Siku sheria zote za nchi hii zikifuatwa zote 100%, Kutakuwa na kilio kikuu cha mabadiliko ya sheria na sio Katiba tena

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
Kilio kikubwa sasa hasa kwa wapinzani na wananchi wengi ni Mabadiliko ya katiba.
Ila sheria tulizojiwekea tukisema kesho asubuhi zifuatwe zote Bila kukwepwa 100% itakuwa ni kilio Kila kona na kila sekta.

Mfano moja tu ya kodi, Kila mtu akibanwa kulipa kodi popote alipo na kila njia ya kukwepa ikazibwa 100% kutakuwa na kilio Kila kona. Sababu sio hiyo kodi bali wahusika hawakuwahi kudhani mfano Kuna siku hayo mambo yatakuwa halisi.

Lakini kilio hicho kikikomaa na kuvimilika kutakuwa na Maendeleo makubwa kiuchumi kuliko siku zote tangu kuwepo kwa Tanzania.

Najiuliza Mwanasiasa atamteteaje
Mwananchi aliyejenga kwenye hifadhi ya barabara...
Atamteteaje mpangishaji anaetaka kukwepa kulipa kodi ya pesa anayopokea kutoka kwa mpangaji wake.
ATAMTETEAJE mwenye shamba pori
Atamteteaje mmachinga asiyelipa kodi kisa anahamahanama na hatulii sehemu moja


....

Nawaza...
 
Back
Top Bottom