Siku Tanganyika na Zanzibar Tulipopigana Vita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku Tanganyika na Zanzibar Tulipopigana Vita

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JohnShao, Jun 4, 2012.

 1. J

  JohnShao Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku Tanganyika na Zanzibar Tulipopigana Vita

  Katika “Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha” (by Minael-Hosanna Mdundo, DUP 1999, pg 28-29), Sheikh Thabit anaelezea vita iliyotokea kati ya Tanganyika na Zanzibar mwaka 1914 wakati Thabit ana miaka 10. Anasema:

  “Kutokana na mikataba ile ya kuihami Zanzibar, ilikuwako meli moja ya vita jina lake Pegasus, iliyokuwa ikiranda baharini wakati wote kulinda visiwa hivi. Haikuondoka hata mara moja.

  Siku moja Jumapili,sikumbuki tarehe, ikaja meli ya Mjerumani kutoka Dar es Salaam, inaitwa Lord Minna. Meli hiyo ya Mjerumani ikapiga mizinga hapa Unguja. Mzinga mmoja ukaenda moja kwa moja mpaka katika meli ya Pegasus, na meli hiyo ikaanza kuzama. Kwa siku ile Pegasus ilikuwa katika matengenezo madogo ya kusafishwa. Meli hizo za zamani, Pegasus na hata Minna zilikuwa zinaendeshwa kwa nguvu za mvuke, unaopatikana kwa kuchochea kuni au makaa. Wakati huo sikuwa na habari ya ugomvi uliokuwako baina ya Waingereza na Wajerumani, lakini ni dhahiri kwamba ni matokeo ya uroho huo huo ninaoelezea. Nasikia kuna watu waliokwenda Dar es Salaam kuwanong'oneza Wajerumani kuwa Pegasus imo katika matengenezo, basi Minna ikaja usiku usiku na kukaa mwisho wa kisiwa mpaka alfajiri ndipo ikashambulia.

  Siku hiyo, kwa mshindo huo wa mizinga, watu walitoka mbio kukimbilia mashambani. Wengine pale mwanzo walidhani kuwa Pegasus inafanya mazoezi, wakakimbilia pwani kuangalia; walipofika wakaiona Pegasus inateketea, inazama, na watu wanakufa! Basi wakataharuki, na kila mmoja akenda kujificha mahali alipoona pana usalama.

  Baada ya siku tatu za hekaheka Waingereza wakaagiza manowari (man-of-war) nyingine kutoka India inayoitwa SS Charlton, ikaenda kupiga Dar es Salaam. Charlton ikafanikiwa kuipiga Minna, meli ya Wajerumani, na kuivunja vipande vipande; likavunjwa hata gati la kupandishia meli. Baadaye Charlton ikarejea Zanzibar. Mizinga iliyokuwa inapigwa Dar es Salaam ikasikika mpaka Zanzibar, na kwa vishindo hivyo wananchi wa Visiwani humu wakatambua kuwa vita ndivyo hivyo vimefika. Wakati huo askari wa polisi na wa K.A.R. walikuwa wachache sana.

  Ikawa vita ndiyo vimekwishaanza kati ya Waingereza na Wajerumani. Ikabidi sasa serikali ya Sultani kufanya utaratibu wa kuwapata raia kwenda vitani "kusaidia" katika ulinzi unaosimamiwa na Waingereza. Hakuwako raia aliyependa kujiandikisha kwenda vitani; wao hawakuwa na sababu ya kupigana vita, na tena kila mtu alikuwa na hofu kwamba akienda vitani atakufa, hana nafasi ya kurudi hai.

  Basi mbinu zikafanywa za kuwakamata raia kwenda vitani; na waliokamatwa wakatokea kuwa Wahadimu tu, yaani Waafrika. Waarabu, Wahindi na Wangazija hawakukamatwa. Basi Waafrika wengi wakapata sababu nzuri ya kuhamia kabisa mashambani, wakauhama mji kwa kuogopa kupelekwa vitani.

  Baada ya kuwakosa Wahadimu kwa kipindi, Waingereza wakabuni hila nyingine ya kupiga bendi, matarumbeta na ngoma za kienyeji. Bendi ilipigwa na askari wa K.A.R. ambao wengi wao walikuwa wanatoka Kenya; Wakamba, Wajaluo, na kadhalika; watu wa Zanzibar wakawaita askari hao "Mburumburu” (sauti ya matarumbeta). Basi bendi ilipopigwa vijana walifuatia kwa mamia mpaka pwani Malindi. Huko ikawa imeandaliwa meli maalum, na vijana walipofika huko wakachukuliwa kwa urahisi na kupelekwa Tanganyika kujiunga na vita.”

  - End -
   
 2. H

  Hurricane Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hapo kwenye red nimeipendaje!!
   
 3. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,314
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Hii ni sawa na ile hadithi ya mpiga filimbi wa hamellin
   
 4. S

  SuperNgekewa Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ahsante kwa JohnShao kwa kutukumbusha kuwa Tanganyika na Zanzibar zilikuweko kabla ya 1961 au 1964. In fact kuzaliwa kwa Tanganyika ilikuwa tarehe 27 May 1885 wakati Karl Peters alipoteuliwa Administrator wa kwanza kabisa wa Tanganyika (wakati huo German East Africa). Karl Peters aliharibu na baada ya muda si mrefu nafasi yake ikachukuliwa na Von Wissman. Zanzibar nayo mwaka 1890 baada ya "kutumbukia kwa Waingereza" kama anavyosema Sheikh Thabit Kombo. Kitu muhimu ni kwamba hizi ndizo tarehe ambazo nchi imepata mipaka inayoeleweka pamoja na serikali kuu.

  Wanaotupa fikra kwamba hatukuweko kabla ya 1961 au 1964 wanatupotosha na wanaodai kuwa tulikuwa nchi kabla ya miaka hiyo ya 1885 kwa kuwa tu ardhi ilikuweko na watu walikuweko ni uzushi wa wasomi wanaofikiri kijuu juu tu. Nilimsikia profesa mmoja akidai kuwa Afrika ilikuwa imeungana kabla ya 1884 na mwaka huo ndiyo tuligawanywa! Jamani, kwa mtaji huo tutafika?
   
Loading...