JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,937
Wengi hamlijui jina hili maarufu la Kajole, kifupi huyu alikuwa mwanariadha na baadae mcheza mpira katika kijiji chetu, alichaguliwa katika timu ya mpira kwa sifa ya mbio, kocha akiamini kazi itakuwa kumtangulizia mpira na yeye kukimbia, jamaa huyu alikuwa na miguu kama mikono, tofauti na matarajio ya kocha akiwa kiwanjani kwa kuwa hakujua kudrible mpira basi mara nyingi alikuwa akikimbia hadi kuutangulia mpira na hivyo kuwa kazi bure tu. Mfano wa kajole umefanana kabisa na kitendo nilichowahi kukifanya mbele ya bibi yangu, enzi hizo tukiwa watoto tunazuiwa kula nje ya nyumbani, siku hiyo tunatoka shambani na bibi, tukapita kwa rafiki yake, tukapewa viazi na maziwa, chakula nilichokipenda/ninachokipenda sana, kwa mshangao bibi akala na mimi nikagoma na nikatoa sababu ile ile, siwezi kula kwa watu, bibi alihangaika sana bila mafanikio, sikula. Hadi leo nimebaki kuwa mtu wa msimamo mkali.