo ya CCM na serikali yao. Mfano wa jeshi hilo kutotosha hata kuwathibiti wananchi wa mkoa moja upo wazi hata pamoja na silaha zote.

  Tumeona juzi tu Arusha ilibidi wachukue askari kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Dar na vurugu zilikuwa Arusha mjini tu je ingekuwa mkoa wa arusha wote watu wameandama ingekuwaje.

  Askari najua mko humu JF hasa WAKUBWA tafadhali msifanye kazi kwa maagizo ya CCM mtapata matatizo ya kutokaa mtaani vizuri na watoto wenu watanyanyasika.
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nawaonea huruma. Siku zao ziko tu karibu

  Kama Congresswoman kala shaba, hawa nao watakula beto one day.

  Na hivyo tunakaa nao vibanda umiza huku na wengine jioni tunagongana nao mitaani wamepiga ulabu hadi wanaangukia mitaroni, we ngoja ni kuwafanuyia kitu cha mande


  Watalipa damu za ndugu zetu wanaowaua bila msingi wowote
   
 3. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
   
 4. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  [​IMG]

  Hizi avatar zote ni za kimapinduzi lakini je, zinaendana na dhamira na nia zenu??
   
 6. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu atahukumu
   
 7. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gharibu bilal yupo serengeti na wanawake wawili katika mapumuziko na gharama zake ni 10m kwa siku . Sasa kaenda na waker wawili hii hatari kwa matumizi makubwa ya fedha wakati wahadhari wanamtaka akajibu maswali udom
   
 8. M

  Mesaka Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wananch msiwe na Hasira sana na Polisi, kwanza nao ni wananchi wenzetu, wanachofanya ni kutekeleza maaigizo ya watawala kama walivyoapa kuwa watii kwa Rais.

  Mbona mnasahau kwamba Rais wa Tz alisema atawaamuru polisi watumie silaha za moto? hivyo kuwatia vilema yeyote atakaye andamana? kumbukeni alivyo kuwa akitaka wafanyakazi wasiandamane.

  Sasa yaliyotokea Arusha ndiyo hayo Rais aliyasema may, 2010, na polisi wametekalaza amri au agizo la amiri jeshi mkuu.

  Hivyo naomba tusiwachukie tu Polisi mchukieni anaye watuma.
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,613
  Likes Received: 4,719
  Trophy Points: 280
  mkuu ushauri wako mzuri lakini angalia usijepigwa ban kuwa unatishia watu maisha . Yamenikuta
   
 10. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  To my side the answer is absolutely YES. Mabadiliko lazima.
   
 11. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Usiogope mimi natoa ushauri maana sometimes hawajui madhara ya wanayoyafanya.
   
 12. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Si kweli maana unapotumwa kumwuua mtu na wewe unatekeleza ni sheria gani inasema hivyo? Leo hii CCM ndio iliwatuma askari lakini sisi ndio tumepoteza wananchi wenzetu. Ushauri wangu uko pale pale wasifanye kazi kwa maagizo ya CCM.
   
 13. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Rudi kwenye mada.
   
Loading...