Siku njema kama alivyomaanisha Ken Walibora kwenye riwaya ya ''Siku Njema''

Cenetor

Member
Oct 1, 2014
12
2
"SIKU NJEMA" hii ni tittle ya riwaya ya kiswahili ya Ken Walibora.Kwake SIKU NJEMA ni ile ambayo itakuwa:
1.Hakuna vita,bunduki,mizinga wala mabomu maana hakuna adui,wavamizi wala wezi.
2.Hakuna vifo wala magonjwa.
3.Kutakuwa na maendeleo.
NB:Kwake,maendeleo ni.
1.Kutokwepo kwa magereza maana hamna wa kwenda gerezani.Watu wote ni raia wema.
2.kuwa na barabara nzuri,shule na mahospitali ya kisasa......N.K
[HASHTAG]#KWANGU MIMI TOFAUTI NA KEN WALIBORA,NATAMANI[/HASHTAG] KUIONA SIKU NJEMA KWA NCHI YANGU:
Kwangu "SIKU NJEMA" ni siku ambayo nitaona yafutayo yakitokea Tanzania yetu:
1.Kuna wanasiasa wanaotanguliza "state interests" badala ya "Party interets"
2.Kuna viongozi ambao ni "policy and agenda oriented" badala ya "Political sycophants"
3.Kuna "proffesional journalists,newspaper editors and writters" badala ya "proffesional ghossipers and rumour mongers".
4.Kuna vyombo vya habari ambavyo vinatayarisha vipindi Maalum vya elimu ya ujasiliamali,Biashara,Elimu,Afya n.k,na kuvipa majina yenye akili kama "KIJANA NA BIASHARA"."KUKU NI MALI".SUNGURA NI PESA"."KIJANA NA MBOGA MBOGA" "ELIMU NI MWANGA" "AFYA NI MTAJI" . Au hata "SHIVIKUDU" yani SHIRIKA LA VIJANA WAFUGA KUKU DUNIANI" Badala ya vipindi nyenye majina ya ajabu ajabu kama "SHILAWADU" yaani SHIRIKA LA WAMBEA DUNIANI.
Kwanini watanzania ndio tuanzishe mashirika ya umbea duniani wakati wachina wanaanzisha mashirika ya simu,usafiri,viwanda n.k duniani??? Wabrazil wanaanzisha mashirika vya "football academies" wakenya wanaazisha mashirika ya walima miwa!!
NATAMANI KUIONA SIKU NJEMA IKICHA TANZANIA!
MUNGU UBARIKI TANZANIA! MUNGU IBARIKI AFRIKA!
 
Back
Top Bottom