Siku si nyingi watu kwa asilimia kubwa watahamia kwenye mitandao ya kijamii kama vyanzo vya habari vya kuaminika

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
651
853
Nimefungua kurasa mmoja wa chombo cha habari fulani, kinaarifu kuwa...'wakazi wa Dar Es Salaam wamepongeza utendaji wa miaka kadhaa ya Mkuu'. Maoni ya wafuatiliaji wengi kwa asilimia kama 70 au zaidi hivi, yamepingana na statement hiyo. Chombo hicho na vinginevyo (majina kapuni) kwa siku za hivi karibuni, vimebadilisha muelekeo kabisa kwa kuripoti aina fulani za habari ambazo ukiziangalia kwa undani utagundia ni za kinafiki.

Ninachokiona kutokana na observation yangu kupitia maoni ya wafuatiliaji wale, ni kwamba, muda si mrefu, watu wataacha kufuatilia vyombo vya habari vya ndani na badala yake watakuwa wakifuatilia vyombo vya habari vya nje. Ama, watu watakuwa wanatumia mitandao ya kijamii kujipatia habari za uhakika ili kuepuka kulishwa habari zilizo na mapungufu. Mfano, tukio lililotokea kule Ukonga, mimi kwa mara ya kwanza nililipata kupitia jamiiforums na badaye youtube wakati vyombo vya habari vikiwa vimekaa kimya.

Aftermath:
Kama watu watabadilisha njia ya kujipatia habari za kuaminika, maana yake ni kwamba, hata matangazo kwa vyombo vya habari toka kwa wafanyabiashara yatapungua hivyo mapato kupungua.

Ushauri: Vyombo vya habari, rudini kwenye mstari, mmekuwa mkilalamikiwa siku za hivi karibuni aidha kuripoti taarifa za upande fulani, ama kushindwa kabisa kuripoti taarifa muhimu. Msipofanya hivyo, na watu wakabadilisha kweli kweli namna ya kufuatilia ama kujipatia habari kupitia mitandao ya kijamii, maana yake hakutakuwa na matangazo yanayofanya muenddeshe media house zenu, na msipopata matangazo maana yake ndiyo mwanzo wa kufilisika kwa sababu hamtakuwa na uwezo wa kuwalipa wafanyakazi na kulipa kodi. Kumbukeni kuna njia nyingi mbadala za kufanya matangazo dunia ya leo, shauri yenu; angalieni isije ikabaki story tu, kwamba niliwahi kumiliki chombo cha habari kikafa na usijue ni kwa nini kilikufa.
 
hilo limeshaanza kitambo tu....
mie nishaachana kabisa na taarifa ya habari za tv na redio, mitandao peke yake inatosha kupata habari, manake nyingine haziandikwi, cha ajabu sasa mpaka sisi wa vijijini tuna smartphone na tunapata kila kitu, yaani kifika taarifa ya habari ya channel yoyote nahamia kwenye movies,
 
Ha ha h ha ha ha ha...kuna mtu alinambia kuwa, TV kwake ipo tu ili watoto wajue kuwa kuna kitu kinaitwa TV na kinafanyaje kazi, ila kiukweli hakuna mwenye time na TV hasa linapokuja suala la habari. Ananambia, yeye kwake ukienda, unaweza ukadhani ni mtu toka South Africa, maana ni full DSTV na channel zilizotawala kwake ni SABC, Supersport, M-Net kwenye habari ni BBC, Al-Jazeera, CNN etc.
 
haha

hahaha
 
Mie huwa nikisoma JF wala sihitaji tena kusoma gazeti labda nisome tu zile kurasa za WANAOTAFUTA MARAFIKI WA KALAMU hahahaha
 
mie nishaachana kabisa na taarifa ya habari za tv na redio, mitandao peke yake inatosha kupata habari, manake nyingine haziandikwi, cha ajabu sasa mpaka sisi wa vijijini tuna smartphone na tunapata kila kitu, yaani kifika taarifa ya habari ya channel yoyote nahamia kwenye movies,
upo sahihi kabisa.....
 
Back
Top Bottom