Siku ukiona Mwajiri anaomba Msamaha kwa Mwajiriwa Tambua Adhabu inapande Mbili

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,036
3,478
Wakuu,

Kama mada inavyotanabahanisha, nchi yetu ya Tanzania ina wananchi na wageni wote wanalipa kodi zote stahiki ijapokuwa wanaweza wasitambue kwamba walipa kodi hizo.

Ilikupambana na maadui watatu tuliowarithi kutoka ukoloni ni watatu ijapokuwa wapo walioongezeka baada ya kupewa hati ya umiliki wa kipande cha eneo kwa matumizi mtambuka ya kibinadamu.

Maadui
1. Umasikini-tumezaliwa tukaukuta na bado upo kwa kiwango kinachotofautiana kutoka eneo moja had jingine. Hakuna serikali duniani ambayo ilishafaulu kumaliza umaskini miongoni mwa watu wake ila hutengenezwa mazingira wezeshi, salama, nafuu na rafiki kwa nguvu za pamoja na mtu mmoja mmoja kufanya bidii kujiletea maendeleo ya toshelezi kwa nchi kiuchumi, kijamii, kibinafsi na kwa aina ya uongozi tunaoutaka kufanikisha lengo hilo. Mfano-Marekani pekee ina zaidi ya watu milioni arobaini (mil 40) wanaoishi chini ya dola moja lakini huwezi kusikia wametajwa na jumuia yoyote kwamba hali hiyo ipo

1604244820283.png
1604244893614.png

Hapo ni Marekani jimbo la Escobares mpakani na Mexico, hali ya umaskini inatisha

2. Maradhi-tumezaliwa nayo, yamehangaisha wazazi, tumehangaika nayo hadi sasa bado yapo na uwezo wa kupambana nayo ni duni isipokuwa wenye vipato vya uhakika na kutosha lakini nao wanahangaika na hayo maradhi mara nyingine yanawashinda kama wananchi wa chini wanaotegemea neema ya Mwenyezi Mungu. SULUHISHO: Huduma za afya ziwe nafuu kwa watu wote kupitia bima ya afya. Usumbufu kwa wazee, akina mama wajawazito, walemavu, watoto, wasiojiweza kiuchumi uondolewe ili kuleta nafuu ya kimaisha.

3. Ujinga-tumezaliwa tukiwa wajinga, tumelewa tukiwa wajinga, tumekua tukasomeshwa kwa njia rasmi na za kijamii lakini tunaendelea kuwa wajinga. TATIZO hatukiri na kukubali kwamba wote sis ni wajinga na kwamba tunahitaji kuelimishwa, tutambue makosa na udhaifu wetu kisha tujibiidishe kuuondoa ujinga. Kimsingi kuna ujinga wa aina mbili kuu ijapokuwa zaweza kuwepo nyingi kadhaa. i) ujinga wa juu juu-huu unawahusu wanafunzi wanaofunzwa jambo fulani ambalo hawajawahi kulijua wala kubashiri kwamba lipo, kwanini lipo na linauhusiano gani na mwanadamu.

Watu wengi wanaojumuishwa kwenye kundi hili la ujinga ni watu wanaoongozwa ambapo wenyewe wanafikiri kuna mtu mwingine ambaye anajua kuwasaidia wao kujua wakati walitakiwa kujibiidisha kuyafahamu vema mazingira yanayowazunguka na kuhoji kwanini yapo namna hiyo ilvyo ili waelewe na kujua. ii) ujinga wa kweli-huu unawajumuisha watue ambao tayari walishajitahidi kufuatilia jambo fulani ili waelewe pamoja na wasomi na watalaamu ambao kimsingi wanajua kwamba hawajui na kwamba hakuna mwingine anayejua lakini wanashupaza shingo kwa kuwapotosha wengine ili wabaki wakionekana ndio wanaojua hivyo kusababisha lengo la kupunguza ujinga kama sio kuuondoa kabisa wanakwamisha kwa makusudi kwa faida ya kuhodhi fursa na ukwasi binafsi. SULUHISHO-Elimu ya awali, msingi na sekondari (kidato kwanza-kidato cha sita) wasilipe ada).

Chuo-ada ipunguzwe na marejesho kwa anayepata kazi yawe asilimia saba kila mwezi na sio kumi na tano kama ilivyorekebishwa kwenye sheria Kuondoa ada chuo ni vigumu na wala ILO article hailazimishi kufanya hivyo ila kama nchi inakunsanya kipato cha kutosha kutokana na miradi mikakati iliyoiva ni busara kutoa ruzuku kwenye vyuo husika ili ada ipunguzwe kwa kiwango kinacholipika kwa kila mwanafunzi anayechaguliwa kujiunga kupata maarifa mbalimbali ili hatimaye kusaidia kuondoa ujinga uliotopea miongoni mwa jamii. Ikumbukwe kwamba hata wasomi na wenye taaluma nao wana ujinga wa kweli wa kujifanya wanajua wakati hawajui. Hii ina maana kwamba elimu ya darasani ni nyongeza ya ujuzi kuwa jasiri kupambana na changamoto za maisha.

Maadui Nyongeza ndani ya kizazi kipya
1.Rushwa, ufisadi na ubadhirifu
2. Ubaguzi (kijinsia, hali ya maumbile, dini, kabila, kanda, itikadi siasa, rangi, nguvu za kiuchumi,, kielimu, matumizi mabaya ya nafasi za kiuongozi

Matokeo hasi
1. Mifarakano
2. Chuki,
3. Visasi,
4. Migogoro,
5.Kukwamisha maendeleo jumla
6. Kukwama kwa maendeleo binafsi
7. Manung'uniko na lawama singiziji

Nawasilisha
 
Unapiga picha za makambi ya wahamiaji haramu waliovurushwa kurudi kwao Mexico na kuwaita maskini wa marekani? Hebu zungukazunguka maeneo mengine utuletee picha zenye uhalisia na hoja yako! Kinyume chake hatununui propaganda hii kwani ipo too low!
 
Back
Top Bottom