Siku tukiachana wa kuichunguza serikali na kuyasema kwa uwazi makosa yake ndiyo itakuwa mwanzo wa kuidumaza

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Siku tukiachana na utamaduni wa kuichunguza serikali na kuyasema kwa uwazi makosa yake ndiyo itakuwa mwanzo wa kuidumaza kama siyo kuchimba kaburi la umasikini.

Wakati wa Julius Nyerere kulikuwa na ukosoaji mkubwa juu ya sera za uchumi,waliokosoa wakati huo walionekana siyo wapenda maendeleo,waliitwa mabeberu,baada ya muda wakaonekana walikuwa sawa.

Wakati wa Mwinyi kulikuwa na ukosoaji mkubwa juu ya sera za soko huria na utekelezwaji wa sera na mipango ya benki ya dunia na shirika la fedha ulimwenguni,waliokosoa walionekana kama vichaa hivi,lakini baada ya Mwinyi kutoka wakaonekana wapo sawa.

Wakati wa Mkapa wakaibuka wakosoaji wakubwa kuhusu sera ya ubinafsishaji na ukaribishwaji wa makampuni makubwa kutoka nje wakina Prof Chachage,Haroub Othman,Issa Shivji,Jenerali Ulimwengu,Tundu Lisu,waliitwa watu wenye wivu waliojitwisha upofu wa kutoona maendeleo makubwa kwenye uwekezaji na ujenzi wa miundo mbinu,baada ya Mkapa kutoka ndiyo tukaja kujua kuwa hawa watu walikuwa sawa!

Alipokuja Kikwete,wakaibuka wakosoaji wakubwa hasa baadhi ya vyombo vya habari,sauti za matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya watendaji wa umma,Rushwa kukithiri,watu kujilimbikizia mali zilisikika kila kona,wakosoaji hawa akina Dr Slaa,Zitto Kabwe,David Kafulila,Deo Filikunjombe,John Mnyika,magazeti kama mwanahalisi wakaitwa wanaharakati,wapinzani,baadhi ya watu walisema wanatumiwa na mataifa ya nje ili kutaka kuwagombanisha watanzania na kuifanya nchi isitawalike,wengine waliitwa Tumbili,leo wameonekana kumbe walikuwa sawa kabisa kwenye ukosoaji wao.

Kwenye serikali hii kumeibuka kundi la wakosoaji wakubwa kwenye sera za uchumi za serikali ya sasa,ukosoaji mkubwa umejikita kwenye sera,mipango na mfumo wa utawala,tayari wakosoaji washaanza kuitwa kuwa watu wasio na uzalendo.

Kama ilivyo huko nyuma,baada ya Rais Magufuli kumaliza kipindi chake,hawa wanaoitwa siyo wazalendo itakuja onekana kumbe ndiyo walikuwa wazalendo kwa kuwa na moyo wa kusema bila woga yale wanayoamini yanaweza kuisaidia serikali.

Tusiache kuikosoa serikali na kuionesha nini. ingefanya,tukiacha tutakuwa tumefanya kosa kubwa,inapofanya vizuri ipongezwe na kuambiwa hapo sawa kabisa,shikilia hapo hapo.Muwe na mapumziko mema ya mwishoni mwa wiki.

Mwanahabari Huru
 
kukosoa na kupinga, kukejeli, kudhihaki ni vitu tofauti, mkosoaji anakupa nafasi ya kipi bora kingekuwa kile ulicho fanya, how better you were to do, sasa Tanzania watu wa hivyo hawapo, wapo wasaka tonge, Hawana msimamo, mchana anasema hivi, asubuhi yake anasema vile, anampinga huyu, kesho anamsapoti pasipo sababu, wala kufuta ile kauli ya mwanzo. poor wapingaji TZ
 
kukosoa na kupinga, kukejeli, kudhihaki ni vitu tofauti, mkosoaji anakupa nafasi ya kipi bora kingekuwa kile ulicho fanya, how better you were to do, sasa Tanzania watu wa hivyo hawapo, wapo wasaka tonge, Hawana msimamo, mchana anasema hivi, asubuhi yake anasema vile, anampinga huyu, kesho anamsapoti pasipo sababu, wala kufuta ile kauli ya mwanzo. poor wapingaji TZ
Wewe ni wa komoro?
 
Back
Top Bottom