Siku niliyotongozwa na huyu Msichana wa Instagram (Shabiki wa Harmonize)

Sharobaro la jf

JF-Expert Member
Apr 23, 2020
237
323
Katika maisha hakuna kitu ambacho uwa kinaleta mshtuko kwa sisi mabaharia kama kutongozwa na demu mkali ambae na wewe ulikuwa unajiandaa kumtokea live, ilikuwa jumapili moja nipo zangu mtandao pendwa wa instagram naperuzi kwenye page ya mmakonde Harmonize Temboo.

Sasa nakumbuka Harmonize alikuwa amempost Ibrah yule msanii wake na mimi nikakomenti hivi nakumbuka nilikomenti, "daah huyu dogo anajua sana", sasa baada ya kukomenti haijapita hata dk tano mara naona demu kaja ku reply, " sanaa mimi nampenda", mwisho wa kumnukuu , basi ikabidi nimfuate Dm tukapiga stori mbili tatu akaniambia yeye yupo Zanzibar ila anatajaria kuja Dar baada ya wiki mbili hau tatu.

Hakika ni bonge moja la demu shepu kama lote kiukweli ameumbika kila idara, basi siku hiyo hatukupeana namba za simu, ikapita kama wiki mimi sijaingia insta kutokana na ubussy wa kazi sasa siku naingia insta nakuta kanidm anasema , "NIMEKUMISS SANA", nikamwambia mimi pia nipe namba zako ile nimekaa haijapita hata dakika mara sms hiyo mtoto katuma namba nikamwambia poa basi nikazisave sikumtafuta zaidi ya siku5 nikawa na mambo yangu, inshort wanawake wazuri hakuna kitu wanaumia kama wakupe namba halafu usiwatafute uwa wanajiuliza sana maana wanawake wanapenda sana kushobokewa sasa ukiwa mtu usie penda shobo utawafuna sana😊😊

Ile nakuja kumpigia akaniuliza nani nikamjibu mimi J, akaanza kulalamika ooh kwann umenidharau nimekupa namba hata kunitafuta, ikabidi nimpige uongo na kweli mtoto akaelewa, kukatisha stori aliniambia anakuja dar mda sio mrefu nikamwambia sawa basi siku sio nyingi mtoto akaja dar aliniambia anakuja kwa dadaake anakaa Tabata, mimi nipo mombassa pale so sio mbali na tabata, basi kweli akaja dar tukawa tunawasiliana tu kawaida hapo bado hatujaonana, atimae siku moja akanipigia akaniambia unaishi pekeeako?

Nikamjibu ndio, akasema kesho nakuja nitakuwa mgeni wako, daah nikajikuta napagawa nakumbuka siku hiyo nilikuwa na furaha isiyo ya kifani hata usingizi hauji, mara asubuhi hiyo, mtoto mida ya saa4 akanipigia ndio nataka nije, nikamwambia ukishuka mombasa niambie nije nikuchukue akasema poa, mzee mungu sio Juma mara baada ya mda mrefu kidogo sms hiyo nishafika, daah kidume nikakodi boda fasta, by the way nilipo na stendi sio mbali ilichukua dk 7 nikafika stendi sasa kazi ikawa kumtafuta kwa macho, katika kuangalia pale stendi kulikuwa kuna wadada watano sasa japo sura yake najua ila nilitaka kuona nae atanitambua haraka, mara nikamuona anatabasamu ,

Note:
Hatuwahi kuonana zaidi tu ya kuonana instagram,

Mtoto akaja hadi pale nilipo, mambo?, mimi poa nikamtania kumbe upo makini akacheka yeah ulijua sitakujua eeh, basi hao tukakodi boda hadi magetoni, kiukweli nilikuwa naona kama ndoto sikuamini kama kweli J nimepata toto kama ili, tukiwa gheto sasa nikawasha jiko fasta nikaanza kukaangiza mazaga, mtoto alikuwa yupo sebureni amekaa tu kWenye kochi anaangalia video, by the way nina ka tv kangu kadogo kakuzugia, basi msosi ukaiva nikamkaribisha, tukawa tunapiga msosi kila nikimcheki mtoto macho yote kwangu ananiangalia kimahaba, daah mtoto sura kama malaika, yani kimoyo nikawa nasema huyu jini nn maana sio kwa uzuri ule, baada ya kula, tukawa tunapiga stori hapo sijamtongoza,

Mara mtoto anaanza kuniambia J na jambo nataka kukwambia ila naona aibu,

Itaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom