Siku saba za mrema

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Salaam WanaJF,

Nimejikuta nikiukumbuka utaratibu wa aliyekuwa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani ya nchi ndugu yetu Mrema.
Ukiwa unatoka Ubungo kuja Fire pembeni ya barabara kuna mfereji, huu mfereji ni mchafu mwanzo mwisho, tena kuna maeneo una harufu kali na kwengine wakazi wanatupa taka humo.
Hii barabara ni ya nani, Jiji,TANROAD au Serikali za mitaa? hali ni mbaya uchafu inasikitisha.Usafi huu ni wajibu wa nani wana JF hebu tubadilishane mawazo.
Ndio maana namkumbuka Mrema, angetoa siku saba tu na mambo yote yangekuwa safi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom