Siku Rais Samia akigundua wanawake ndio wanaompinga zaidi, atawapigia magoti wanaume

Kuna jambo moja ambalo Rais Samia huenda bado hajaligundua ni kuhusu nafasi yake ya kisiasa kuwa imetengenezwa na nguvu ya siasa za vyama kuwatumia wanawake kama mtaji wa kisiasa ili kupata madaraka au kuendelea kuwa madarakani na kamwe sio kuwapa wanawake madaraka ili wawatale wanaume.

Pili mama Samia asahau kabisa kuwa wanawake wa Tanzania wanaweza kujipanga kumpa madaraka au kulinda madaraka yake, kwa sababu ya tabia za kisiasa za wanawake wa Tanzania walivyo. Kwa mfano.

1. Wanawake wengi wa Tanzania husukumwa na wanaume kimaamuzi.

2. Wanawake wengi wa Tanzania wanaamini kufanikiwa kwao kimaisha kunategemea kuwezeshwa na wanaume.

3. Wanawake wengi wa Tanzania hawapendi kuongozwa na mwanamke mwenzao.

4. Wanawake wengi wa Tanzania wanaamini adui mkubwa wa mwanamke kwenye maisha ni mwanamke mwenzake.

5. Wanawake wengi wa Tanzania wanaamini uanamke mbele ya wanaume ni ishara ya udhaifu na sio ujasiri au ufahari.

Mwisho kabisa ninapenda kuandika kuwa, Siku Rais Samia akigundua kuwa mateso ya kimaisha wanayopata wanawake yanaletwa na mwenendo mbovu wa seikali yake, hakika ataogopa kuwaambia wanawake wamuunge mkono kwenye mbio zake za urais 2025.
Huyo mama ni kipusa awezi kuona mbali
 
Si kweli bana acheni kumpinga Rais kisa jinsia yake na kusingizia eti tuna amini wanaume kimaamuzi si kweli.
Samia akosolewe kiuomgozi na sio kumshambulia mara dhaifu kisa jinsia yake.
Lakini yeye ndo ameweka kipaumbele hayo mambo ya kijinsia kuliko hata changamoto zinazoikabili nchi yetu kwa Sasa, Mimi nilivyowaelewa watanzania hawajali Rais awe mwanamke au mwanaume, watanzania wanataka Rais atatue kero zao za ajira, uchumi na huduma za jamii.

Kwa Sasa mama alitakiwa ajikite katika utendaji zaidi ili watu waone matokeo wawe na Imani nae, hayo maswala ya kijinsia awaachie wamaharakati na taasisi za kijamii zinazohusika. Yeye ni Rais wa jinsia zote hatakiwi kuchagua upande.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Ovyo tu,mzee cheyo nimemsikia anasema wanaume tumezaliwq na wanawake zikapigwa kelele nyingi na vigelele kama vile walikuwa hawajui

Kwa mujibu wa huyo mzee,hiki ndicho kigezo cha kwamba wanawake wana uwezo mkubwa wa kuongoza nchi, huu ni ubahuzi wa kijinsia huyu bibi analeta
Hangaya anazingua sana
 
Uliichosema ni kweli mkuu,yaani hapa kitaa kuna kakikundi ka wanawake ni CCM kindaki ndaki wakiongozwa na mama yangu mdogo ndio hua wapiga vigelegele na wawakilishi wa mtaaa kwenye mikutano
Duuuu huwezi amini Hawamkubali Madame wanamkandia balaa,wanasema anajua kulembua tu wakati mahitaji madogo madogo kama mafuta ya kula yapo bei juu?

Hua nawakejeli kwa kuwaimbia CCM Mbele kwa mbele nikiona wana dis

Juzi kati wakakili kumbe bungeni bila wapinzani kuwepo kuna wagonga meza wananapitisha upumbavu bila kupinga,naona wanajipanga sasa et Tundu Lisu akirudi 2025 kugombea watamuunga mkono kwa kishindo

Naishia kucheka tu nakusema
Hiiiiii bha ghoshaaaaaaaa
Ama kweli wanawake hawapendani!
So far TL is the best Candidate ukiondoa magaidi wa ccm. Anashinda mchana kweupe.
 
Kuna jambo moja ambalo Rais Samia huenda bado hajaligundua ni kuhusu nafasi yake ya kisiasa kuwa imetengenezwa na nguvu ya siasa za vyama kuwatumia wanawake kama mtaji wa kisiasa ili kupata madaraka au kuendelea kuwa madarakani na kamwe sio kuwapa wanawake madaraka ili wawatale wanaume.

Pili mama Samia asahau kabisa kuwa wanawake wa Tanzania wanaweza kujipanga kumpa madaraka au kulinda madaraka yake, kwa sababu ya tabia za kisiasa za wanawake wa Tanzania walivyo. Kwa mfano.

1. Wanawake wengi wa Tanzania husukumwa na wanaume kimaamuzi.

2. Wanawake wengi wa Tanzania wanaamini kufanikiwa kwao kimaisha kunategemea kuwezeshwa na wanaume.

3. Wanawake wengi wa Tanzania hawapendi kuongozwa na mwanamke mwenzao.

4. Wanawake wengi wa Tanzania wanaamini adui mkubwa wa mwanamke kwenye maisha ni mwanamke mwenzake.

5. Wanawake wengi wa Tanzania wanaamini uanamke mbele ya wanaume ni ishara ya udhaifu na sio ujasiri au ufahari.

Mwisho kabisa ninapenda kuandika kuwa, Siku Rais Samia akigundua kuwa mateso ya kimaisha wanayopata wanawake yanaletwa na mwenendo mbovu wa seikali yake, hakika ataogopa kuwaambia wanawake wamuunge mkono kwenye mbio zake za urais 2025.
Hata mama mwenyewe anaaminj hivyo hivyo. Yeye mwenyewe anajua kuwa waliomwezesha kuwa ni mgombea mwenza ni wanaume!!
 
Udibidhe wewe uliza wanawake wakioko jirani t'yaki utapata majibu mwenyewe
Ulihoji majirani wangapi? ukilinganisha na wanawake walio nchi nzima? Je sample size yako ni halali kweli? Tuache kutoa hoja zisizo na mashiko bado nasema ni sweeping statement. Tujihadhari na maelezo kama haya.
 
Sasa hivi,madaraka yanaamliwa na ukubwa wa K,yu wapi miss Natafuta aliyedai K yake ina uzito wa kilo kumi?
 
Nijuavyo mimi ni kwamba, mpaka sasa, kama tungefanya uchaguzi mkuu leo hii, mambo mawili yangetokea:

(1)Watu wengi wasingekwenda kupiga kura.

(2) Wale watakaokwenda kupiga kura, wangepiga kura kwa hasira na kati ya 75% na 89% wangechagua viongozi wa UPINZANI.

Kama hali itakuwa hivi au duni zaidi ya hii mpaka 2025, haya mambo mawili niliyoyataja hapo juu yatatimia hakika.

Kwa anayebisha leo, atunze kumbu kumbu vizuri hadi mwaka huo.
Kwani tume imekuwa huru? Katiba je,imebadilika?
 
Wanawake wa kwenye vikao na posho, naamini watampa kura, ila wengi wasiohudhuria vikao jaribu kuwasikiliza utaogopa, ila kwenye kushangilia wanawake wote kitu kimoja, ila kwenye box tofauti, hatende haki tu itasaidia!
 
Si kweli bana acheni kumpinga Rais kisa jinsia yake na kusingizia eti tuna amini wanaume kimaamuzi si kweli.
Samia akosolewe kiuomgozi na sio kumshambulia mara dhaifu kisa jinsia yake.
Sasa huyo mama anasahau yeye nirais muda wote anaongelew wanawake utazan yuko kwenye harakat zafeminism
 
46 Reactions
Reply
Back
Top Bottom