Siku uliyofika Jijini Arusha, Jijini Dar es Salaam au Jijini Mwanza kwa mara ya kwanza ulipaonaje?

Kwani bila foleni DSM, kutoka Boko hadi Kongowe ni muda gani? Nina uhakika humalizi Arusha kwa dk 5 lkn pia ukweli ni kwamba miji yetu ni midogo. Sijui unalinganisha na mji gani ila kwa Tanzania tu, Arusha imeacha miji mingine mbali sana isipokuwa DSM. Iwe kwa miundo mbinu ya barabara, majengo na mishe mishe za mjini kwa ujumla.
Achana na muda,angalia umbali. Boko hadi Kongowe si chini ya 30km. Kama uko na gari inatembea 60kph ni nusu saa. Je km30 si ushatoka Arusha uko Moshi?
 
Mnalinganisha Arusha na mji upi labda? Inaonekana kuna wengine wamefika Dar na Arusha tu. Arusha kwa Tanzania hii ni mji mkubwa sana na inastahili sifa inazopewa. Arusha ina majengo ya maana. Ina Barbara za lami za kutosha. Ni mji gani mwingine wenye barbara za lami mji mzima kama Arusha ukiondoa DSM?
 
Mtoa mada ungetoa mfano wa jiji ambalo unaona ni bora kuliko iyo arusha tuweze kufanya comparison

Categories zipi umeangalia mpaka kufikia kusema kuwa arusha ni ya kawaida

Mbona ata mimi nimefika bongo mwaka jana...ubungo stand niliyotegemea kuikuta ni tofauti kabisa na ukiskia kwa watu wanavotueleza wakati ndo.jiji kubwa Tz
 
Nijuze waliweka rami mwaka gani maana nadhani 2017 mwishoni au 2018 mwanzoni ndio nilipita pale ikiwa full vumbi
Wewe unaongea kufurahisha genge au unaongelea ulichokiona?

Barabara ya kisongo ina lami muda mrefu sana! Nakumbuka nilipita hiyo barabara kuanzia 2014 hadi muda huu.
Tena kwa sasa ile barabara ya east Africa imepita kwa mbele yake kilomita chache kutoka mjini Arusha
 
Mimi niliona kama nipo Gongo la Mboto hivi. Eti ndani ya dakika 5 nimeumaliza mji wote!

Hahaha ila wenyewe wakikuhadithia sasa, uongo mwingi sana, utasikia Geneva ya Africa!

Machalii wa Arusha mnazingua asee, Arusha ni ya kawaida sana!

MAPOVU YOTE RUKSA!
HAhhaa.

Hawa machali si ndio wamesombwa na maji ya mtaro?
 
Back
Top Bottom