Elections 2015 Siku tano za kampeni: Chokochoko za CCM, serikali yake na vyombo vya ulinzi

Huu uzi nimeu-screen shot, ikifika tar 1 September, utaisaidia polisi, watu waropokaji kama nyie ndo tunawatafuta!!! Usidhani nyuma ya keyboard uko safe!

We ---- nini?Acha kutisha watu kijinga....lofa wewe
 
Tuliombee Taifa linapita kwenye kipindi kigumu, ni hatari sana kuamua jambo litakalo egemea upande wowote wakati huu,

Naamini katika mungu lkn hizi fikra za kuomba huku dhamira haikutumi kutenda haki hata uombe mpaka jioni hakuna kitakachobadilika. Dhamira yetu kama mchi itutume kutenda haki amani itakuja yenyewe
 
Kulalamika humu ndani hakutusaidii, tuufahamishe umoja wa mataifa, mahakama ya kimataifa ICC na mashirika makubwa ya haki za bindamu kama transparency international na Human right watch wajue unyama unaoendelea. Tukinyamaza bila kupaza sauti nje hakuna takayejua tunaumia
 
Ukawa wakianza mchakamchaka huko mashinani si ndo watawapiga risasi huku wanatembea?
 
mod;

angalia kichwa cha habari hapo juu,

badilisha ; jf inatumika vibaya

mbona unatutisha. Rekebisha wewe basi na uisome kwa jinsi unavyotaka wewe lakini humu usiiweke.
Kuna uongo kwa alilolieleza Mtatiro?
Hukumsikiliza Chagonja jana? Na leo polisi wanazikamata bodaboda hovyohovyo kila kona ya jiji ili kuwatisha au kuwadhoofisha wapenda mabadiliko kuhudhuria shughuli ya jumamosi.
Kwa taarifa yako na wenye kubuni mbinu za kuidhoofisha ukawa tuna plan b,c,d na e. Mtasumbuka sana lakini hamtatuweza na ikulu ccm hamwendi mwaka huu.
 
Wapi katika bandiko lake amechochea vurugu ?

Kwani aliyoyaandika hayajatokea?

Binafsi nimeshajiandaa kuwatifua
fafanua lolote linaweza kutokea ina maana gani fuateni taratibu km kura zitatosha mtapewa nchi si kuleta vurugu hapa patachimbika.
kwani ni lazim wapewe huo uwanja wa mikitano? ni mali yao ?hakuna siku wapinzani watahisi wanatendew haki kabla ya kushika dola
 
Hilo ni kweli kabisa.

Nimesikitika sana kuona Chadema ya Mzee Slaa imepotea. Siamini macho yangu Leo ukumbi w LAPF hakuna mwenye gwanda.

Gwanda ilikuwa alama ya ukamanda. Nasikitika Leo hakuna gwanda kwa kina Mbowe, Mdee n.k

Kweli Mamvi kaiua CDM.

Queen Esther

Chadema imeshauzwa. Kuna kila dalili kuwa mnunuzi wa Chadema anataka kuibadilisha iwe kikundi cha sanaa...
 
Mtatiro acha kuchochea vurugu Tanzania tambua kuwa amani ikivurugika utakuwa sehemu ya washitakiwa ICC The Hague.
Mbona wajitoa ufahamu? Yule aliewahi kuwa kiongozi Mkuu wa nchi alivyoropoka kwenye uzinduzi wa kampeni za ccm haikuwa uchochezi? CCM mmeshachoka kilichobaki ni sukuma twende wakimtafuta wakumtwika huo mzigo. Unamnyooshea Mtatiro kidole kwa lipi? Au ukweli kwenu mwiko?
 
Naomba kuungana na wana UKAWA wenzangu kwa kuishukuru Serikali yetu kwa kuendelea kutunadi.

Mambo wanayoyaleta muda huu wakitumia Mamlaka zake ni Kampeni TOSHA.

Mh. Lowassa, Kamanda wetu hata usipopiga KAMPENI kura yangu unayo.

Asanteni
1. Kizungumkuti Jangwani
2. Kampeni Hospitalini
3. Kutumia Chopa
4...

Naomba wana UKAWA tuendeleze mapambano
 
SIKU TANO ZA KAMPENI: YAFUATAYO YANAONESHA DHAHIRI KUWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZINASHIRIKIANA NA CCM KUJARIBU KUHARIBU UCHAGUZI HUU;


Na. Julius Mtatiro.


1. Kumzuia mgombea urais wa CHADEMA/UKAWA kuhudhuria msibani eti kwa sababu amesindikizwa na watu, kana kwamba watu walewale kwa idadi ileile wangekwenda wenyewe wangeleta madhara yoyote. Najiuliza tu, ingekuwaje mgombea na watu wale wangelazimisha kwenda msibani; JIBU: Mapambano na Polisi, mgombea kukamatwa na kufunguliwa kesi, wafuasi kujeruhiwa kwa risasi, kuuawa ama kukamatwa.


2. Kupiga Marufuku maandamano na mbwembwe za kuwasindikiza wagombea kurejesha fomu. Hili lilifanywa mara baada ya Magufuli na Lowassa kwenda kwa maandamano lakini yale ya Lowassa yakionekana kuwa na maelfu mengi ya watu zaidi kuliko ya magufuli. Lakini pamoja na marufuku hiyo majuzi nimejionea wafuasi wa CCM wakiandamana kutoka Manzese hadi Jangwani wakiwa na MASABURI, bila polisi kuwazuia.


3. Kuzuia mgombea wa UKAWA/CHADEMA kufanya ziara maalum za kushtukiza kuwatembelea wananchi wa kawaida. Hizi zinapigwa marufuku kwa mgombea huyu wakati wale wa CCM wakifanya watakavyo. Mfano ni Bi. Samia Suluhu alivyoonekana Moshi akiacha ratiba ya ziara na kutembelea raia mtaani bila kukatazwa na Polisi.


4. Kuzuia UKAWA kufanya mkutano wake wa uzinduzi Uwanja wa Taifa na hata UKAWA ilipoamua kufanyia mkutano huo katika viwanja wa JANGWANI umezuiwa na Manispaa ya Ilala nadhani kwa shinikizo la CCM chini ya sababu dhaifu sana kwamba kuna watu wameshaukodi, Ni halmshauri ipi hivi sasa ambayo ina-PRIORITIZE shughuli zingine kwenye viwanja vikubwa wakati vyama vya siasa viko kwenye uchaguzi mkuu jambo ambalo ni kipaumbele cha taifa kwa sasa?


5. CCM kufanya mkutano wake wa uzinduzi hadi saa 12.38 jioni tena mbele ya Mkuu wa nchi na viongozi wote wa serikali wakati wanajua fika kuwa sheria inawataka kufunga mkutano saa 12.00 jioni. Kwamba CCM na inavionesha vyama vingine kuwa iko juu ya sheria na kwamba wengine wakiiga watajiju. Na baada ya kupitisha muda huo CCM inamshinikiza Mkurugenzi wa manispaa ya ILALA aandike barua NEC kuijulisha kuwa ni yeye ndiye alielekeza mkutano uendelee hadi muda huo (very illogical reason).


6. Rais mstaafu wa awamu ya 3 Benjamin William Mkapa kusimama hadharani na kuwatukana wapinzani kuwa ni "MALOFA na WAPUMBAFU". Mpumbavu ni neno kali na lina maana ya "juha", "zuzu", "mtu asiyejielewa", "-----", "----", n.k. Wakati Mkapa akitukana hivyo hadharani na kuachwa juu ya Sheria, Lawrence Masha ambaye ni mwana UKAWA (hivi sasa) lakini zamani akiwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Tanzania, yeye amekamatwa na kuwekwa rumande na kunyimwa dhamana (inacheleweshwa kimakusudi) kwa "kosa" la kumtukana askari polisi (wengi kama sikosei) kwamba ni "washenzi", "wasio na shukrani na wasio na dini". Kwamba kwa tafsiri ya CCM na serikali yake pamoja na vyombo vinavyosimamia sheria (POLISI), neno "Upumbavu na Ulofa" siyo tusi lakini neno "Ushenzi na Kutokuwa na shukrani" ni tusi baya sana.


Hayo mambo sita niliyoyataja na mengine kadhaa ni dalili tosha kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaweza kuishia mahali pabaya. Hadi sasa sijaona CHOKOCHOKO kutoka upande wa UKAWA, hii ina maana kwamba hizi za CCM, VYOMBO VYA DOLA NA MAMLAKA ZA SERIKALI zikiendelea na zikawa zinahujumu kwa dhahiri maslahi ya UPINZANI na UKAWA, lolote lile linaweza kutokea.


Julius Sunday Mtatiro,
Dar Es Salaam.

- 7. Lowasa kukuwekea mgombea wake huko Segerea uliyetaka kupigana naye ngumi kugombea nafasi ya kuwakilisha UKAWA, hili mbona hujalisema mkuu?


Le Mutuz
 
Tatizo lenu UKAWA mnafikiria mambo ni rahisi tu kwamba mpite mnadanganya watu kuwa mnataka kuwaletea mabadiliko wakati hamuwezi halafu serikali iwaache tu mfanye mnavyotaka. Haiwezekani.

Kauli hizi zinaonyesha tuna safari ndefu kabla ya kufikia demokrasia ya kweli.
 
kuna usemi kwamba siku zote mti wenye matunda ndio urushiwa mawe. nina maana kuwa LOWASA ni mti wenye matunda na ndio maana serikali ya CCM inahangaika kumuwekea vigingi, kuna mifano iliyo wazi hapa,tukianzia kule moshi kwenye mazishi serikali ilitumia polisi kumzuia, ukija huku dar napo polisi wamempiga marufuku kutembea mitaani kuongea na watu,mara wakazuia uwanja wa jangwani asizindue kampeni zake. ila kwa kifupi LOWASA anatisha na ataendelea kuwa mti wa matunda
 
images
 
Back
Top Bottom