• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Siku Waingereza walipowapiga mabomu ya machozi wananchi wa Kamachumu

Mohamed Said

Mohamed Said

Verified Member
Joined
Nov 2, 2008
Messages
13,339
Points
2,000
Mohamed Said

Mohamed Said

Verified Member
Joined Nov 2, 2008
13,339 2,000
Azaria C. Mbughuni
December 31, 2019 at 10:05 PM ·

''One thing that Mwalimu Nyerere did every December between 1953 and 1959.

December 1953 Mwalimu Nyerere visited Bukoba to investigate an incident at Kamachumu where the police used teargas to disperse a crowd.''

Hayo hapo juu nimenyambua kutoka kwa Prof. Mbughuni.

Naomba nishereheshe kidogo ili safari hii ya Mwalimu Nyerere kwenda Bukoba kuhusu wananchi kupigwa mabomu ieleweke vyema:

''Katika mambo ya kusikitisha sana wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika ni kisa cha wananchi waliokuwa katika mkutano wakimsikiliza kiongozi wao Ali Migeyo, kupigwa mabomu ya machozi huko Kamachumu.

Lakini jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa shujaa huyu wa uhuru wa Tanganyika historia imemsahau.

Hakuna popote pale ambapo utalisikia jina lake likitajwa.

Nimekutana na Ali Migeyo wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.

2259215_1577939271432.png

Bahati nzuri Mutahaba ameandika kitabu cha maisha ya Ali Migeyo, ''The Portrait of a Nationalist,'' na ndani ya kitabu hiki kuna mengi kiasi yamenifanya mimi kuamini na nikaandika katika kitabu cha Sykes kuwa kama si kwa Ali Migeyo kufungwa kufuatia kesi ya mabomu ya machozi kwa hiyo kuasisiwa kwa TANU mwaka 1954 kumkuta akiwa jela ya Butimba akitumika kifungo cha miaka mitatu, Ali Migeyo angekuwa mmoja wa wale waasisi 17 wa TANU.

Baada ya uhuru Ali Migeyo aliwekwa kuzuizini Ukonga Prison kwa tuhuma ya ''kuchanganya dini na siasa'' lakini akaja kutolewa baada ya kuteuliwa na Rais Nyerere kuwa Mbunge.

Inspector General of Police (IGP) Hamza Aziz alinihadithia kuwa alipopewa amri ya kwenda kumtoa jela Ali Migeyo alishtuka jinsi alivyomkuta.

Migeyo alikuwa ndani ya selo yake hana nguo.

Ilibidi arudi mjini amnunulie nguo na viatu ndipo aliporejea jela na kujanae mjini akampangia International Hotel akae wakati anasubiri kwenda bungeni, Karimjee kuapishwa.

Napenda kuhitimisha kwa kusema kuwa baada ya Migeyo kufungwa mwaka wa 1954, Abdul Sykes, Julius Nyerere alikwenda kijijini kwake Bugandika kuijulia hali familia yake.

tatizo kubwa ambalo nimeliona katika kumwandika Mwalimu Nyerere ni kuwa huwa ahusishwi na mtu mwingine hata kama alikuwa bega kwa bega na yeye.

Hii inatoa ladha historia yake.
Mifano iko mingi sana.

Sijui kwa nini Mwalimu alikuwa kimya kuhusu wenzake.

Mfano pale Makao Makuu ya TAA New Street alikuwapo Dr. Michael Lugazia yeye 1953 katika harakati za kuunda TANU ndiye alikuwa kiungò baina ya Makao Makuu na TAA Bukoba akiwatia hima viongozi wa Bukoba kutorudi nyuma kwa ajili ya kufungwa Migeyo waendelee na mapambano.

Dr. Lugazia hatajwi popote katika historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Dr. Lugazia alimaliza udaktari wake Ocean Road Hospital Dar es Salaam na amekufa akiwa na kinyongo kuhusu historia ya TANU.

Dr. Lugazia katika miaka yake ya mwisho alifungua kinywa chake kwa yeyote aliyekuwa tayari kumsikiliza akawa anaeleza historia ya kweli ya kuasisiwa kwa TANU.''
 
L

Laki Si Pesa

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2018
Messages
2,819
Points
2,000
L

Laki Si Pesa

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2018
2,819 2,000
hicho kitabu cha Abdul Sykes itabidi tukitafute sasa inaonekana kina mambo mengi sana, lakini kwa nini cover la kitabu lisingekuwa hivi " HISTORIA YA TANU ILIYOSAHAULIKA" hapo ingeleta hamasa kwa watu wengi, kuliko kukiita Abdul Sykes watu wengi watajua kinaelezea historia binafsi ya abdul sykes
 
Mohamed Said

Mohamed Said

Verified Member
Joined
Nov 2, 2008
Messages
13,339
Points
2,000
Mohamed Said

Mohamed Said

Verified Member
Joined Nov 2, 2008
13,339 2,000
hicho kitabu cha Abdul Sykes itabidi tukitafute sasa inaonekana kina mambo mengi sana, lakini kwa nini cover la kitabu lisingekuwa hivi " HISTORIA YA TANU ILIYOSAHAULIKA" hapo ingeleta hamasa kwa watu wengi, kuliko kukiita Abdul Sykes watu wengi watajua kinaelezea historia binafsi ya abdul sykes
Laki,,,
Historia ya Abdul Sykes ni historia ya pekee sana.

Si watu wengi Mungu anawajaalia kupitia kufanya makubwa kwa jamii zao kama alivyofanya Abdul Sykes.

Ikutoshe tu kuwa waliogopa kumtia katika historia ya Tanganyika na TANU wakafuta jina lake na la mdogo wake Ally na la baba yao Kleist.

Si bure kuna jambo hapo.

Si unaona wewe mwenyewe ushapata mshawasha wa kumjua Abdul?

Nilichagua kukipa kitabu jina la Abdul kwa sababu nyingi sana.

Kubwa niliamua kutumia uandishi wa historia ya TANU kwa staili ya ''biographical approach,'' yaani kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kupitia maisha ya Abdul Sykes.

Sababu yake ni kuwa tayari historia iliyokuwapo ilikuwa imemweka Nyerere kama ndiyo muasisi pekee wa TANU.

Nilimleta Abdul na historia ya TANU kwa staili hiyo kuwafikirisha wasomaji wangu.

Kwa hakika kitabu kiliwashtua pakubwa.

Hebu soma hii:

Kila msomi aliyepata historia ya hawa akina Sykes alivutiwa kutaka kujua zaidi ni nani watu hawa?

John Iliffe mwanahistoria wa University of Cambridge wakati anasomesha Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar es Salaam 1960s ndiye aliufungua mlango huu.

Nina file nimelipa jina ''Sykes Obsession'':

Ndjabu...
Ondoa tu hayo matusi hayana maana lakini yote uliyoandika ni muhimu. Obsession honestly...Hakika kisa cha akina Sykes ni kisa mimi kimenikamata sana.

Achilia ule udugu lakini siku niliposoma kitabu, ''Modern Tanzanians,'' kitabu alichohariri John Iliffe na kusoma, ''The Townsman: The Life of Kleist Sykes,'' sura iliyoandikwa na mjukuu wa Kleist Sykes, Aisha ''Daisy'' Sykes Buruku historia hii ilikamata fikra zangu (Modern Tanzanians, (ed), East African Publishing House, Nairobi, 1973).

Nakumbuka kama vile jana nilikuwa katika Maktaba ya Taifa, Arusha ndipo nilipokikuta kitabu hiki.

Utafiti wangu wa kutaka kujua mengi ulianza siku ile.

Nikawauliza hawa ndugu zangu juu ya kitabu cha Iliffe.

Wakanifahamisha kuwa babu yao, Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949 alikuwa ameandika ''kitabu,'' ambacho alimwachia mwanae Abdul Sykes.

Kwa hakika hakikuwa kitabu bali mswada wa kitabu. Mwanae Abdul Sykes, Daisy alipoingia Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki mwaka wa 1967 kusoma Elimu na Historia ndipo alipokutana na John Iliffe na huyu mwalimu wake baada ya kufahamu historia ya akina Sykes na yeye kama mimi akakumbwa na hii ''obsession,'' akataka kujua mengi vipi walifika
Tanganyika kutoka Afrika ya Kusini.

Hapo ndipo Daisy akawa anachukua nyaraka zilizokuwa katika familia na kumuonyesha Iliffe pamoja na mswada wa kitabu alichoandika babu yake...

Kutokana na nyaraka hizi Iliffe akaandika paper hii: '‘The Role of the African Association in the formation and Realisation of Territorial Conciousness in Tanzania.’ Mimeo, Universityof East Africa Social Sciences Conference,'' 1968.

Iliffe kapatwa na homa ya ''obsession,'' ya akina Sykes anataka kujua mengi zaidi Daisy akipewa ''assignment,'' anakwenda kwa baba yake anauliza anapewa maelezo na ushahidi wa nyaraka.

Iliffe kila akielezwa hili ndani linazuka jingine akataka kujua ilikuwaje Abdul Sykes akawa General Secretary wa Dar es Salaam Dockworkers Union mwaka wa 1948.

Iliffe akapewa maelezo na nyaraka akaandika paper hii:‘A History of Dockworkers of Dar es Salaam’ TNR, Dar es Salaam, 71, 1970.

Iliffe kama mimi miaka mingi baadae akawa Sykes, Sykes na Sykes.

Sijui kwa nini Iliffe hakuandika historia ya TANU kwa ukamilifu wake wala hakuwa na shauku ya kukutana na Abdul Sykes, baba wa mwanafunzi wake hodari Aisha ''Daisy,' Sykes ambae kamsaidia sana kuijua historia ya African Association na TANU.

Mohamed Said na yeye kwa kumsoma Iliffe gonjwa la Sykes likamkumba.

Mimi nikaamua kufanya kile Iliffe hakufanya nacho ni kuandika maisha ya Abdul Sykes lakini nikaamua pia kuweka mguu wangu pale unyayo wa Iliffe ulipokanyaga.

Hapa ndipo ilipoaanza safari yangu iliyonifikisha hadi Imhambane kijiji kinachoitwa Kwa Likunyi alipotoka Sykes Mbuwane kuelekea Laurenco Marquis akiwa ameongozana na Chief Mohosh na Wazulu wengine kupanda manowari ya Wajerumani kuja Pangani kuanza vita na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa mwishoni mwa miaka ya 1880.

Huyu Chief Mohosh ndiye akaja kujulikana kama Affande Plantan Tanganyika akiwa mkuu wa Germany Constabulary.

Prof. Emmanuel Achiempong wa Harvard na yeye gonjwa la Sykes likamkumba akaniandikia mwaka wa 2008 kuniomba anijumuishe katika mradi wa Dictionary of African Biography (DAB) anataka niandike mchango wa Kleist Sykes katika historia ya Afrika.

Mradi huu ulijumisha waandishi na watafiti takriban 500 kutoka kila pembe ya dunia. Oxford University Press, New York wamechapa volumes sita ya kazi hii.

Ndjabu,
Yako mengi lakini kwa leo tuuishie hapa sitaki kuwachosha wasomaji.

NB:
Mwaka wa 2011 katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika serikali ikaamua kutunuku Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa Ally na Abdul Sykes kwa kutambua mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.''
 
K

Kamara Kusupa

New Member
Joined
Jul 16, 2018
Messages
1
Points
20
K

Kamara Kusupa

New Member
Joined Jul 16, 2018
1 20
Kuna makusudi mabaya ya kuficha ukweli wa historia ya makubwa yaliyofanywa na wazalendo wengi enzi za kupambana na ukoloni, walioficha hawakutaka kizazi kipya cha Watanzania kujua walikotoka hadi hapo walipo. Lakini ukweli hautafichika kwa wakati wote, ila Mohamed Said usiache kuweka wazi sababu zilizofanya Alli Migeyo awekwe kizuizini. Ipo haja kwa wanazuoni kufafanua juu ya mada ya KUCHANGANYA DINI NA SIASA ama mada ya HATARI ZA SIASA ZA KIDINI. Tuliona kwenye utawala wa Rais Mwinyi jinsi baadhi ya Waislamu walivyokuja na moto wa kidini wakavunja bucha za nguruwe, wakashinikiza Tanzania iwe mwanachama wa OIC. Wakaibuka tena wakati wa Rais Kikwete wakashinikiza Hijabu mashuleni na mahakama ya kadhi, KWELI HAYO YANAWEZA KUTUFANYA TUWE NA TANZANIA IMARA?
 
balibabambonahi

balibabambonahi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Messages
8,350
Points
2,000
balibabambonahi

balibabambonahi

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2015
8,350 2,000
Ninacho
hicho kitabu cha Abdul Sykes itabidi tukitafute sasa inaonekana kina mambo mengi sana, lakini kwa nini cover la kitabu lisingekuwa hivi " HISTORIA YA TANU ILIYOSAHAULIKA" hapo ingeleta hamasa kwa watu wengi, kuliko kukiita Abdul Sykes watu wengi watajua kinaelezea historia binafsi ya abdul sykes
Sent using Jamii Forums mobile app
 
boywise

boywise

Member
Joined
Mar 20, 2017
Messages
42
Points
125
boywise

boywise

Member
Joined Mar 20, 2017
42 125
Kuna makusudi mabaya ya kuficha ukweli wa historia ya makubwa yaliyofanywa na wazalendo wengi enzi za kupambana na ukoloni, walioficha hawakutaka kizazi kipya cha Watanzania kujua walikotoka hadi hapo walipo. Lakini ukweli hautafichika kwa wakati wote, ila Mohamed Said usiache kuweka wazi sababu zilizofanya Alli Migeyo awekwe kizuizini. Ipo haja kwa wanazuoni kufafanua juu ya mada ya KUCHANGANYA DINI NA SIASA ama mada ya HATARI ZA SIASA ZA KIDINI. Tuliona kwenye utawala wa Rais Mwinyi jinsi baadhi ya Waislamu walivyokuja na moto wa kidini wakavunja bucha za nguruwe, wakashinikiza Tanzania iwe mwanachama wa OIC. Wakaibuka tena wakati wa Rais Kikwete wakashinikiza Hijabu mashuleni na mahakama ya kadhi, KWELI HAYO YANAWEZA KUTUFANYA TUWE NA TANZANIA IMARA?
Mkuu Kamara Kusupa umemalizia kwa swali zuri ambalo jibu lake ni NDIYO tunaweza kuwa na Tanzania Imara kwa hayo uloyataja na mengine mengi ikiwa Dini haitotumika kuwanyanyua hawa na kuwadidimiza wale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,404,215
Members 531,529
Posts 34,447,684
Top