Siku nitakapokufa

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
14,176
22,577
SIKU NITAKAPOKUFA ..01
AUTHOR: NEXT LEVEL.

Katika kila maisha ya binadamu kuna sehemu tunapitia na kukutana na majaribu ya kila aina mbalimbali, lakini kuna kuzaliwa kuishi na kufa, lakini Mimi siku nitakayokufa ...!siku nitakayokufa!..

Asubuhi na mapema jogoo anawika kuashiria kuwa watu waamke na kuanza shughuli zao za utafutaji, japo waliokereka na taarifa ya jogoo huyo kuwika kuashiria kuwa ni asubuhi kumekucha.

Mmojawapo alikuwa ni kijana mdogo Mussa matalu, alikuwa ni kijana wa miaka 16 tu, damu bado changa, mwili uliojengeka vizuri kutokana na kazi za suruba nyumbani kwao kwani yeye pekee ndiyo alikuwa kijana pekee wa kiume hapo kwao. "Wee mtoto utaendelea kulala mpaka saa ngapi?"

Huyo alikuwa ni baba wa damu wa mussa aliyejulikana kama mzee matalu, alikuwa mkali asiyependa mzaha kabisa wala utani wa kipuuzi.

Mussa aliamka harakaharaka kwani alielewa akiendelea kulala atachelewa shule na baba yake pia atamuadhibu.. Haraka akajiandaa na kutoka katika kibanda chake haraka kuelekea shule iliyojulikana kama WELLA SECONDARY.. Ilikuwa ni shule pekee kijijini hapo .
Oyaa mussa..!

Alikuwa na rafiki ake wa damu kabisa aliyejulikana kama Emanuel chigoni mwenyewe alijiita Emma uzo..Oya damu yangu nimepita kwenu bi mkubwa wako kasema umeshatangulia skuli nikaona nikufukuzie ..!

Mussa: aah we kila siku unachelewaa?
Imma uzo: aah mwanangu nilisahau kukuchana Jana si nilikuwa na mtoto Lydia?
Mussa: acha uzushi mtu mwenyewe utamuwezea wapi wewe?Ukweli ni kuwa mussa alipinga kwa nje lakini moyoni aliumia sana kwani hakuwahi kuwa na mpenzi tofauti na wanafunzi wenzake kama alivyo imma uzo angefanyaje na anawaogopa?

Alichoamua ni kubadilisha story maana imma hakuchelewa kuanza kumkandia kwamba kwanini hana demu..(mpenzi)

Well wanafika shuleni vijana hao wawili wa kidato cha NNE shuleni hapo . Baada ya mambo mengine kama usafi wanaenda mstarini (paredi) na kumkuta mwalimu mkuu amefura kwa hasira mithili ya chura mwenye mimba ..!

Kikawaida akiwa amekasirika basi huwa kunaKikawaida akiwa amekasirika basi huwa kuna jambo kubwa limemkasirisha ...alikuwa ni mwalimu DANIEL SHENDU.. Mkali mithili ya mbogo, ngozi yake nyeusi ya kung'aa, miwani yake ya macho aliyoining'iniza machoni pake ..hakuwa na utani hata kidogo.

Vijana kuna baadhi ya wanafunzi wanafanya shule kama ya wazazi wao, kwamba wanatenda wanavyojiskia "alianza mwalimu huyo"
Sasa basi ili kuonyesha mfano na onyo kwa wengine lazima sheria ifuatwe.

Erick mazinde..!, noel machemba.! Piteni mbele upesi.
 
Yaaani sijasoma story nimeona hiyo shule WELLA sekondari... Nilipita Juzi Kati TU pale...Kikuyu
 
Hadithi inaanza na kuisha kabla haijafika kati
 
SIKU NITAKAPOKUFA ...02
AUTHOR NEXT LEVEL..
Kila mtu alipigwa na butwaa vijana hao wawili wamefanya nini kwani walisifika kwa utukutu uliopindukia ...nao pia walibaki na kitete na hofu kubwa kwani walijua kitakachowapata.!
"Nyinyi wapumbavu aliyewaambia muandike barua ya kumtongoza mwalimu Imelda ni nani? Mmekua sana si ndio?"
Alifoka mwalimu huyo kwa hasira , hali iliyofanya wanafunzi wengine wapigwe na butwaa..! Haikuchukua muda wanafunzi hao watukutu hao wawili walipelekwa ofisini kwa hatua Kali zaidi na waliobaki kurusuhusiwa kwenda madarasani.

Dah mwanangu yule ticha Imelda me mwenyewe nilikuwa namtamani sana yaani ana bonge la takoo...alizungumza kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la amosi
Darasani kwa kina mussa akiwa amekaa akisubiri mwalimu aingie kuanza kufundisha ghafla bin vuu anaingia mwalimu wa academic aliyejulikana kama MLELWA..akiwa sambamba na binti mgeni shuleni hapo ..
" jamani huyu ni mgeni shuleni hapa atakuwa darasa lenu hapa mkaribisheni msaidieni akiwa na shida ...(kisha anatoka zake)
Watu walishangaa sana kumuona binti huyo mrembo darasani hapo, alikuwa mrefu,shingo ya wastani, maziwa kiasi kifuani ,wahuni waliita saa sita, shepu ya wastani ...
Haraka akaoneshwa siti ya kukaa na monta ..
Mussa aliduwaa kwani licha ya kutowahi kuwa na mpenzi lakini pia hakuwa kuona msichana mrembo kama huyo hilo alikiri.
Angefanyaje sasa kama sio kufunga domo lake kama bakuli la njegere?
Hatimaye muda wa mapumziko umefika na kwakuwa hakuwa na pesa ya chai ilibidi akae chini ya mti mkubwa akiwaza na kuwazua .
Ghafla akastuka akiguswa begani kwa nyuma..
Alishtuka sana, na kugeuka nyuma kisha kukutana na binti mrembo yule mgeni darasani kwao.
"Samahani kantini ni wapi? " aliuliza binti huyo
"Aah ni Kule mbele twende nikupeleke" alijibu mussa kwa pupa nyingi kutokana na mshtuko.
Hao wakaenda zao mpka kantini,msichana yule alipoona mussa ameishia nje ikabidi amwite " njoo unywe chai mbona umeishia nje ?"
Mussa alishangaa na kupigwa butwaa kwa wakati mmoja ,kwani hakuwahi kunywa chai kantini hapo, hakuwa na pesa hata kidogo ,alinuka shida sana na hata kwao wazazi hawakuwa na uwezo mkubwa kama familia zingine walimtegemea yeye asome ili aje kuwakomboa kwenye umaskini mkubwa ulioziba future ya maisha yao.
Mara kwa Mara wamekuwa wakilala njaa kwani ni kawaida sana umaskini waliuzoea.
Kwa mussa kupata chai tena ya kununuliwa kwake nilikuwa ni sawa na kukataa kwenda mbinguni,
 
SIKU NITAKAPOKUFA.. 03
AUTHOR NEXT LEVEL
haraka alinawa mikono na kuletewa chapati 2, alizifakamia kwa pupa sana..njaa ilimkaba..baada ya hapo wakatoka wote wawili na kurudi kwenye ule mti wa awali alipokuwa mussa ..
"Naitwa Maureen niliskia unaitwa mussa?"alijitambulisha binti huyo.
" aah ndio naitwa mussa matalu "
Maureen: baba yangu ni daktari hapa kijijini tumehamia majuzi tu ndo akanileta shuleni hapa..
Kwa mussa aliona hata aibu kutaja kazi ya wazazi wake ,walikuwa ni wakulima tu wanaotegemea mvua za msimu ,kupata na kukosa. Hilo halikumzuia Maureen kumzoea mussa akawa rafiki yake pekee shuleni hapo .
Mussa akaheshimika na marafiki,akakubalika zaidi na zaidi kutoka kwa waliomdharau.

Ingawa Maureen alitokea kumpenda sana mussa ,lakini angeanzaje kumwambia? Ikiwa yeye mussa haoneshi hata dalili za kumpenda? Aandike barua? atume rafiki zake? Aliamua kukaa na kusubiri matokeo mwishoni huenda mussa akamfungukia ,wazungu wanasema let the feeling speaks..!
Siku zilienda na Maureen na mussa wakawa wameanza kutembeleana makwao .
Walipanga kuonana jioni yake mtoni maeneo ya mkalama ..ilikuwa sehemu pekee ya utulivu ambayo ingewapa amani ya moyo.
Walikutana wakakaa ,walichezea maji, walirushiana vya kutosha sana lakini katikati yao kulikuwa na hisia zao zikiogopa kukutana na kutengeneza kitu ,kutengeneza upendo.
"Hivi mussa shuleni una mpenzi?"
Mussa alishtuka sana kuskia kauli hiyo kutoka kwa Maureen hakutegemea kabisa.
Alibaki kimya hakujibu kitu..!
Waliongea mengi muda sio rafiki jioni ilifika na wakaanza kuondoka taratibu kabisa ..
Hatimaye waliagana lakini ghafla Maureen alimkumbatia mussa kama ishara ya kumuaga .alihisi kupigwa shoti mwilini..hakuwahi kukumbatiwa na msichana yeyote maishani mwake.
Ilikuwa Mara ya kwanza .alibaki kaduwaa mpaka msichana huyo alipopotea usoni mwake. Usiku hakulala, alibaki akiwaza na kukumbuka feeling ile pale alipokumbatiwa .hisia za upendo zilianza kuchanua moyoni mwake ,taratiiiibu...

Waswahili walisema kila tamu na chungu yake
 
SIKU NITAKAPOKUFA.. 04
AUTHOR NEXT LEVEL..

Kwa mussa kwake alikuwa ameshampenda Maureen vivo hivyo kwa Maureen alikwishachagua mussa awe wake .hakujali maneno ya wenzie kuwa mussa ni maskini mchafu, namengine mengi .kilichomsaidia mussa ni uwezo wake mkubwa darasani hali iliyopelekea kukubalika na wengi .
Kama mjuavyo hisia za watu wawili hazizunguki bure.uvumi ulisambaa sana na kufikia kuenea shuleni na mtaani kuwa mtoto wa mkulima mussa anatoka na binti wa daktari wa kijiji bwana Rwegasira.
Na baada tu kuwa wapenzi hawakuanza kujificha kama mwanzo.
Hilo liliwakera wanafunzi wakware waliokuwa wanamfukuzia Maureen ,kwani waliona kama mussa ndo kawazibia ,mmojawapo akiwa ni Christopher ama mwenyewe alijiita tofa.
Alikuwa ni kijana mtukutu, mkorofi mwenye kupenda Shari muda wote shuleni .
Macho mekundu mithili ya nyanya ,

Aliwaza sana hatimaye akaamua kupanga kitu ili tu kumkomesha mussa kwani yeye akikataliwa Mara nyingi sababu ya uvutaji mkubwa wa bangi ..alikasirika sanaa
Alirudi nyumbani akiwaza na kuwazua..

Itaendelea
 
SIKU NITAKAPOKUFA.. 05
AUTHOR NEXT LEVEL..

Mwalimu Michael lugolei akiwa ofisini siku hiyo alikuwa na kazi nyingi, hali iliyomfanya achelewe kutoka shuleni tofauti na wengine .
Ilipotimu saa 11 jioni aliamua kutoka shuleni na kurejea kwake .
Na shuleni hapo huwa kunakuwa na ratiba ya michezo siku ya ijumaa
Hivyo siku hiyo kulikuwa na mechi kati ya form 4A na form 4b ..
Hiyo ilikuwa ni fursa tosha kwa Tofa kulipiza aliyoyapanga kwani alikuwa form 4A huku mussa akiwa form 4b

Uwanja ulijaa wanafunzi wakipiga kelele za kila aina ilimradi kuwe na furaha .
Mpira ulipoanza tu dakika 38 mbele mussa alipokea pasi ndefu kutoka kwa kiungo namba 6 Ernest ama mwenyewe alijiita Pele.
Mussa anakimbia na mpira spidi Kali akitokea pembeni .huku mashabiki wakilitaja jina lake mussa! Mussa! Mussa! Poor mussa hakujua kitakachomkuta
Akiwa mita chache tu na goli ghafla tofa anatokea pembeni spidi na kumkwatua mussa kwa nyuma ..bahati ilikuwa kwake kwani aliruka juu na kukwepa haraka ,akafumua shuti Kali lililotinga wavuni ,
Hali iliyofanya mashabiki kuingia uwanjani kwa furaha kubwa hasa akiwa mpenzie Maureen na kwenda kumkumbatia mussa kitu. Kilichozidi kumpa hasira zaidi tofa.
Hakuridhika alisubiri mechi iishe.

Mussa akiwa njiani baada ya kutoka kumsindikiza kipenzi chake Maureen. Ghafla njiani anakutana na kundi la watu 6 waliovaa vinyago usoni ..
"Eeh we boya tulia hivyo tumekutafuta sana wewe"
Alishtuka lakini akajiamini.alizidi kuwafuata
 
SIKU NITAKAPOKUFA 06
AUTHOR NEXT LEVEL

Mussa akiwa katikati ya watu wale na akijua labda huenda wamemfananisha .ghafla akastuka wamemzingira pah! Ilikuwa ni fimbo matata pigo lililopigwa na kijana mmojawapo wa kundi la kina stofa na kumpata mussa mgongoni.! Alichanganyikiwa na kushikwa na uoga kwa maumivu makali ..
Alichangiwa wa kupiga teke alipiga, wa kupiga ngumi alipiga wa kuchana na wembe alimchana..dakika chache tu alikuwa sio mussa tena kwani uso wake kuharibiwa vibaya sanaa..
"Nyie vijana ondokeni hapo mnafanya nini"?
Alikuwa ni mwalimu lugolei akiwa safarini kutokea shule kwenda nyumbani kwake ..wanafunzi wale mabaradhuli waliokosa staha na utu wakiongoza na stofa walikimbilia vichakani huku wakimuacha mussa chini hoi asijue cha kufanya zaidi ya kutoa kilio ,mwilini alijaa damu, uso wake uliopendwa sana na kuitwa handsome na mpenziwe Maureen sasa umekwisha haribika mithili ya mwizi aliekwiba mitaa ya chang'ombe ama Kikuyu.
Mwalimu lugolei alimtambua kuwa huyo ni mussa ,alimuonea huruma sana na kubigwa na butwaa kwa wakati mmoja.haraka sana alimbeba na kumpakia kwenye pikioiki yake na kumwahisha zahanati ya kijiji kwa iliyojulikana kama kwa dk motto.
Hospital pale watu walishangaa na kubigwa butwaa jinsi mgonjwa yule (mussa) alivyoharibiwa mwili kwa kipigo.! Aliachwa hapo hospital na mwalimu lugolei kisha akaanza safari kwenda kwa wazazi wa mussa kutoa taarifa haraka kwani ilitakiwa na lazima.

Mama mussa ama Juliana akiwa hana hili wala lile miguu yake kaitandaza chini akimenya dagaa wake kama kitoweo kwa ajili ya jioni, akijiimbia wimbo wa taarab kutoka kwa mwanamama siti bint saad uliojulikana kama "njiwa". Anashangaa ujio wa mwalimu lugolei hapo nyumbani tena jioni mmh kuna nin?
" mama shikamoo" alianza kusalimia mwalimu.
"Marahaba baba angu" za kazi? Mbona ujio wa jioni hii mussa kafanyaje huyu mtoto?"

"Aah hapana mama mussa kapata matatizo kidogo amelazwa hospitali"

"Ooh mungu wangu mwanangu amekuwaje acha niengeshee mlango baba twende"

Itaendelea
 
SIKU NITAKAPOKUFA. 07
AUTHOR NEXT LEVEL
******************

Mwalimu lugolei alikuwa ni mwalimu msomi hivyo alijjua iwapo ataleta habari kwa kushtua ingeleta matatizo zaidi ,hivyo hakusema kama mussa kapigwa vibaya sana..
Haaao wakaondokaa.
***********
Akiwa ametoka ofisini kwake hospitali bwana Rwegasira aliwaza mengi kichwani ..aliwaza akawazua, nadhani hata ungekuwa wewe msomaji ungewaza ,ungewazua.
Bwana Rwegasira ni mmoja kati ya watu waliochukizwa na uhusiano ulioendelea baina ya bintiye Maureen na kijana yule aliemuona maskini na hana future mussa ..alimchukia sana japo hakuwa na uwezo wa kumfunga kamba bintiye kuwa asiendelee kuwa na mussa, sasa aliona matunda ya kufanikisha alilopanga yapo waziii, wazi kabisaa!
Well mussa aliletwa hospitalini hapo na akakabidhiwa kwake ,yeye kama dkt wa kijiji jukumu lake lilikuwa ni kuangalia wagonjwa mahututi kama mussa ..alifurahi ,ndio alifurahi kuona sasa mbaya wake yuko mahtuti kitandani na sasa bintiye atakazana na masomo na sio mapenzi..
Kwa wakati mwengine moyoni aliwapongeza sana waliomfanyia unyama mussa ,alitamani hata awaone na kuwapa hela ya soda.
*****
Maureen alipopata tu taarifa kuwa mpenziwe mussa ameshambuliwa vibaya na yuko na hospitali alipata mshtuko na majonzi makubwa .haraka alitoka mbio mithili ya mwanariadha usain bolt kutoka Jamaica ,watu njiani walimshangaa walidhani huenda mtoto wa daktari amedata kidogo..
Mama mussa alipomuona mwanae tu hospitali alishikwa na uchungu mwingi, alipiga mayowe , Huyo ndo mwanae pekee aliyekuwa nae ,alimtegemea amtoe katika dimbwi kubwa la umaskini liliwazunguka ,alikuwa ndio tegemeo lao la pekee alilia alihuzunika ,kilichobaki ni kumuomba MUNGU
 
SIKU NITAKAPOKUFA ..01
AUTHOR: NEXT LEVEL.

Katika kila maisha ya binadamu kuna sehemu tunapitia na kukutana na majaribu ya kila aina mbalimbali, lakini kuna kuzaliwa kuishi na kufa, lakini Mimi siku nitakayokufa ...!siku nitakayokufa!..

Asubuhi na mapema jogoo anawika kuashiria kuwa watu waamke na kuanza shughuli zao za utafutaji, japo waliokereka na taarifa ya jogoo huyo kuwika kuashiria kuwa ni asubuhi kumekucha.

Mmojawapo alikuwa ni kijana mdogo Mussa matalu, alikuwa ni kijana wa miaka 16 tu, damu bado changa, mwili uliojengeka vizuri kutokana na kazi za suruba nyumbani kwao kwani yeye pekee ndiyo alikuwa kijana pekee wa kiume hapo kwao. "Wee mtoto utaendelea kulala mpaka saa ngapi?"

Huyo alikuwa ni baba wa damu wa mussa aliyejulikana kama mzee matalu, alikuwa mkali asiyependa mzaha kabisa wala utani wa kipuuzi.

Mussa aliamka harakaharaka kwani alielewa akiendelea kulala atachelewa shule na baba yake pia atamuadhibu.. Haraka akajiandaa na kutoka katika kibanda chake haraka kuelekea shule iliyojulikana kama WELLA SECONDARY.. Ilikuwa ni shule pekee kijijini hapo .
Oyaa mussa..!

Alikuwa na rafiki ake wa damu kabisa aliyejulikana kama Emanuel chigoni mwenyewe alijiita Emma uzo..Oya damu yangu nimepita kwenu bi mkubwa wako kasema umeshatangulia skuli nikaona nikufukuzie ..!

Mussa: aah we kila siku unachelewaa?
Imma uzo: aah mwanangu nilisahau kukuchana Jana si nilikuwa na mtoto Lydia?
Mussa: acha uzushi mtu mwenyewe utamuwezea wapi wewe?Ukweli ni kuwa mussa alipinga kwa nje lakini moyoni aliumia sana kwani hakuwahi kuwa na mpenzi tofauti na wanafunzi wenzake kama alivyo imma uzo angefanyaje na anawaogopa?

Alichoamua ni kubadilisha story maana imma hakuchelewa kuanza kumkandia kwamba kwanini hana demu..(mpenzi)

Well wanafika shuleni vijana hao wawili wa kidato cha NNE shuleni hapo . Baada ya mambo mengine kama usafi wanaenda mstarini (paredi) na kumkuta mwalimu mkuu amefura kwa hasira mithili ya chura mwenye mimba ..!

Kikawaida akiwa amekasirika basi huwa kunaKikawaida akiwa amekasirika basi huwa kuna jambo kubwa limemkasirisha ...alikuwa ni mwalimu DANIEL SHENDU.. Mkali mithili ya mbogo, ngozi yake nyeusi ya kung'aa, miwani yake ya macho aliyoining'iniza machoni pake ..hakuwa na utani hata kidogo.

Vijana kuna baadhi ya wanafunzi wanafanya shule kama ya wazazi wao, kwamba wanatenda wanavyojiskia "alianza mwalimu huyo"
Sasa basi ili kuonyesha mfano na onyo kwa wengine lazima sheria ifuatwe.

Erick mazinde..!, noel machemba.! Piteni mbele upesi.
Hangaikia maisha achana na kufa. Utakufa na kila kitu kwako kitakwisha kama wengine
 
Back
Top Bottom